Tuna wabunge 150 wa kuteuliwa ....

pigeni hesabu kila mbunge mmoja ana tu cost kiasi gani na natumaini katiba mpya itaondoa huu upuuzi

Kila mbunge aingie bungeni based on merit ya kuingia mle (kwa kuteuliwa kuingia mle na si kwa sababu ni mlemavu au mwanamke au anajuana na mtu)

Natumai hawa wanasiasa wetu pamoja na WAPINZANI wataunga mkono hoja ya kuondoa huu upuuzi

Wanawake watakubali kupunguzwa??

Kumbuka wengi wao ni VITU MAALUM
 
pigeni hesabu kila mbunge mmoja ana tu cost kiasi gani na natumaini katiba mpya itaondoa huu upuuzi

Kila mbunge aingie bungeni based on merit ya kuingia mle (kwa kuteuliwa kuingia mle na si kwa sababu ni mlemavu au mwanamke au anajuana na mtu)

Natumai hawa wanasiasa wetu pamoja na WAPINZANI wataunga mkono hoja ya kuondoa huu upuuzi
Katiba mpya iende mbele zaidi. Hata hawa wa majimbo tusiwaruhusu kujipangia malipo wanavyotaka. Kwanini tunamlipa Lusinde malipo zaidi ya Professor wa chuo?
 
Wanawake watakubali kupunguzwa??

Kumbuka wengi wao ni VITU MAALUM

Watawala wa sasa ni vigumu kukubali kuondoa viti maalumu,lakini ni ukweli hatuna budi kupunguza ukubwa wa Bunge kwa kuondoa viti hivi na kuunganisha baadhi ya majimbo ya uchaguzi.
 
Viti maalum 105
BLW 5
Washikaji wa rais 10
Mwansheria mkuu 1
JUMLA 121
Sijaelewa umetumia vigezo vipi kupata hiyo idadi ya 150. Maana nasikia viti maalumu ni 103,mpaka sasa wa kuteuliwa na Rais ni 7 kama siyo 8,sifahamu idadi ya wanaowakilisha BLW Zanzibar ni wangapi na unaongeza AG! Kuna utitiri wa wabunge toka Zanzibar ambao idadi ya wapiga kura wao wanazidiwa na vitongoji huku bara. Wengi wa hawa wapo bungeni kuzomea na kugonga meza wakishirikiana na wabunge wa Tanganyika toka majimbo masikini zaidi huko kusini,pwani na kati!
 
Lack of principle gani?

Umetueleza tatizo lako ni wabunge ambao hawajaingia kwa kupigiwa kura, mimi nimekuunga mkono, nikasema kweli kabisa na wafutwe, halafu baada ya hapo, wawaundie majimbo mapya ya Mabwepande Mashariki na Mabwepande Magharibi, Kijichi Kaskazini na Kijichi Kusini, mpaka Dar iwe na wabunge 20, lakini wote wameingia kwa kura.

Utakuwa umetatua tatizo lako la wabunge ambao hawaingii "based on merit."

Au?

mi naona wabunge wengi tu hawana la kufanya na huu mfumo wa utawala uliopo zaidi ya poroja nyepesi na marupu rupu kibao. Majimbo ya ubunge kwa style yako ni siasa tupu na mzigo ule ule. Mbunge wa Buguruni kwa malapa atasema nini bungeni zaidi ya petty issues ambazo diwani wa kata anaweza kuzifanyia kazi?

mi naona majimbo yachorwe upya kutokana na uwinao wa wingi wa watu, rasilimali, na ukubwa wa eneo. hizi wilaya zitengenezwe upya kuendana na mahusiano ya kiuchumi na mfumo mpya wa utawala. Tuwe na wakuu wa mikoa wanaochaguliwa na wananchi (hata kama itaongeza ukabila ni sawa kwani ukabila tayari upo mfano mtu wa pwani hawezi pata ubunge usukumani, uchagani, mbeya vijijini, kigoma, musoma au bukoba n.k) hatuwezi kuogopa kitu ambacho ni halisi na kipo.

Kila wilaya itakua na mbunge mmoja (mfano) ondoa hawa political DCs na mpe MP resources zote za ofisi ya DC, (ukitoa masuala ya kiusalama kama Polisi etc ambayo yatakua huru chini ya wizara ya mambo ya ndani na RPC ili kuvizuia kutumika kisiasa)

Huku ukiwa na fixed cabinet posts za professionals peke yake (wasiokua wabunge) hapa tutaona Tanzania inafika mahali.
 
Lakini what does CHADEMA say about this

I dont trust CCM kuondoa huu upuuzi

so our hopes ziko CHADEMA je watakubali huu upuuzi au watakuja na radical ideas za ku reform haya mambo?


Viti maalum ni UJINGA kwa sasa HAVITAKIWI sanasana Awepo mwakilishi wa walemavu wote mmoja tu wengine wote tupambane hadharani. HAYA NI MAMBO YA KATIBA ITAKAVYOELEKEZA cyo chadema wala ccmizi
 
Watawala wa sasa ni vigumu kukubali kuondoa viti maalumu,lakini ni ukweli hatuna budi kupunguza ukubwa wa Bunge kwa kuondoa viti hivi na kuunganisha baadhi ya majimbo ya uchaguzi.

vibaki 10 tu

wengi wao ni mizigo na wabwabwajaji tu mule ndani na ushabiki usio na kichwa wala miguu
 
wakuu tuache utani kweli hawa wabunge viti maalumu nimzigo sana kwetu walipa kodi!

kuna mtu hapa anaweza kueleza faida yao ilihali kila jimbo linamwakilishi?
 
Back
Top Bottom