Tunawakaribisha walio wasafi kutoka ndani ya chama cha magamba

Jaji

Senior Member
Sep 4, 2011
129
13
"Nimeupokea kwa furaha sana uwamuzi wa James Ole Millya kuhamia chadema na pia ninapenda kuwakaribisha wanaccm walio wasafi ndani ya chama chao wajiunge na chadema watuongezee nguvu ya kuharakisha mabadiliko" Mbowe anena
 
kumpokea mwanachama mmoja wakati waTZ wapiga kura mamilioni wamejaa si tija, cha msingi ni kupanua wigo wa vyama na kuwafikia wananchi wote popote walipo ili kujenga nguvu ya umma yenye sauti ya pamoja ya mabadiliko......
 
CCM wamenishangaza sana hasa Shigela,anasema huo ni utekelezaji wa sera ya kuvijua gamba,Hivi kwa nini walimwacha ashike nyadhifa zote hizo huku wakijua ni gamba!Nape nae kasema amekisadia chama chake!
Kweli ukiwa ccm unaweza pata mtindio wa ubongo!nasubiri maamuzi magumu ya whitehead!
 
"Nimeupokea kwa furaha sana uwamuzi wa James Ole Millya kuhamia chadema na pia ninapenda kuwakaribisha wanaccm walio wasafi ndani ya chama chao wajiunge na chadema watuongezee nguvu ya kuharakisha mabadiliko" Mbowe anena

Hajamkaribisha pia baba yake MILLYA? EDU. Siasa bhana. Eti hatuna historia chafu ya MILLYA teh teh teh. Inabidi sasa niwe narekodi matamshi ya Viongozi ili kuyatumia baadaye kwenye kuweka kumbukumbu sahihi. Sishanghai lakni kwenye uchaguzi nilisikia SLAA akisema ROSTARM AZIZ anakihusudu chama chao, kumbe alikwenda kutengeneza njia ya MILLAYA kuhamia CHADEMA. Karibu sana EL ugombee urais kwa kupitia CDMA. Mungu wabariki MILLYA, SHIBUDA, MPENDAZOE, LOWASA katika safari yao ya kukisadia CDMA.
 
"Nimeupokea kwa furaha sana uwamuzi wa James Ole Millya kuhamia chadema na pia ninapenda kuwakaribisha wanaccm walio wasafi ndani ya chama chao wajiunge na chadema watuongezee nguvu ya kuharakisha mabadiliko" Mbowe anena
Tamko hili la Mbowe limenisikitisha sana. Maana yake mtu yeyote bila kujali historia na rekodi yake akitoka CCM akajiunga CHADEMA basi uchafu wake wote unakuwa umekosheka? Sad. Mfadhili wa Millya si anajulikana? Inawezekana Milllya ni Yohana Mbatizaji amekuja CHADEMA kumuandalia Yesu njia. Basi kama Mbowe anataka kufanya 'harakiri' au 'suicide' ya CHADEMA ni kuwakaribisha Magamba ndani ya Chama bila tafakuri ya kutosha. Wapiga kura, hasa vijana, hawatakosa kuuuona unafiki huo. Na hapo ndipo imani na CHADEMA itaporomoka. Mbowe na CHADEMA wasipumbazwe na kubomoka kwa CCM wakasahau misingi na maadili ya Chama, kama ni siyo vigeugegu.
 
Napata wasiwasi sana namna wanavyopokelewa kwa shangwe wanaotoka CCM na kuingia upinzani.Si vema kukurupuka kuwapokea bila kufanya tafakari tunduizi.Kwanini sasa?pia kama wahusika wangepata nafasi walizokuwa wanahitaji,je wangetoka na kwenda upinzani?Mimi ninavyoelewa mtu mwenyewe anaweza kuwa chanzo cha mabadiliko bila kujali yuko chama kipi.
 
Tamko hili la Mbowe limenisikitisha sana. Maana yake mtu yeyote bila kujali historia na rekodi yake akitoka CCM akajiunga CHADEMA basi uchafu wake wote unakuwa umekosheka? Sad. Mfadhili wa Millya si anajulikana? Inawezekana Milllya ni Yohana Mbatizaji amekuja CHADEMA kumuandalia Yesu njia. Basi kama Mbowe anataka kufanya 'harakiri' au 'suicide' ya CHADEMA ni kuwakaribisha Magamba ndani ya Chama bila tafakuri ya kutosha. Wapiga kura, hasa vijana, hawatakosa kuuuona unafiki huo. Na hapo ndipo imani na CHADEMA itaporomoka. Mbowe na CHADEMA wasipumbazwe na kubomoka kwa CCM wakasahau misingi na maadili ya Chama, kama ni siyo vigeugegu.
sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi ili wapate kutubu...hahahaa..waache ata hao wachafu waje bana tutawasafisha etii..
 
wewe ruge kwa taarifa yako huyo millya alituma maombi toka mda sio chadema imekurupuka waulize wadau sio unaropoka tu mbona lowasa amekataliwa mpaka aombe rath kwa watanzania
 
Back
Top Bottom