Tumeshindwa kila mahala

dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,725
255
Ndg.WanaJF takribani miaka hamsini baada ya uhuru tumeshindwa hata kimojawapo kati ya haya: Kiuchumi, Kisiasa na kijamii(kiutamaduni).

Kiuchumi: Mwalimu Nyerere (R.I.P) alijitahidi kukuza uchumi katika hali ya shida kubwa pale ambapo hakuwa na wataalamu wa kutosha. Alifungua viwanda sehemu mbalimbali katika nchi hii na kutoa fursa za ajira kwa ambao walikuwa wamesoma japo elimu ya msingi, sekondari na vyuo kwa wakati huo. Pamoja na changamoto zilizokuwepo kati ya nguvu ya west na east na itikadi zilizokuwepo viwanda vilishamiri. Awamu ya pili, tatu na nne tunajua yaliyotokea na viwanda kufa kabisa. Tumebaki na matamko uchumi unapaa huku tukiwa ombaomba pamoja na kuwa awamu ya tatu na nne wameingia mikataba ya uchimbaji wa migodi tofauti na awamu ya kwanza. Tayari pia tumeshuhudia MAKULEWA wameanza kuwekewa pesa huko nje zikiusishwa na gesi na mafuta katika nchi hii hii.

Kisiasa: Tumeshuhudia matukio yanayousishwa na mauaji yanayousishwa siasa, katiba mbovu, kuweka kura zilizopigwa kwenye ma-hotpot, kuandika majina ya wapiga kura kunakofanywa na viongozi wa mashina wa CCM, kuchakachua kura waziwazi kwa pendeleo, wabunge kutangazwa washindi kwa mtutu wa bunduki, miswada kupita bungeni kwa ushabiki wa vyama hata kama ni mibovu na haina tija kwa nchi n.k

Kijamii (kiutamaduni): (1) elimu - WanaJf tunaona tumeshindwa kabisa kutoa elimu bora kwa watoto wa kitanzania. Sote tumeshuhudia wanafunzi 5000 kujiunga na sekondari pasipo kujua kusoma wala kuandika na tumeshindwa kutoa elimu ya uraia ili watanzania wote waishi kama ndugu.
(2) dini: Tumeshuhudia vyombo vya habari vya dini nyingine vikiwakashifu watu wa dini nyingine. Vyombo hivyo ni magazeti na radio. Tumeshuhudia inayoitwa mihadhara ya kidini ikiandaliwa kukashifu dini nyingine kwa makusudi kabisa.


NINI CHA KUFANYA SASA???
 
Back
Top Bottom