Tunafurahia mgao wa bilioni 8 dhidi ya bilioni 320 ? Tafakari

namimih

Member
Jan 4, 2012
64
20
Wana jamii forums nimesoma kwenye gazeti la IPP la tarehe 6 July, na kuna maelezo kuwa Unesco wamekubali kuachia kilomita 200 za mraba katika mbuga ya Selous kwa ajili ya uchimbaji wa uranium, kinachonishangaza ni baadhi wa wahusika katika kujenga nchi hii kufurahia na kuona ni hatua ya kuongeza kipato kwa Taifa hili la Tanzania kwa mgao wa bilioni 8 dhidi ya bilioni 320 kwa mwaka, kweli hii ndiyo haki au ndiyo aliyeturoga ameshakufa, naomba maoni yenu wana Jamii.
 
Wapatie jina lako wakuweke kwenye mgao, maana sasa ni kubeba kinachowezekana hata kwa damu ya watanzania. Ukiona ubatili njoo kwa Yesu tusubiri ufalme wake wenye usawa usioisha. Tumsifu yesu kristo aliyeshinda ubaguzi; ccm watakuua na presha maana wamajiandaa pia kuchukua nchi 2015
 
Mm sijakuelewa nidadavulie kwanza hivi tukiwanyima hiyo Mbuga ya Selous , hao wanyama watatuingizia Dola bilioni 320 kwa mwaka au tukiwanyima kuchimba na sisi tukachimba wenyewe tutapata dola hizo bilioni 320 kwa mwaka hebu funguka
 
Mm sijakuelewa nidadavulie kwanza hivi tukiwanyima hiyo Mbuga ya Selous , hao wanyama watatuingizia Dola bilioni 320 kwa mwaka au tukiwanyima kuchimba na sisi tukachimba wenyewe tutapata dola hizo bilioni 320 kwa mwaka hebu funguka


Ww ndio unatakiwa kufunguka coz wanachofanya ni overexploitation na mwisho wa cku madini yanakua exausted wakati hukupata manufaa hata kidogo mkuu. Mfano mrahisi ni Buhemba saizi wamekuachia mapango tu.
 
Back
Top Bottom