Tulivyokuwa tukiiba almasi mgodi wa Mwadui na wenzetu kuuawa

Hii ilikuwa ni miaka ya '90 mwanzoni, tukitokea pembezoni mwa mgodi wa Mwadui, tulifahamika kwa jina la "Wabeshi".

Zana zetu za kazi ilikuwa ni sululu, chepe na majembe yaliyonolewa sana, tulikabiliana na jeshi la polisi la mgodi wa Mwadui waliokuwa na kikosi cha farasi na mbwa wenye uweredi mkubwa sana na mafunzo ya hali ya juu.

Nakumbuka siku rafiki zangu wawili walivyouwawa kwa kuumwa na mbwa sehemu za siri na jirani yangu Jilingumika Masufulia alivyopigwa risasi ya kichwa akivuka fensi ya mgodi wa Mwadui.

Almasi tuliibatiza jina la "ng'ana", na ilikuwa hauwezi kwenda kuiba bila kuchanjwa chale za kwapani na matakoni. Mganga wetu mkubwa alikuwa ni Mzee maarufu sana wa Kijiji cha MWIGUMBI, Nje kidogo ya mgodi, huyu ndio mzee aliyetupa dawa na kinga wakati wa kwenda kuiba almasi,wakati huo nikiwa na miaka kama 16 tu hivi, nimemaliza darasa la saba shule ya msingi Luhumbo. Tajiri wetu mkubwa alikuwa mwarabu wa Maganzo maarufu kwa jina la Abeid, huyu alitupikia vitumbua na chai kabla ya kwenda mgodini kuiba almasi, na chote tulichokipata tulipeleka kwake kama tajili na kupata ujira wetu.

Tajiri Abeid hakuwa mtu "rahisi rahisi", yeye mganga wake alikuwa anatokea kijiji cha Idukilo, mganga hatari sana aliyekuwa na madawa ya kisukuma ambayo yaliwabadilisha watu na kuwa mbwa mwitu au nyani pindi walipoingia ndani ya mgodi kuiba, tajiri Abeid alikuwa anaishi kijiji cha Maganzo, akiwa na duka la bidhaa la kuzugia,lakini deal zake kubwa ilikuwa ni kununua almasi na kuziuza kwa matajili wakubwa wa Mwanza na Shinyanga mjini.

Almasi zote tulizopeleka kwa Abaeid zilikuwa zinatunzwa na mbuzi dume, beberu mkubwa aliyekuwa anazimeza na kuzihifadhi tumboni hadi mteja atakapokuja,hata polisi wakifika na ku-search vipi,wasiongeziona almasi kwani beberu alikuwanazo tumboni,hakuwa beberu wa kawaida maana alikuwa na chumba chake na alilala ktk godoro. Mbuzi hakula nyasi wala majani ya miti, bali vitumbua, chai, ugali na "maparage". Kipindi hicho hatukuwa na ruhusa ya kuongea juu ya mbuzi yule, tulimuogopa na kumtii zaidi hata ya kiongozi wa msafara wa wabeshi.

Tajiri wa uhakika alikuwa Fantomu wa maeneo ya Mipa,huyu hakuonana na sisi wabeshi maana tulikuwa watu "wadogo" sana, bali alipitia kwa Abeid na waarabu wengine wa Maganzo.

Maisha ya kuwa "mbeshi" yalikuwa magumu sana,maana kifo na kujeruhiwa ilikuwa ni njenje,tuliuwa na kuuwawa. Polisi, mbwa na farasi waliokuja bila tahadhari waliuwawa kwa chepe zilizonolewa na mapanga. Tukio moja nalokumbuka ni la mwenzetu Masunga kumuua mbwa wa polisi kwa kumkata na chepe mdomoni na kuutenganisha mdomo pande mbili.

Wenzetu wengi walikufa tukiwa bwawani tukiiba,wengi walizama kwenye tope liliotokana na mabaki ya kusafishwa kwa almasi ambayo sisi tulikuwa tunakwenda kuchota na kuchekecha upya,bwawa hili la tope zito lilukuwa karibu na "sorting area" ambayo ililindwa kwa kiasi kikubwa sana. Lakini kwa imani ya chale za mganga wa MWIGUMBI na Idukilo watu wengi tulikuwa na ujasiri wa kukatiza kila mahali bila hofu.

Wengi waliojeruhiwa na kuumizwa walilazwa ktk hospitali ya Mwadui.Siku nilipoamua kuacha "kazi" hii na kurudi shule,ilikuwa ni siku hatari sana... binamu yangu kipenzi Luhende alipigwa risasi ya kichwa na ubongo kutawanyika, mbele ya macho yangu Luhende alikufa bila hata kuomba maji. Askari wakiwa umbali wa kama mita 100,sisi tukiwa na makarai yetu na chekecheke tukiambaaambaa pembeni ya reli maeneo ya SONGWA ktk njia ya mzunguko kuelekea Maganzo tuliwekwa katikati yao na kuuliwa baadhi yetu. Katika kundi la wabeshi kumi, saba walikufa hapo hapo..watatu walifia hospitali na mimi pekee nilipona baada ya kujitumbukiza kwenye bwawa la maji ya kunywea mifugo, niliogolea chinichini kwa chini na kuibukia upande wa matete, ambapo nilikaa ndani ya maji zaidi ya masaa 12 bila kutoka..nikiwa nimetoa pua tu na kujishikiza kwenye "msitu" wa matete.

Kikosi cha polisi wenye mbwa na farasi walizingira bwawa lile mpaka usiku wa kiza kinene, wakaamini nimeshakufa na kuzama hivyo wangefika kesho yake kukuta ninaelea baadaya kufa.Katikati ya kadhia ile ndipo nilpoona kazi ya ubeshi si lolote si chochote, zaidi ya mwili kujaa chale za tako mpaka kwapani.

Pesa tuliyopata ilishia mnadani Maganzo,ambapo tulikula na kunywa. Hatimaye niliamua kurudi kijijini Luhumbo,nikakariri tena darasa la saba kwa jina la mtoto wa mjomba aliyeacha shule na kwenda kuchunga na kulima vibarua maeneo ya Muhunze. Nilikuwa mkubwa kuliko wote darasani lakini sikukata tamaa. Nilisoma kwa mwaka mmoja wa darasa la saba kwa bidii na usongo na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na shule ya Tabora Wavulana.

Kwa mara ya kwanza napanda train kwa "warrant" ya serikali, station ndogo ya Songwa kupitia Shinyanga kuelekea Tabora. Nakutana na Afande Chacha kwenye geti la Tabora boys, ananipokea kwa kichurachura na bakora za mgongo bila sababu, wakati huo Tabora Wavulana ipo chini ya jeshi. Mwanzo naona maisha ya ubeshi ni afadhali kuliko shule ya aina hii..mchakamchaka na Afande Chacha kila asubuhi kupitia Kwihala mpaka Kipalapala.Juma la kwanza natamani kutoroka lakini sijui mahali pa kuelekea, shule ipo nje ya mji na mfukoni sina nauli.Baada ya mwezi ndani ya kombati ya kijani mwanajeshi,inatangazwa disko ya "welcome form one".

Disko langu la kwanza maishani,nakutana na watu wenye lafudhi nzuri na Kiswahili kilichonyooka, mimi nashindwa kuongea mbele za watu sbb lafudhi yangu ni "ngumu" kusikika na kueleweka. Ninapata marafiki toka pande mbalimbali za Tanzania. Kapufi wa Mpanda na Mwaisengela wa Mbeya wanakuwa marafiki zangu kwenye bweni la Kimweri. Miaka minne ndani ya Tabora,wao wanaita Mboka Manyema..ninabahatika kurudishwa tena kidato cha tano na cha sita,baadae naamua kuingia Jeshi bila kwenda chuo Kikuu. Ninalitumikia jeshi kwa muda mrefu, safari yangu ya Lebanoni kusiamamia amani inanirudisha nyumbani na kukuta mke wangu akiwa na mimba ya miezi sita na mimi nilikuwa nje kwa mwaka mzima.

Nikukumbuka nilipotoka,shida na vurugu za kuwa mbeshi....Oooops!!! Naona dunia sio mahali salama pa kuishi
Umenikumbusha kitambo ndugu, enzi za wabeshi, nilikuwa naona Tu miili Yao ikiletwa na land rover pale mwadui hosptali. Namkumbuka Sana abeid tajiri wa maganzo na phantom. Umenikumbusha mambo mengi, songwa kwenye bwawa pale,
 
Umenikumbusha kitambo ndugu, enzi za wabeshi, nilikuwa naona Tu miili Yao ikiletwa na land rover pale mwadui hosptali. Namkumbuka Sana abeid tajiri wa maganzo na phantom. Umenikumbusha mambo mengi, songwa kwenye bwawa pale,
Mkuu upo sahihi,zaidi ya hospital ya Korandoto,hospital nyingine iliyokuwa na huduma nzuri zaidi ilikuwa ya Mwadui Mine.Pale jamaa zetu wengi waliojeruhiwa na mbwa au kupigwa risasi walipelekwa mle kutibiwa wakiwa ndani ya pingu.Mule Mwadui ndani kulikuwa na Hospital mbili...Government Hospital na Private,watu wetu wengi walikuwa wanalazwa pale Gvt Hospital.

Lile bwawa la Songwa lilikuwa na beach fulani,ambapo kulikuwa na club ya usiku inaitwa Songwa Club!Pale ilikuwa njia yetu kuingia mgodini mkuu momo j seme nyie vijana wa Mwadui mlikuwa mayai mayai sana,mnakaa na almasi mnaitazama tu
 
Waambie hao mkuu Ntaluke.N. wengine wanafikiri tunayoyaeleza hapa ni story za kutunga...na hapa tumesimulia machache tu kati ya mengi yaliyofanyika na kuyashuhudia

Napajua mwadui na karibu migodi yote ya tanzania, mwadui wanaitwa wabeshi na kule nyamongo wanaitwa intruder, kiukweli hiyo shughuli inahitaji ukakamavu sana. Kiukweli wale wa nyamongo ndio wanawakati mgumu sana maana wao huingia pit kabisa kupitia kwenye benchi za shimo ambapo ni mbali sana kutokea juu na pia kurudi juu, kidogo pale mwadui wabeshi walikuwa na nafuu aisee kuliko ile shughuli ya Nyamongo pale. Lakini mwisho wa siku pale maganzo naona mlitajirisha sana waarabu na watu wachache kuliko wabeshi wenyewe ambao asilimia kubwa wameishia kwenye gonjwa letu hili duh aisee pole sana na mapito na hard time uliyokuwanayo, shemeji huyo mpige tipper asikuumize kichwa wapo wengi sana siku hizi hutakiwi kuwanyenyekea sana hao watakufanya mtumwa.
 
Napajua mwadui na karibu migodi yote ya tanzania, mwadui wanaitwa wabeshi na kule nyamongo wanaitwa intruder, kiukweli hiyo shughuli inahitaji ukakamavu sana. Kiukweli wale wa nyamongo ndio wanawakati mgumu sana maana wao huingia pit kabisa kupitia kwenye benchi za shimo ambapo ni mbali sana kutokea juu na pia kurudi juu, kidogo pale mwadui wabeshi walikuwa na nafuu aisee kuliko ile shughuli ya Nyamongo pale. Lakini mwisho wa siku pale maganzo naona mlitajirisha sana waarabu na watu wachache kuliko wabeshi wenyewe ambao asilimia kubwa wameishia kwenye gonjwa letu hili duh aisee pole sana na mapito na hard time uliyokuwanayo, shemeji huyo mpige tipper asikuumize kichwa wapo wengi sana siku hizi hutakiwi kuwanyenyekea sana hao watakufanya mtumwa.
Upo sahihi mkuu!!Waarabu wengi sana waliweka makazi yao pale Maganzo ili kufanya biashara ya ng'hana(almasi).Na hakika wametajirika kwa biashara hiyo.Wapo wengine mpaka leo ni "wadhamini" wa Wabeshi wanaoingia mgodini kufanya yao,wengine sasa ni viongozi wa kisiasa ndani ya vyombo vya maamuzi na kutunga sheria lkn utajiri wao wameupata kwa njia hiyo.

Sio siri.Wabeshi wengi sana wamekufa na hili gonjwa la kisasa,hii ni kwa sbb walikuwa wanapata pesa ya haraka na uwezo wa kuhonga!Wengi sana wametangulia mbele za haki kwa ngoma!!Watu wangu wa nguvu kina Masunga,Mwanaluhende na watu wangu wa ukweli wa kijiji cha Mwigumbi na Utemini
 
Wewe "mtoto mayai" huwezi kujua hizi hustling...Uliza wenzako wanajua maisha..kwako unayoona kusadikika sisis ndio maisha yetu halisi..ni bahati nzuri unaongea ukiwa nyuma ya keyboard
Kwani wewe unaongea nyuma ya nini
 
Upo sahihi mkuu!!Waarabu wengi sana waliweka makazi yao pale Maganzo ili kufanya biashara ya ng'hana(almasi).Na hakika wametajirika kwa biashara hiyo.Wapo wengine mpaka leo ni "wadhamini" wa Wabeshi wanaoingia mgodini kufanya yao,wengine sasa ni viongozi wa kisiasa ndani ya vyombo vya maamuzi na kutunga sheria lkn utajiri wao wameupata kwa njia hiyo.

Sio siri.Wabeshi wengi sana wamekufa na hili gonjwa la kisasa,hii ni kwa sbb walikuwa wanapata pesa ya haraka na uwezo wa kuhonga!Wengi sana wametangulia mbele za haki kwa ngoma!!Watu wangu wa nguvu kina Masunga,Mwanaluhende na watu wangu wa ukweli wa kijiji cha Mwigumbi na Utemini
Mike nimependa sana story yako ukianza ya lebanon nishtue nijue fatik lak lipoje
 
Swala la kuuwawa kwa wabeshi halijaisha hadi leo,ilikuwa mwaka -2009-2010 nilipitia kwa waganga wawili tofauti mmoja Kutoka BUBIKI na Mwingne wa NZEGA Walinihakishia nitaenda kupata ALMASI,Lakini niliposhuhudia jamaa yangu akikoswa kuuwawa kwenye lile tope..ndio ilikuwa mwisho wangu kuwa mgoni.
Mkuu Waganga wa siku hizi wamekuwa matapeli...Kiukweli!!Bila kupepesa macho,haya mambo ya Waganga hasa wa maeneo ya Mwigumbi na Utemini pamoja na Idukilo ilikuwa balaaaaaa!!Akikupa dawa zake unaweza kupishana na polisi na farasi wake uso kwa uso na wala wasikuone,muhimu ni kutimiza masharti na uwe na roho ngumu...Ningetoa ushuhuda wa mganga mmoja wa Idukilo,lkn bado yu hai na familia yake ipo..inaweza mletea matatizo
 
Back
Top Bottom