Tunachekwa, kwa jinsi tulivyokuwa miaka mitano iliyopita na miaka ya sasa

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,639
4,526
Habari hii nimeikopi sehemu..

TUNACHEKWA NA DUNIA NZIMA!!

Tumekuwa kicheko cha Dunia. Tunachekwa na kila mtu mwenye akili timamu kwa sababu sisi wenyewe tunachekesha.

Piga picha unamsimulia mtu mwenye akili timamu habari zifuatazo;

1. Miaka mitano nyuma nchi ilikuwa na umeme wa uhakika. Haukutosha nchi nzima lakini uliendelea kusambazwa kwa bei nafuu na uliokuwapo uliwaka kwa uhakika usiku na mchana.

Mwaka mmoja baadaye katika nchi ileile, mifumo ileile, vyanzo vilevile, hali ya hewa ileile umeme umegeuka lulu. Sio tu hauendelei kusambazwa au unasambazwa kwa bei ghari zaidi lakini hata uliopo hauwaki.

2. Miaka mitano nyuma maji yalikuwa ya uhakika Daslama na maeneo ya jirani. Kuna wakati watu walilazimika kujifunza namna ya kupunguza matumizi ili kupunguza bill lakini maji yalikuwepo lufufu, yaani ya kumwaga, full tank.

Mwaka mmoja baadaye katika nchi ileile, mifumo ileile, vyanzo vilevile maji yamegeuka dhahabu ya Geita. Kuyapata ni hadi usote!!

3. Miaka mitano nyuma, miwili kati yake Dunia nzima ilikuwa imefunikwa na Janga la corona. Watu hawakuzalisha kwa sababu hawakutoka ndani lakini hapa kwetu bei ya chakuka ilikuwa ya chini, unakula asubuhi, mchana na usiku. Sembe shilingi mia tisa kwa kilo, Mchele buku na mia mbili kwa kilo na Maharage nusu elfu na mia moja.

Mwaka mmoja baadaye tena Dunia ikiwa imefunguka kwa sababu hakuna corona na uzalishaji ukiendelea katika nchi ileile, mifumo ileile, hali ileile lakini Chakula hakinunuliki tena. Mchele umefika efu tatu mia tano kwa kilo. Sembe inapepea haikamatiki inakwenda buku mbili kwa kilo, Maharage nayo hayashikiki. Ni bei juu kwa juu!! Kula milo mitatu kwa siku imegeuka anasa.

4. Miaka mitano nyuma, miradi ya maendeleo ilikuwa inamea kama uyoga kila pembe ya nchi. Sio hospital wala shule, sio reli wala umeme. Meli Maziwa yote hadi baharini zilijengwa, kuanzia Victoria, Nyasa, Tanganyika hadi Kilwa. Barabara na madaraja ndio usiseme!! Ilikuwa ni bandika bandua, mara Ubungo interchange mara Tazara interchange, Tanzanite Bridge, Wami bridge, JPM bridge huko Mto Kilombelo,nk. Nchi nzima ilitapakaa miradi mikubwa mikubwa ya maendeleo!!

Mwaka mmoja baadaye miradi yote haieleweki tena imefikia wapi. Standard geuge iliyopaswa kuwa imekamilika sehemu ya kwanza haijulikani imeishia wapi. Tunasikia tu Waziri Mkuu wa nchi anakwenda Korea Kusini kukagua Mabehewa lakini mradi haujulikani umefikia wapi.

Stierglas Gorge (JNHP) umekwenda na maji, kifo cha Mende chali. Daraja la JPM lilikwenda na mwenyewe, bagenda bayoyo!! Meli ya mizigo imewashinda pale Maliasiri Mwanza imeanza kujiozea yenyewe, Waziri Mkuu anakwenda kunyang'anya Wakandarasi passport na kuwarudishia mwenyewe baada ya siku moja. Ni vichekesho pro max!!

Tumekuwa kicheko cha Dunia, tunachekwa na kila mtu. Nchi ileile, mifumo ileile, hali ileile isipokuwa mtu mmoja amekosekana, JPM. Kila kitu chali. He was so briliant! Heshima full tank kwake marehemu. Kwetu kuna msemo; hata mwenye kujisaidia njiani hukumbukwa!! Tunakukumbuka daima CHUMA; We miss you JPM!!

Halafu anatokea Shaka Hamdu Shaka amenawilishwa na vieite inayotokana na kodi zetu anasema tumuunge mkono Rais, tuiunge mkono CCM. Muulizeni Shaka, tumuunge mkono Rais kwa lipi!? Kwa kushindwa kusimamia na kutekeleza miradi!? Kwa kushindwa kusimamia stability ya umeme nchini!? Au kwa kushindwa kusimamia stability ya maji!? Shaka aseme tumuelewe perhaps anayo hoja ya msingi.

Tumuunge mkono Rais huyu kwa jambo lipi!? Kwa kushindwa kupanga bajeti ya chakula cha ndani au kwa kusafiri Amerika, Ulaya na Asia ndani ya muda mfupi!? Hapana. Unamuungaje mkono Baba aliyeshindwa kupangilia chakula cha familia!? Au, unaanzaje kuiunga mkono CCM katika dhiki hii, mateso haya, machozi namna hii na maumivu makubwa kiasi hiki!? Unaanzaje!?

Hapana. Haiwezekani. Mtu mwenye akili timamu akose umeme halafu aiunge mkono Serikali kwa kumnyima umeme, is that possible!? Yaani mtu akose maji halafu aiunge mkono Serikali kuwa kumnyima maji, inawezekanaje!? Kwamba mtu akose chakula kwa Serikali kushindwa kusimamia mfumko wa bei halafu aiunge mkono Serikali hiyohiyo kwa kumkosesha chakula.

Nadhani Shaka anajaribu kutukana watu hadharani!! Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuinga mkono CCM katika matendo machungu haya. Ni mgonjwa pekee anaweza kufanya jaribio hili. Kama unaiunga mkono CCM leo, katika dhiki hii nawe sio Waziri kama Nape, basi huhitaji vipimo vya kitabibu kujua kuwa wewe ni mgonjwa wa akili. You are so sick!! Unahitaji matibabu ya haraka, nenda hospital. Tunachekwa na kila mtu, tunachekwa na Dunia nzima!!

Mwalimu Mkuu (MM).
#FikraHuru.
#FikraHuru
 
Kila zama zinapita Kwa kasi Zama za nunuanunua wabunge na madiwani kukesha uwanja wa ndege serikali yote tukisubilia kupokea ndege zimepita Kwa Sasa tupo session ya kuzindua lipoti ya sensa na matozo kibao Kisha tunasema CCM ni Ile ile.
 
Nami niungane na hao wanaotucheka😀😄😂
Japo nacheka huku nalia.

Halafu kwa ujasiri anasema tatizo dogo watu wanalamika. Hasa watu wa Dar😄
Kwamba hayo matatizo ni kutokana na idadi kubwa ya watu.

Ama kwa hakika tutamkumbuka sana hayati JPM. Wanatoa majibu rahisi kwa matatizo magumu.

Na wanaharakati wengi wako kimya kwasababu walianza na sifa na mapambio kila mahali. 😄😂
Ncheke mie japo moyoni nalia!
 
Habari hii nimeikopi sehemu..

TUNACHEKWA NA DUNIA NZIMA!!

Halafu anatokea Shaka Hamdu Shaka amenawilishwa na vieite inayotokana na kodi zetu anasema tumuunge mkono Rais, tuiunge mkono CCM.
Huyo kijana mzururaji anayetembelea V8 iliyonunuliwa kwa kodi zetu Watanzania, mkimuona anapita mzomeeni. Hakuna chochote anachojua zaidi ya kutafuna kodi zetu kwa kueneza propaganda za uongo na majungu. Masikini akipata matako hulia mbwata!
 
Serikali inayotumia bilioni 600 kutuhesabu raia,ambao hata milo miwili ni tatizo!

Serikali inayotumia mabilioni kwa gharama za kututajia idadi ya watanzania,mpaka na helkopta zinarushwa!

Serikali ya matabaka Mawili moja la Walamba "Asali" na Walamba "Shubiri"

Serikali ya matabaka ya "Walala Hai" na
"Walala Hoi"

Serikali ya matabaka Mawili ya
"Wapanda Bodaboda" na "Wapanda V8"

Serikali ya matabaka mawili ya
"Royal Tour" na "Roho Tua"

Halafu anatokea Mtu asie na "SHAKA" na kutuambia tumuunge mkono "Queen Safari"

#mtanikumbuka.
FB_IMG_1667143072487.jpg
 
Isimee tu miradi Ile iliyo na tija,usilinganishe tu Hali ya mwaka mmoja na mwingine Ila kwa utafiti na vigezo,ikiwemo na taarifa sahihi.Kuanzisha mradi sii shida Ila unaihudumiaje na kwa gharama ipi kutoka wapi,hivyo ni sawa na ule usemi kuwa mwenye shibe hamjui mwenye njaa,ama anayeuona mradi wenye manufaa kwake hamwoni aliyepata madhila kwa mradi huo.Kwahio hapa ni nammna ya akili ya mtu kutazama Nini sawa Nini sio sawa.Na usimsemee wingine.Fikiria usemi huu ugumu wa Maisha ni kipimo Cha akili🥱
 
Huu ukweli walamba asali wataupinga.. lakini moyoni unawachoma kama sindano kwenye pulizo
emoji23.png
 
Kuna vitu umesahau,ngoja niviongeze.

Mwaka na ushee tulikuwa utaratibu wa kutekana leo hatusikii tena

Mwaka mmoja na ushee kulikuwa na mpango wa kukigeuza kijiji cha Chato kuwa Jiji kubwa kuliko Mwanza au Dodoma leo hatusikii tena ule ujinga CRDB Chato,Airport Chato,University Chato,NMB Chato,Takukuru Chato,Tanesco Chato,Hospital ya rufaa Chato,BOT Chato,National Park Chato,Bohari ya madawa Ya kanda Chato,VETA Kanda Chato,Mahakama Chato,Zimamoto Chato,Trafic light Chato.

Mwaka na zaidi WaTanzania wanaishi bila hofu.

Mwaka na zaidi hakuna kupora fedha za wafanyabiashara.

Mungu ni mwema siku zote.
 
Back
Top Bottom