Tunategemea uongozi zaidi kuliko malalamiko

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Siku za nyuma niliwahi kuweka makala hapa niliyokuwa najadili kuwa "Failures will always find an excuse for their misfortunes" na nikamhusisha Rais wetu katika kundi hili, niliongeza pia kuwa endapo hali ya ukame inayoendelea nchini itasababisha upungufu wa chakula, Rais wetu angehusisha ukosefu wa chakula na ama mwenyezi Mungu kutoleta mvua au CHADEMA ama Dr Slaa, ili mradi tu yeye na washirika wake wabaki bila lawama (angalau kwa maono yake). Siku chache baadaye Kikwete ameibuka na lawama lukuki badala ya kutuonyesha uongozi!

Upungufu wa Chakula nchini
Kama kweli Kikwete angelikuwa kiongozi anayestahili angeliliambia taifa hatua zinazochukuliwa na serikali yake kuhakikisha kuwa taifa hili haliendelei kutegemea kudra za mwenyezi Mungu na wahisani kupata chakula badala yake anakuja na malalamiko tu ya kusema kuwa tatizo la mvua halikusababishwa na yeye au serikali yake.. malalamiko ya namna hii ni malalamiko ya Failures, anataka tuamini kuwa mwanadamu hawezi kupambana na changamoto ya ukosefu wa maji ya kunyweshea mimea... Israel wanazalisha mwaka mzima ingawa Israel inapata mvua kidogo kuliko sisi.
Badala ya kutatua changamoto ya ukosefu wa maji amekuja na mradi wa kunufaisha matajiri na kuwaacha wakulima wakitweta kwenye lindi la umasikini, serikali yake imezilazimisha halmashauri zote nchini ziweke bajeti ya kununua matrekta kwenye bajeti zao za 2011/2012 ili waweze kuidhinishiwa maombi yao... HUU NI UFISADI NA HAUTATAUA UKOSEFU WA CHAKULA NCHINI!

Usalama wa taifa na amani ya nchi hii
Nilitarajia Rais aje na majibu ya kutatua changamoto inayotukabili ya taifa hili kutumbukia katika machafuko. Bila kuzitatua changamoto zinazoweza kuleta machafuko lazima tutaingia kwenye migogoro, Libya ni nchi ambayo raia wake wanapatiwa kila kitu na serikali lakini wamesema basi! Binadamu yeyote anapenda kuona haki inatendeka na ana asili ya kuwa huru, kama anafikiri kuwa kuendelea kuwalinda washirika wake wahalifu (DOwans, Kagoda, Meremeta, Mwananchi Gold, Radar, Presidential Jet, RITES, IPTL, n.k, n.k) wakati wananchi wengine maskini wakiendelea kuonewa na kunyanyaswa na vyombo vya serikali yake ndiyo amani na utulivu ambao watanzania wanautaka anajidanganya, Watanzania wanataka kuona haki ikitendeka na tumechoka na ngonjera na maigizo yake na CCM yake.... Hatutaki aendelee kutuhadaa kuwa hawafahamu wamiliki halali wa Dowans wakati anakula nao kila siku...

Umeme
Je serikali inataka tuamini kuwa Tanzania haiwezi kujitosheleza kwa nishati hii na kwa bei stahili? Tunasema hapana, inawezekana!
 
Sishangai kwa rais wetu kuendelea kulalamika na kutokujua suluhisho la matatizo ya watanzania kwani kuna wakati aliwahi kuulizwa swali,kwanini nchi yako ina rasirimali nyingi lakini wananchi wake ni masikini,akajibu kuwa hata yeye hajui na anashangaa.
 
Sishangai kwa rais wetu kuendelea kulalamika na kutokujua suluhisho la matatizo ya watanzania kwani kuna wakati aliwahi kuulizwa swali,kwanini nchi yako ina rasirimali nyingi lakini wananchi wake ni masikini,akajibu kuwa hata yeye hajui na anashangaa.

Ni kweli hajui kwani angekuwa anayajua angekuwa anayatafutia suluhisho badala ya kuilalamikia Chadema
 
Back
Top Bottom