Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
KWA JAMHURI YETU HII YA MUUNGANO WA TANZANIA - HIVI KWELI WANANCHI TU WAKWELI??
Kama mtu anaona ajabu kwa taifa kubwa kama nchi yetu Tanzania ambayo tumeishi kwa zaidi ya miaka 50 BILA YA KATIBA ilioandikwa na wananchi wenyewe basi nikuombe to ukanisaidie jibu la swali langu dogo to hapo chini.
1. Je, katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania, ni Zanzibar ndio iko Tanganyika au ni Tanganyika ndio iko Zanzibar???
2. Je, katika kujikumbusha kule sayansi zetu za jikoni pindi tunapopika chai, ukiunganisha glasi mbili za maji na glasi mbili za maziwa na kisha kukolezea majani chai; kile kinachopatkana mwisho wa mapishi hayo ya kimuunganiko itakua ni nini hasa??
a) Ni maziwa yalio na majani chai.
b) Ni maji yalio na majani chai.
c) Ni chai ya maziwa na maji pembeni.
d) Ni chai ya rangi na maziwa pembeni.
e) Ni chai ya rangi (maji pamoja na majani chai basi).
f) Ni chai ya maziwa (maji mchanganyiko na maziwa ikikolezwa majani chai basi).
Je, kwa wale mliowahi kushiriki sayansi ya kupika chai jiko walau hata kwa siku moja tu unafikiri ni jibu gani moja tu ambayo ni sahihi kuliko yote hapo juu??
Sasa, ukiwa umesimama katika vyatu vyake mwenzetu mpika chai hapo juu na tukirudi katika hali ya kawaida unaweza ukaelezea kwamba Jamhuri yetu tuipendayo saaaana ya Muungano wa Tanzania yenyewe itakua inachukua aina gani ya MUUNGANIKO ukipewa
(i) Serikali ya Zanzibar
(ii) Serikali ya Tanganyika na
(iii) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili vile vile ukachanganye madawa???
Kwa jibu lako lolote utakalokua umelipata kutokana na hili zoezi la pili, tukisimama kwenye ukweli unafikiri mambo yamejipandanga vizuri nchini mwetu???
SWALI:
Nawashilisha hoja huku nikiwaulizeni enyi Wana-JF mliosoma sayansi walau hata kwa shule za msingi na kushiriki kupika chai nyumbani wenzetu mnaona nini katika Muungano wetu ambalo watu hua hatudhubutu kuuzungumzia kwa kinywa kipana???