Tuliandamana kwanini tusiandamane?

mbarikiwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
505
39
Tuliandamana kwanini hatuandamani?

Bushi alipokuwa anakuja Tanzania tuliandamana kupinga ziara yake maana anatuonea sisi wanyenyekevu

Waisrael walipowachapa Hamas tuliandamana maana wanyenyekevu tunaonewa

Mahakama ya ICC ilipomtia hatiani mnyenyekevu mwezetu Bashiri tuliandamana na kusema wanyenyekevu tunaonewa.

Sasa Bashiri amewafukuza watoa msaada wa kimataifa kule Darfur, na pia jana wafuasi wake wamemuua mslam wa kiafrika kule Darfur kwa sababu anafanya kazi na hawa umoja wa mataifa wanaotaka kumkamata mnyenyekevu Bashiri.

Zaidi ya hayo Waslam wenzetu wa kule Darfur wanakufa kila siku kwa matatizo yaliyoanzishwa na Bashir.
Swali langu ni hili kama tuliweza kuandamana kwa hayo mengine yote yanayowahusu Wanyenyekevu wa kiarabu, Je hapa Waslam wenzetu wanakufa tu kwa kunyanyaswa na waarabu kwa nini hatuandamani?

Nachelea kusema kuwa huwa tunaandamana kutokana na njaa zetu ili waarabu watuongezee mafedha yao ya mafuta.

Tuandamane wajameni,

Tuliandamana, kwa nini tusiandamane?
 
Duu! hii imetulia subiria wenyewe waje kuchangia utakiona!
 
uko sasa kaka,mara nyingi huw tunaandamana tukiwa hatujui kiini cha maandamano,
wewe jiulize, mambo mangapi yanalikumba taifa letu, tena ya ajabu,lakini ukijaribu kuwaambia watu tuandamane kwa ajili ya mstakabali wa taifa hili, hakuna anaejitokeza
sasa ngoja wasikie israel imevamia palestina na kuwaua warabu, tunaandamana!!!
yetu yanatushinda, sisi tuna matatizo sana tz.
we fikiria mtu anakwambia ( tena kiongozi) anamjua mmiliki wa kagoda, ukimwambia amtaje anarudi nyuma. UNAFIKI UNATUSUMBUA SANA
 
Asante mwanzisha mada. Kama kawaida sio asili ya waAFRICA kuandamana. Katika nchi nyingi Madikteta na Mafashisti wa Kiafrika wamepiga marufuku maandamano kwa Wa-Tz NI LAZIMA upate kibali cha POlisi na sio kutoa taarifa kama kwa wenzetu walio Huru. Rais JK alikuwa Mwenyekiti wa AU yeye na wanzake wanamtilia kifua eti akikamatwa fujo itazidi? He is the sitting president they don't want it to happen !!![If you live in a glass house never throw stones][/I][Kwa waswahili kama unaishi nyumba yenye vioo ni marufuku kurusha mawe][/I] Who told them kutakuwepo na fujo? Southern Sudan under Garang who was killed by El Bashir with the help of Museveni there was a war for Oil for 20 years leo hakutawaliki lakini akina JK hilo haliwanyimi usingizi !!wanamtetea kwa nguvu zote unajua kwa nini labda anawachotea mafuta kwa kijiko sijui. Ndio maana kama hatujafadhiliwa na Iran au Saudia hatuwezi kuandamana kwa Sababu ya kulinda Uislamu/Uarabu wa El bASHIR. Maandamano hayaruhusiwi kama utapingana na tamko la Rais kwanza hatakamatwa El bashir ile ni sawa na kumtishia nyau mtu mzima. Kama tukipokea tende na nyama ya kondoo kutoka Iran tutaandamana hata ijumaa hii tu!!!! Wa tz bila chochote hawandamani labda CCM iwaite!!!
 
Back
Top Bottom