Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Huyo alikuwa ni Twaha Jenerali Ulimwengu akituasa katika makala yake ndani ya Gazeti la Raia Mwema la Septemba1, 2010 kabla ya uchaguzi. Alituasa kuwa tukichagua hovyo na halafu tukajikuta tunaanza kutendewa hovyo, tusiseme hovyo.Tunachagua kama vipofu, kisha tunalalama kama vichaa. Sasa tuamue: ama tuchague viongozi wetu kwa makini, au tukae kimya wakati wakitunyanyasa. Wachagua hovyo wasiwe wasema hovyo wakitendewa hovyo.
Watanzania kama kawaida yetu tulipuuzia ushauri wake na tukamrudisha madarakani Rais yuleyule, chama kilekile, mafisadi walewale na sasa tunaanza kuonja machungu yale yale ! Kwa kifupi tulichagua hovyo na hivyo tunaendelea kutendewa hovyo, je tukae kimya ?
Ndani ya mwezi moja tayari lile zimwi lisilo na sura tulilokuwa tunapambana nalo ghafla limefufuka na safari hii limeingia kwa staili mpya na ya kutisha. Majeraha tuliyompa yalimfanya akimbilie Ulaya kwa matibabu na sasa kapona na karudi kwa ari na nguvu zaidi.
Hata hivyo linaloogopesha zaidi ni kuwa hii ya Dowans ni rasharasha tu, dhoruba yenyewe ya miaka mitano inatusubiri. Katika hii awamu ya pili, tutashuhudia ambayo yataifanya awamu ya kwanza ionekane kama vile tulikuwa peponi - si tumechagua wenyewe ?