Tumsaide huyu mtanzania mwenzetu

goodhearted

JF-Expert Member
Feb 15, 2015
943
1,110
Ni mtumishi wa umma. Mshahara umeingia kupitia ac ya bank flani naihifadhi. lakini ukawa na nyongeza ya shilings kiasi cha milioni plus. Kutokana na hicho kiasi kilichongoozeka akaunti yake imeshikiliwa. Hawezi hata kuangalia salio.

Kila alipokuwa anaenda kuwaomba waachie account yake ni danadana kuwa baada ya masaa 24 kila kitu litakuwa ok lakini hola.

Ijumaa iliyopita alienda tena kuomba waiachie acount yake. Walimlaghai kwa maneno matam tena mbele ya bank manager kuwa kufika jumatatu kila kitu kitakuwa sawa. Lakini mpaka leo mambo ni yale yale tu. Acount bado haisomi chochote

Kinachotia mashaka ni pale alipoomba bank statement alikuta pesa yake ya mshahara yote haipo ikiwa ni pamoja na kiasi kilichokuwa kimeongezeka. Alikuta pesa aliyoiacha kabla ya mshahara haujatoka. So bank statement zote anazo za baada tu ya mshahara na hii ya juzi aliyokuta mshahara haupo wote na kiasi walichokuwa wameongeza.

Ameongea na customer care makao makuu wanamdirect tawini kuwa case yake inatatuliwa hapo.

Amepambaana kwa gharama kila siku anatoka kijijini kwenda mjini kwa hilo jambo lakini hola

Wataalamu wa mambo haya hii kisheria imekaaje
 
Tujifunze kuwa wakali kwenye haki zetu na mali zetu....

Naamini hii kesi inaweza kumpa pesa nzuri tu kama ushahidi wa sauti na hizo slip anazo...

Au unaweza kumtafuta rafiki au mtu mwenye biti kidogo akaenda wakoromea.... Muda mwingine ukichaa huwa nafaida.
 
Isiwe iliingia kimakosa jamaa kaila Sasa anatakiwa kulipa hiyo 1M.Tunatakiwa kujifunza kama ela imeingia kwenye account Yako na haujui ilikotoka basi kuwa na subira.
Hajachukua chochote kwenye mshahara. Ni ile mshahara unaingia unajiridhisha kwa kuangalia salio then unaitafuta ATM machine ilipo unapofika ndio unajikuta huwezi kufanya chochote
 
Hajachukua chochote kwenye mshahara. Ni ile mshahara unaingia unajiridhisha kwa kuangalia salio then unaitafuta ATM machine ilipo unapofika ndio unajikuta huwezi kufanya chochote
Ok! Nyongeza ya Milioni plus hapo iliniletea shida.Ukienda Bank kinyonge wanakupapasa.Chimba mkwara Kwa huyo Manager hapo alafu aone.
 
Huyo jamaa ni mpumbavu ambaye hajui haki zake. Yaani kila kesi utasikia ni mtumishi wa umma kadhulumiwa na benki. Kwanini isiwe wafanyabiashara? Yaani hapo aipeleke kesi mbele avune hela kwenye hiyo benki.
 
Nahisi kuna jambo hujaliweka wazi,au alipita na pesa iliyo ingia kimakosa?
 
Huyo jamaa ni mpumbavu ambaye hajui haki zake. Yaani kila kesi utasikia ni mtumishi wa umma kadhulumiwa na benki. Kwanini isiwe wafanyabiashara? Yaani hapo aipeleke kesi mbele avune hela kwenye hiyo benki.
Hata mimi nimemshauri hivyo ila hajui aanzie wap
 
Back
Top Bottom