DOKEZO Tukuyu: Baadhi ya mitaa yenye wananchi wa kawaida inanyimwa maji, huku yenye viongozi ikipendelewa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Katika mji wa Tukuyu-wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya kumekuwa na mgao wa upendeleo kwani kuna mitaa inakosa maji kwa miezi kadhaa na bill tunakula. Mfano mtaa wa Tanesco Power Station- chini tunakosa maji kabisa.

Licha ya kwamba Serikali ilitoka pesa nyingi za miradi mipya ya maji lkn ndio kabisa hatupati maji. Watu wa mamlaka za maji hufungulia maji kwenye mitaa wanayoishi wao na Viongozi wakubwa tu ila kwa wananchi wa kawaida hatupati maji.

Majibu ya Mamlaka ya Maji soma hapa - Mamlaka ya Maji Tukuyu: Mgao wa maji unahusu watu wote, hadi nyumbani kwa Spika Tulia na kwa DC napo kuna mgao
 
Back
Top Bottom