Tukio la ujambazi lasababisha mauaji kijiji cha Gwarama wilayani Kakonko-Kigoma

gidytitus

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
332
28
Habari za kusikitisha nimezipata leo asubuhi ambapo watu wawili wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa na hali zao ni mbaya sana. Tukio hili limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia nyumba tatu yaani familia tatu ndani ya usiku huo huo mmoja, katika familia moja waliyovamia wamempiga mama wa familia hiyo na mama huyo kupoteza maisha papo hapo lakini baba wa familia hiyo akafanikiwa kuwaponyoka, wakaenda familia nyingine na kumwua baba wa familia hiyo kwa kumpiga risasi lakini mwisho kabisa wakaingia nyumba nyingine na kuacha watu wa familia hiyo wakiwa katika hali mbaya mara baada ya kupigwa kwa mapanga na visu. Lakini pia wameondoka na baba wa familia moja na mpaka naingia humu jamvini alikuwa bado hajapatikana.

Kwa wanaozaliwa kijijini hapo kama mimi wanafahamu kuwa kijiji hiki kipo mpakani kabisa na nchi jirani ya Burundi, na matukio kama haya yamekuwa yakijirudia mara kwa mara, na inasakikika kuwa ni askari wa jeshi la Jirani huingia na kufanya uhalifu huo, lakini pia maeneo haya hakuna hata hospitari inayoweza kunusuru maisha ya wahanga kama hawa isipokuwa kuna nahanati ya mission ambayo hata haiwezi kutoa huduma ya damu. Vijiji hivi vyote vilivyoko pembezoni mwa mkoa huu wa kigoma hatuna hospitali ni mpaka kusafiri kilometer kama 1000 kufuata hospitari ya wilaya ya Kibondo, na watu wengi wamepoteza maisha njiani wakati wakisafirishwa kuelekea hospitali hiyo ya wilaya.
Cha kusikitisha zaidi ni kwamba kijijini hapa kuna kituo cha polisi na moja kati familia ambayo imevamiwa ni karibu sana na mahali kituo kilipo, sasa najiuliza hawa police wanafanya kazi gani mpaka ifike hatua ya raia kuteswa wakati wamewezeshwa kwa kila namna ili kuilinda mali na maisha ya watz.
Christopher Chiza mbuge wa hili eneo upoooooo..........................!!!
Umeyasikia hayo kabla yangu au ni kwamba ndo unashtuka, hay shtuka basi afu uchukue hatua maana hali ya wananchi wako tunaoishi maeneo haya yapo taabani na mashakani tunaishi kama vile tupo Africa ya kati...!!
Tafadhali chukua hatua za msingi................... ;asaaasad.....!!
Source; Baba yangu mzazi aliyeko kijijini hapo.
 
Poleni sana mkuu. Mimi babu zangu wako Manyovu nimepata kufika mahala pale mara kadhaa najua hali ya huko kiasi, kwa mambo ya ujambazi ukanda ule ni hatari hakika serikali inabidi ichukue hatua kulinda raia na mali zao walioko karibu na ule mpaka wa Burundi. Hospitali ya Heri mission ilikua nzuri miaka ya nyuma vp siku hizi?
Pole kwa wote waliofikwa na majanga hayo
 
......lakini pia maeneo haya hakuna hata hospitari inayoweza kunusuru maisha ya wahanga kama hawa isipokuwa kuna nahanati ya mission ambayo hata haiwezi kutoa huduma ya damu. Vijiji hivi vyote vilivyoko pembezoni mwa mkoa huu wa kigoma hatuna hospitali ni mpaka kusafiri kilometer kama 1000 kufuata hospitari ya wilaya ya Kibondo, na watu wengi wamepoteza maisha njiani wakati wakisafirishwa kuelekea hospitali hiyo ya wilaya.......
hapo kwenye bold red, vema urudi usahihishe la sivyo tuitaju akuwa stori yote ililenga kumchafua Mh Chiza.
 
Hakuna hospitali , mbona CCM wanasema kila kijiji ktk nchi wamemwaga maendeleo? Viva SISIEM
 
Kigoma iko burundi au DRC naisikia sana hiyo wilaya. eti ni kweli kuna watu wengi wenye pesa huko ?
 
Poleni sana wathirika watukio mungu atawalinda ndio shida ya mipakani. We ---- nini umeona. Kigoma bulundi kwa sababu ipo mpakani uko kwenu mbona atusemi ni kenya?
 
hapo kwenye bold red, vema urudi usahihishe la sivyo tuitaju akuwa stori yote ililenga kumchafua Mh Chiza.

Ndugu mi sina lengo la kumchafua mtu hapa, nachosema ni kweli au kama huamini si uingie google map upate hizo takwimu ninazokwambia?? Angalia distance from Gwarama to Kibondo. Utaelewa nini nachosema, kuna watu tunateseka wakati we are in the same planet particularly in Tz, we pay the same taxes kujenga nchi yetu, WHY....???? Eemu nitokee hapo kama umekereka kumtaja Chiza hapa just leave me alone but he is answerable regarding that tumemchagua kutuwakilisha na sio kukimbilia nchi za wengine walizokwisha jenga wenyewe arudi nyumbani akajenge kwao na sio kwenda kujenga shule na majumba ya kifahali kwa wachaga huku akituacha ndugu zake kwa majahidini hawa wakitutesa na kuua ndugu zetu> >>> I hate CCM to the maximum........!!!! coz ukiangalia jitihada zote zinazofanyika katika vijiji hivi ili kujikwamua kimaisha hakuna support yoyote kutoka serikalini, afu mwisho wa siku tunakuja kunyang'anywa na kile tulichokipata! I repeat again ili unisikie vizuri kama upo karibu nae ukamwambie hiviiiii........!!! Anadaiwa mambo mengi aliyoahidi kwa wazawa hawa walomtuma au kama ni uongo aje atubu kwa hawa watu.... la sivyo asikanyage tena huku yaani amalize muda wake afu asepe, uwaziri wake hauna faida yoyote kwetu.....!!!!!
 
quote_icon.png
By bategereza
Kigoma iko burundi au DRC naisikia sana hiyo wilaya. eti ni kweli kuna watu wengi wenye pesa huko ?



Kigoma ipo Tanzani, we mwehu nini, unafikiri hawa watu wote maarufu waojulikana bongo hii wanatokea wapi?? Ni kweli kuna wenye pesa huku ila hakuna ulinzi wa kuaminika na kuwalinda na ndo mana wengine huishia mikoa mingine na kwenda kuwekeza huko. Ila ni kwamba hatujapata viongozi wenye nia na uzalendo wa kuipigania nchi hii kutoka wenye mikono ya wadhalimu na wasio na utu, siku tukiwapata tu lazima Kigoma iwe moja ya mikoa maarufu hapa bongo na Africa kwa ujumla, Subiri...!!
 
Poleni sana mkuu. Mimi babu zangu wako Manyovu nimepata kufika mahala pale mara kadhaa najua hali ya huko kiasi, kwa mambo ya ujambazi ukanda ule ni hatari hakika serikali inabidi ichukue hatua kulinda raia na mali zao walioko karibu na ule mpaka wa Burundi. Hospitali ya Heri mission ilikua nzuri miaka ya nyuma vp siku hizi?
Pole kwa wote waliofikwa na majanga hayo
Rafiki mitaa hiyo ya kwetu tuna zahanati ya mission inayoitwa kabare ilikuwa nzuri pindi bado hawa watu weupe bado wakiwepo lakini kwa sas kachukua mtu mweusi, hakuna chochote kinachofanyika, ilikuwa na electrical system nzuri lakini ukienda sasa hivi utaona aibu mwenyewe, nakumbuka kipindi hicho ilikuwa iko juu karibu iwe ya hospitali ya kanda lakini kwa sasa ni aibu, Poriii!!!!
 
Back
Top Bottom