Tumemuaga Rais Kikwete ahadi ikiwa haijatimia.

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,911
1,312
Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ameitumia sikukuu ya Mei Mosi kuwaaga wana-mwanza. Akiwa na bashasha na uchangamfu mkubwa alionyesha kufurahia uwepo wake Mwanza. Hakutaka kujikimbusha histori mbaya iliyomkuta hapa Mwanza. Kwanza ni pale alipovamiwa jukwaani mwaka 2005 akiwa kwenye kampeni. Pili ni pale alipoanguka kwenye mkutano na viongozi wa dini. Mh Dr. Jakaya Kikwete ametuaga wana-mwanza bila yaqkitimiza ahadi yake ya kuifanya Mwanza kuwa California ya Tanzania na Afrika Mashariki. Ni aibu lakini ndio ukweli wenyewe ndani ya utawala wake hata barabara ya njia mbili hatujajengewa. Ni karibu sana kutoka Mwanza kwenda kwenye miji mikubwa ya ukanda huu wa maziwa makuu (mfano Kampala, Bujumbura, Arusha, Nairobi, Lubumbashi, Kigali na Dar es salaam) lakini cha kushangaza ni hali ya uwanja wa ndege. Meli kwa ajili ya usafiri wa ziwa Victoria bado ni kitendawili.Treni bado haijawa usafiri wa uhakika kwa mizigo na abilia. Mh. Dr. Jakaya umeondoka bila kuigeuza Mwanza kuwa California. Ahadi ni deni lakini hii yetu itabidi tusamehe.
 
we umeliona la mwanza kuna la kuifanya kigoma dubai

Aende zake na maccm yake yaliyojaa maigizo hususan napi na kinanna
 
Ha ha ha ha ha ha
kuna muda unatakiwa ucheke japo yanasononesha
Sio jambo geni hilo wenzenu walidanganywa itakua Dubai ya Afrika bado watakuja mtadanganywa mpaka mtakufa na watoto wenu ila kumbuka mabadiliko ni wewe kuikataa ccm oktoba ni kukataa uongo wa ccm na kiongozi wake kwa kuwadanganya
 
Wengine wametumia hadi kivuli cha kumuita shemeji nao wameambulia patupu
 
Uongo nayo dawa, JK na CCM ni waongo kweli kweli, lakini ni kwa vile tunahitaji waongo kuongoza nchi
 
wahenga walishasemaga kuwa... wajinga ndio waliwao. sisi wananchi tumeyakubali yote hayo na basi tuvumilie tu. au la yakikukera haya basi tukutane october.
 
Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ameitumia sikukuu ya Mei Mosi kuwaaga wana-mwanza. Akiwa na bashasha na uchangamfu mkubwa alionyesha kufurahia uwepo wake Mwanza. Hakutaka kujikimbusha histori mbaya iliyomkuta hapa Mwanza. Kwanza ni pale alipovamiwa jukwaani mwaka 2005 akiwa kwenye kampeni. Pili ni pale alipoanguka kwenye mkutano na viongozi wa dini. Mh Dr. Jakaya Kikwete ametuaga wana-mwanza bila yaqkitimiza ahadi yake ya kuifanya Mwanza kuwa California ya Tanzania na Afrika Mashariki. Ni aibu lakini ndio ukweli wenyewe ndani ya utawala wake hata barabara ya njia mbili hatujajengewa. Ni karibu sana kutoka Mwanza kwenda kwenye miji mikubwa ya ukanda huu wa maziwa makuu (mfano Kampala, Bujumbura, Arusha, Nairobi, Lubumbashi, Kigali na Dar es salaam) lakini cha kushangaza ni hali ya uwanja wa ndege. Meli kwa ajili ya usafiri wa ziwa Victoria bado ni kitendawili.Treni bado haijawa usafiri wa uhakika kwa mizigo na abilia. Mh. Dr. Jakaya umeondoka bila kuigeuza Mwanza kuwa California. Ahadi ni deni lakini hii yetu itabidi tusamehe.

we umeliona la mwanza kuna la kuifanya kigoma dubai

Aende zake na maccm yake yaliyojaa maigizo hususan napi na kinanna

Ha ha ha ha ha ha
kuna muda unatakiwa ucheke japo yanasononesha
Sio jambo geni hilo wenzenu walidanganywa itakua Dubai ya Afrika bado watakuja mtadanganywa mpaka mtakufa na watoto wenu ila kumbuka mabadiliko ni wewe kuikataa ccm oktoba ni kukataa uongo wa ccm na kiongozi wake kwa kuwadanganya

Vipi kuifanya msoga kuwa kama japan kwa ujenzi wa viwanda na kule bagamoyo kuifanya kuwa bandari kuu ya AFRICA???:what::what::what::what:
 
Back
Top Bottom