SOFTWARE Tumia Mfumo(System/Erp) moja kuendesha Biashara yako(Odoo Erp)

mkushite

JF-Expert Member
Sep 2, 2021
623
1,467
Hapo zamani, TAASISI au COMPANY zilikuwa zinatumia mifumo(systems) nyingi (zaidi ya mmoja) katika kuratibu shughuli za kila siku. Kwa Mfano Taasisi au Kampuni moja yenye departments tano(5) (Finance, Human resources, Sales, Marketing, Procurement e.t.c) lazima iwe na mifumo(systems) tano(5). Na kila system ilikuwa inajitegemea yaani hizo system zote tano(5) haziongei pamoja na hazibadilishani data.

Pia enzi hizo mifumo iliyokuwa inaunganisha departments zote ilikuwa ni ya ghali sana. Yaani. changamoto kubwa ya hizo systems ilikuwa ni gharama manunuzi na uendeshaji kuwa kubwa sana. Makampuni na Taasisi kubwa ndizo zilikuwa na uwezo wa kununua hiyo mifumo. Mfano wa mifumo ya zamani ambayo ni Ghali ni kama SAGE Erp na SAP Erp.

Kulingana na maendeleo ya Teknolojia, ikazaliwa ODOO ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo sokoni kwenye uendeshaji wa biashara. Kwa kutumia ERP aina ya Odoo sasa unaweza pata kila kitu ambacho kinapatikana kwenye SAGE, SAP na ERP zingine kwa gharama nafuu sana. Na kizuri zaidi kwa Odoo unaweza ukamodify source codes ili zifanye kazi kulingana na biashara/taasisi yako. Odoo inaunganisha departments zote zifanye kazi pamoja na ziwasiliane pamoja na inatoa reports bora kusaidia kutoa maamuzi sahihi wa biashara.

Modules kuu ya Odoo ni Accounting full package ambayo inatengeneza invoices, register bills, accounting reports(profit and loss, balance sheet, cash flow, trial balance e.t.c). Pia module ya accounting iko connected na modules zote zinazohusiana na fedha kama sales, payroll, expenses, inventory e.t.c Human resources ni module nyingine kubwa ambayo ina sub modules kama payroll, attendance, employees, leaves management, e.t.c. Modules zingine ni Sales, CRM, Procurement, Inventory, Loan management, Expenses, e.t.c

Odoo inaweza fanya kazi kwenye (Small,Medium, Enterprise) yoyote mf. Shuleni, Hospitalini, Migahawa, Bar, Hotelini, Micro finances, Sheli, Car rental companies, consulting firms, Financial firms, Telecoms, wizarani e.t.c.

Mimi ni mtaalam wa ERPs na nimefanya kazi za Odoo kwa zaidi ya miaka mitano(5). Wasiliana nami kama utaitaji kufunga Odoo Erp kwenye biashara/ofisi/kampuni/taasisi yako
 
Back
Top Bottom