Tumbo kuunguruma, nini tatizo

Mh utakuwa na vidonda mmi nasumbuliwa na hali hyohyo juzi tu nimeenda pima nimekutwa na vidonda vya tumbo kapime kwanza
mimi nimepimwa choo nikakutwa na amiba nimemaliza dawa bado tumbo linaunguruma muda mwingine nahisi kama maumivu yamgongo kuchoma kuchoma kwa mbali sijui kipimo cha endoscopy shiling ngapi sina pesa aisee
 
Habari zenu ndugu zangu:

Naombeni msaada wenu juu ya hili swala, ni kwa muda mrefu tumbo huwa linaunguruma haswa wakati wa usiku kukiwa na baridi,

lakini pia nimejigundua kila ninapomaliza kufanya tendo la ndoa tumbo huunguruma sana, hata ikiwa mchan na kama nikifanya usiku ndo kabisa mpaka mm mwenyewe naogopa, lakini hata haliumi na hali hii ina miaka mingi,

sasa sijafahamu inasababishwa na nn, pia nifanyeje kukabiliana na hali hii.

Nitashukuru kwa msaada wenu wana ndugu.
 
Kunywa maji ya kutosha kabla na baada ya KULA ama kufanya TENDO LA NDOA.

Jizoeshe hivyo na utayaona mabadiriko.
 
Hiyo ni gesi unakaa muda mrefu pasipo na kula tumbo linaingia hewa ya gesi kunywa maji ya Uvuguvugu kila wakati na ule punje 2 za kitunguu saumu meza na maji ya uvuguvugu gesi itakwenda zake.
Ahsante hii inawezekana mana huwa naona uvivu kula mpaka nikajihisi nna minyoo, itabidi nifanye hivyo na niwe najilazimisha kula japo huwa sipati hamu ya kula hata njaa inapouma but kama ndio sababu itanibidi nijilazimishe huku nikiendelea na hyo dawa
 
Tatizo hilo usiliingize kwenye afya ya uzazi tumbo la chakula ndio linanguruma ni vitu vipo tofauti kabisa, ni kwamba una gas nyingi tumbo na huenda unakula vyakula vyenye gas unaiongeza ndio maana tumbo linanguruma hiyo ni gas tu ndugu tumia omeprazole kwa mwezi mmoja na relcer itaiweza kupungua au kuisha kama utazingatia vyakula visivyokuwa na acid
 
Ahsante hii inawezekana mana huwa naona uvivu kula mpaka nikajihisi nna minyoo, itabidi nifanye hivyo na niwe najilazimisha kula japo huwa sipati hamu ya kula hata njaa inapouma but kama ndio sababu itanibidi nijilazimishe huku nikiendelea na hyo dawa
Kapime Minyoo huend unayo Minyoo inayo kusababisha usisikie njaa unaweza kula nyanya mbichi ukatia kidogo na unga wa pilipili mtama ukala inasaidia kuuwa minyoo iliyo tumboni.

Na pia kula kipande cha Tangawizi mbichi au chai yake utaweza kujisikia hamu ya kupenda kula.Au Nenda duka la dawa aka Pharmacy ukanunuwe vidonge vya Vitamin B Complex uwe unakula kila siku kidonge 1 baada ya kwisha kula chakula hivyo vidonge vitakusaidia kukukufanya uwe unajisikia hamu ya kula.
 
Kunywa Maji ya Uvuguvugu na punje 2 za kitunguu saumu gesi itakwenda zake tumia kutwa mara 3 kw siku 3
Mkuu mzizi mkavu, nina tatizo na kuwa kila nikikojoa nahisi makalioni kuna chomachoma mpaka karibu na kiuno.

Alafu sometime najiona kama kuna vitu vinapitapita mwilini haswa kwenye mbavu,tumboni,mgongoni na hata miguuni pia.
 
kapime kwanza hospitali figo lako je lipo sawa? kama hawajaona kitu utakuwa una mambo ya uchawi mwilini mwako. Kuhisi vitu vinatembea mwilini mwako itakuwa ni Dalili ya mambo ya uchawi huenda pia una shetani mbaya anaye kusmbuwa mwilini mwako. jichunguze pia unapo lala usiku huwa unaota ndoto za aina gani?
 
Ahsante sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom