Tulivyokuwa tukiiba almasi mgodi wa Mwadui na wenzetu kuuawa

Hii ilikuwa ni miaka ya '90 mwanzoni, tukitokea pembezoni mwa mgodi wa Mwadui, tulifahamika kwa jina la "Wabeshi".

Zana zetu za kazi ilikuwa ni sululu, chepe na majembe yaliyonolewa sana, tulikabiliana na jeshi la polisi la mgodi wa Mwadui waliokuwa na kikosi cha farasi na mbwa wenye uweredi mkubwa sana na mafunzo ya hali ya juu.

Nakumbuka siku rafiki zangu wawili walivyouwawa kwa kuumwa na mbwa sehemu za siri na jirani yangu Jilingumika Masufulia alivyopigwa risasi ya kichwa akivuka fensi ya mgodi wa Mwadui.

Almasi tuliibatiza jina la "ng'ana", na ilikuwa hauwezi kwenda kuiba bila kuchanjwa chale za kwapani na matakoni. Mganga wetu mkubwa alikuwa ni Mzee maarufu sana wa Kijiji cha MWIGUMBI, Nje kidogo ya mgodi, huyu ndio mzee aliyetupa dawa na kinga wakati wa kwenda kuiba almasi,wakati huo nikiwa na miaka kama 16 tu hivi, nimemaliza darasa la saba shule ya msingi Luhumbo. Tajiri wetu mkubwa alikuwa mwarabu wa Maganzo maarufu kwa jina la Abeid, huyu alitupikia vitumbua na chai kabla ya kwenda mgodini kuiba almasi, na chote tulichokipata tulipeleka kwake kama tajili na kupata ujira wetu.

Tajiri Abeid hakuwa mtu "rahisi rahisi", yeye mganga wake alikuwa anatokea kijiji cha Idukilo, mganga hatari sana aliyekuwa na madawa ya kisukuma ambayo yaliwabadilisha watu na kuwa mbwa mwitu au nyani pindi walipoingia ndani ya mgodi kuiba, tajiri Abeid alikuwa anaishi kijiji cha Maganzo, akiwa na duka la bidhaa la kuzugia,lakini deal zake kubwa ilikuwa ni kununua almasi na kuziuza kwa matajili wakubwa wa Mwanza na Shinyanga mjini.

Almasi zote tulizopeleka kwa Abaeid zilikuwa zinatunzwa na mbuzi dume, beberu mkubwa aliyekuwa anazimeza na kuzihifadhi tumboni hadi mteja atakapokuja,hata polisi wakifika na ku-search vipi,wasiongeziona almasi kwani beberu alikuwanazo tumboni,hakuwa beberu wa kawaida maana alikuwa na chumba chake na alilala ktk godoro. Mbuzi hakula nyasi wala majani ya miti, bali vitumbua, chai, ugali na "maparage". Kipindi hicho hatukuwa na ruhusa ya kuongea juu ya mbuzi yule, tulimuogopa na kumtii zaidi hata ya kiongozi wa msafara wa wabeshi.

Tajiri wa uhakika alikuwa Fantomu wa maeneo ya Mipa,huyu hakuonana na sisi wabeshi maana tulikuwa watu "wadogo" sana, bali alipitia kwa Abeid na waarabu wengine wa Maganzo.

Maisha ya kuwa "mbeshi" yalikuwa magumu sana,maana kifo na kujeruhiwa ilikuwa ni njenje,tuliuwa na kuuwawa. Polisi, mbwa na farasi waliokuja bila tahadhari waliuwawa kwa chepe zilizonolewa na mapanga. Tukio moja nalokumbuka ni la mwenzetu Masunga kumuua mbwa wa polisi kwa kumkata na chepe mdomoni na kuutenganisha mdomo pande mbili.

Wenzetu wengi walikufa tukiwa bwawani tukiiba,wengi walizama kwenye tope liliotokana na mabaki ya kusafishwa kwa almasi ambayo sisi tulikuwa tunakwenda kuchota na kuchekecha upya,bwawa hili la tope zito lilukuwa karibu na "sorting area" ambayo ililindwa kwa kiasi kikubwa sana. Lakini kwa imani ya chale za mganga wa MWIGUMBI na Idukilo watu wengi tulikuwa na ujasiri wa kukatiza kila mahali bila hofu.

Wengi waliojeruhiwa na kuumizwa walilazwa ktk hospitali ya Mwadui.Siku nilipoamua kuacha "kazi" hii na kurudi shule,ilikuwa ni siku hatari sana... binamu yangu kipenzi Luhende alipigwa risasi ya kichwa na ubongo kutawanyika, mbele ya macho yangu Luhende alikufa bila hata kuomba maji. Askari wakiwa umbali wa kama mita 100,sisi tukiwa na makarai yetu na chekecheke tukiambaaambaa pembeni ya reli maeneo ya SONGWA ktk njia ya mzunguko kuelekea Maganzo tuliwekwa katikati yao na kuuliwa baadhi yetu. Katika kundi la wabeshi kumi, saba walikufa hapo hapo..watatu walifia hospitali na mimi pekee nilipona baada ya kujitumbukiza kwenye bwawa la maji ya kunywea mifugo, niliogolea chinichini kwa chini na kuibukia upande wa matete, ambapo nilikaa ndani ya maji zaidi ya masaa 12 bila kutoka..nikiwa nimetoa pua tu na kujishikiza kwenye "msitu" wa matete.

Kikosi cha polisi wenye mbwa na farasi walizingira bwawa lile mpaka usiku wa kiza kinene, wakaamini nimeshakufa na kuzama hivyo wangefika kesho yake kukuta ninaelea baadaya kufa.Katikati ya kadhia ile ndipo nilpoona kazi ya ubeshi si lolote si chochote, zaidi ya mwili kujaa chale za tako mpaka kwapani.

Pesa tuliyopata ilishia mnadani Maganzo,ambapo tulikula na kunywa. Hatimaye niliamua kurudi kijijini Luhumbo,nikakariri tena darasa la saba kwa jina la mtoto wa mjomba aliyeacha shule na kwenda kuchunga na kulima vibarua maeneo ya Muhunze. Nilikuwa mkubwa kuliko wote darasani lakini sikukata tamaa. Nilisoma kwa mwaka mmoja wa darasa la saba kwa bidii na usongo na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na shule ya Tabora Wavulana.

Kwa mara ya kwanza napanda train kwa "warrant" ya serikali, station ndogo ya Songwa kupitia Shinyanga kuelekea Tabora. Nakutana na Afande Chacha kwenye geti la Tabora boys, ananipokea kwa kichurachura na bakora za mgongo bila sababu, wakati huo Tabora Wavulana ipo chini ya jeshi. Mwanzo naona maisha ya ubeshi ni afadhali kuliko shule ya aina hii..mchakamchaka na Afande Chacha kila asubuhi kupitia Kwihala mpaka Kipalapala.Juma la kwanza natamani kutoroka lakini sijui mahali pa kuelekea, shule ipo nje ya mji na mfukoni sina nauli.Baada ya mwezi ndani ya kombati ya kijani mwanajeshi,inatangazwa disko ya "welcome form one".

Disko langu la kwanza maishani,nakutana na watu wenye lafudhi nzuri na Kiswahili kilichonyooka, mimi nashindwa kuongea mbele za watu sbb lafudhi yangu ni "ngumu" kusikika na kueleweka. Ninapata marafiki toka pande mbalimbali za Tanzania. Kapufi wa Mpanda na Mwaisengela wa Mbeya wanakuwa marafiki zangu kwenye bweni la Kimweri. Miaka minne ndani ya Tabora,wao wanaita Mboka Manyema..ninabahatika kurudishwa tena kidato cha tano na cha sita,baadae naamua kuingia Jeshi bila kwenda chuo Kikuu. Ninalitumikia jeshi kwa muda mrefu, safari yangu ya Lebanoni kusiamamia amani inanirudisha nyumbani na kukuta mke wangu akiwa na mimba ya miezi sita na mimi nilikuwa nje kwa mwaka mzima.

Nikukumbuka nilipotoka,shida na vurugu za kuwa mbeshi....Oooops!!! Naona dunia sio mahali salama pa kuishi
Pole sana kama ni story ya kweli andaa kitabu halafu huyo mke we usimwambie lolote wala usionyeshe kushangaa mpongeze then yeye mwenyewe atajiadhibu
 
Nina wasiwasi na hii story kama ya kutunga ma uongo mwingi especially kwenye maeneo ya Maganzo, Mwadui, Songwa.

Nimezaliwa Kolandoto nikikulia hapo Kolandoto, Kisesa na Mipa. Shule pia nimesoma hapo.

Kaka yangu alikuwa mnunuzi wa Almas.

Mdogo wangu anafanyakazi Mwadui katika position kubwa.

Uzushi mkubwa kuliko yote ni huu

Phantom alikuwa akiishi Mipa. Hii haipo na haijawahi kutokea.
Huyo mbuzi kwa Abed ni story ya kusadikika haijawahi kuwepo.

Hiv tu vinaifanya story yako nzima kuwa fake na uzushi.

Na kwa taarifa yako nimetua asubuhi hii Mwanza toka Dar na sasa hivi nipo njiani toka Mwanza kwenda Mipa, kisha Mwadui, Maganzo na Kolandoto.

Almasi kwa Kisukuma inaitwa ng'hana na sio jina lilobatizwa na wabeshi.
Acha ushamba kuku wa mayai wewe...Unafikiri watu wote walegevu??mambo ya ndege yanahusu nini kama sio ushamba?Tulia wanaume waongee
 
Acha ushamba kuku wa mayai wewe...Unafikiri watu wote walegevu??mambo ya ndege yanahusu nini kama sio ushamba?Tulia wanaume waongee

Haya mstaraabu mwenye maguvu, ila jamaa yako mwongo mkubwa na stori ya kutunga.

By the way huu ulimwengu wa leo ni wa akili mshamba wewe, utabaki na maguvu yako yasiyokuwa na tija mwisho utaishia kupigwa risasi kwa kuvamia maeneo usoruhusiwa kuingia.
 
Bill wengine ligi za kubishana sio fani yetu....amini unachoamini,mdogo wako kuwa na position kubwa Mwadui au wewe kuishi Kolandoto hakukupi hati maliki ya kujua yote yanayofanyika..Ungeuliza kwanini Almasi ikauziwe Mipa ambapo si nyumbani kwake!!...Nilidhani unasema si kweli kuwa almasi huitwa ng'ana,kumbe tatizo lako ni neno "kubatizwa ng'ana"...Mwisho nilidhani utasema na wewe ni mbeshi,kumbe umekulia tu Kolandoto,Mipa,Kisesa na Mwadui...Sisi hatujakulia humo,ila tumefanya humo matukio...Mambo mengine ya mbuzi kuwa ni kusadikika yaache kama yalivyo na endelea kuamini unavyojua...Hii Fastjet na bei yake inafanya kila mtu ajieleze kila anapopanda ndege!!Kulikuwa na ulazima wa kusema "umetuwa Mwanza?"......1990's ulikuwa bado Kolandoto unasoma vidudu!!Haya mambo ya wakubwa zako huwezi kujuwa

Haya bhana, wadanganye sana tu wasiojua hii biashara ya ALMAS na Wabeshi. Hata wanunuzi nadhani wewe hauwafahamu haukuwahi kuwafahamu na bado ulikuwa mtoto.

Watakuamin waliombali, lakin mmmhh ni uongo mtupu.
 
Hueleweki na wala hujielewi.
1. Habari za position ya mdogo wako zinahusiana nn na hii story.

2. Kutua kwako mwanza asbh hii na kuelekea Mipa kuna tija gani kwa wanaofuatilia uzi huu.

Acha ushamba.
Hahaaaaa, haya boss uchwara. Basi acha kutokwa mapovu endelea kumeza urojo mlodanganywa
 
Haya bhana, wadanganye sana tu wasiojua hii biashara ya ALMAS na Wabeshi. Hata wanunuzi nadhani wewe hauwafahamu haukuwahi kuwafahamu na bado ulikuwa mtoto.

Watakuamin waliombali, lakin mmmhh ni uongo mtupu.
Bill vyovyote utakavyoamini....kama unasema hiki kitu fulani ni cha uwongo lazima useme upande wake wa ukweli....Tatizo hapo ni jina Fantom ndio linakutoa mapovu,maana inajulikana vibaraka wake mnafikiri anachafuliwa...Huyu hata "system" inajuwa biashara zake kitambo,wakitaka wanamfuata tu...hizi ni habari za 1990's usiogope
 
hapo nwisho nafikiri kuna epsod inaendelea nje mwaka mzima mke mimba ya miezi sita.unatokaje hapo?

Watu wengi wamepata utamu wa jamaa alivyokuwa anasaka pesa mpaka misiba....ila ujumbe na ushauri nadhani alitaka juu ya yeye kuwa nje ya nchi mwaka mmoja ila karudi mke anamimba ya miezi sita!!!!tuanzie hapo
 
Ehh maisha haya,poleni sana
Wasukuma wote wa Jf humu tutawajua
Nshafika mwadui for study tour nikiwa mdogo hivi
Nakumbuka sanamu ya chuma Ile ya mzungu Williamson if my memory serves me right..
 
Watu wengi wamepata utamu wa jamaa alivyokuwa anasaka pesa mpaka misiba....ila ujumbe na ushauri nadhani alitaka juu ya yeye kuwa nje ya nchi mwaka mmoja ila karudi mke anamimba ya miezi sita!!!!tuanzie hapo
Jamaa anapitia mitihanii mizitoo dahh
 
Ehh maisha haya,poleni sana
Wasukuma wote wa Jf humu tutawajua
Nshafika mwadui for study tour nikiwa mdogo hivi
Nakumbuka sanamu ya chuma Ile ya mzungu Williamson if my memory serves me right..
Utakuwa unasemea hii hapa
image.jpeg
 
image.jpeg

Acha ushamba kuku wa mayai wewe...Unafikiri watu wote walegevu??mambo ya ndege yanahusu nini kama sio ushamba?Tulia wanaume waongee
Mkuu Ngaliba Dume toka mababu zetu huko miaka na miaka wamekuwa wakibanwa na wazungu wakati wa uchimbaji mpaka uchambuaji wa almasi...Mababu zetu walishuhudia almasi ikichimbwa na kusafirishwa kwa ndege kwenda nje ya nchi...Kilichobaki ilikuwa ni kuingia na "kuiba" ili nasi tufaidikepo kidogo...Hebu tazama hapa babu zetu wakichambua almasi huku wakiwa wamesimamiwa kwa nguvu ya polisi
 
Back
Top Bottom