Tujifunze ya ndege: Hiki ndicho Kisanduku cheusi (black box) cha mawasiliano kila ndege ipatapo hitilafu au kuanguka huwa kinakitafuta


Mkuu Britanicca chanzo cha ajali ya hii Air France hasa hasa ilikuwa nini?..kwanini nauliza swali hili?... mimi ni mmoja ya wadau wanaopenda sana sana kufuatilia ajali za ndege, hii ni moja ajali niliifuatilia sana, na kwa kituo.

Yahoo walikuwa wana report hii ajali karibu kila siku kwenye mtandao wao, kwa mujibu wa yahoo, chanzo hasa cha ajali hii kutoka kwa wachunguzu wa ajali ilikuwa kifaa kiitwacho Pitot tube.

Pitot tube ni kifaa kinachobadilisha kasi ya upepo kuwa speed halisi, na kinakaa pembeni kwenye bawa la ndege, ukikaa kwenye ndege karibu na bawa kinaonekana, kifaa hiki,ndio hubadilisha kasi ya upepo kuwa Speed na kupeleka kwenye cockpit.

Sasa wanasema kwa mujibu wa uchunguzi wa mwanzo baada ya ajali hiki kifaa ndio kilikuwa chanzo cha ajali, walisema kilijaa barafu kikapelekea kupeleka taarifa za uongo kwenye Cockpit, ndege ikawa haijitambui kila kitu kwenye Cocpit Kikawa hakifanyi kazi kwa usahihi ndio ajali ikatokea.

Pia uchunguzi wao ulionesha ile ndege ilipasuka angani kwa sababu karibu maiti nyingi walizoziopoa kwenye maji zilikuwa hazina maji kwenye mapafu hii ilionesha ndege ilianguka watu wote wakiwa washakufa kitu ambacho walisema si rahisi kutokea kama ingeanguka ki kawaida kuna baadhi ya maiti wangezikuta na Maji kwenye mapafu.

Wakati uchunguzi unaendelea wa ajali ile,iliripotiwa marubani wa Air France wanaoendesha Airbus waligoma kipindi kile wakiomba uchunguzi wa kina ufanyike kwenye Airbus zote, na kwa kiasi fulani ajali ile iliyumbisha biashara ya Airbus Duniani.

Waliandika mengi kuhusu chanzo cha ajali ile mengine nimesahau, lakini katika ambalo sitalisahau kwenye ajali ile ambalo liliripotiwa kwenye media kuna mama wa Kibrazil alikuwa asafiri na ndege ile alichelewa ikamuacha, aliporudi nyumbani saa kadhaa baadae akapata taarifa ndege iliyomuacha imeanguka na watu wote waliokuwepo ndani yake wamekufa.

Yule mama alifanya sherehe ya shukurani na familia kumshukuru Mungu kumuepusha kifo, siku ya pili baada kumshukuru Mungu wake akaenda kugongwa na Gari barabarani mtaani akafa.
 
Elimu nzuri,huwa nafuatilia sana kile kipindi cha Air crush investigation kinachorushwa na National Geographic Channel..wanaelezea vizuri sana hizi habari.
 
Asante kwa bandiko elimishi mkuu.
Je kila aina ya kifaa cha angani kama ndege ,rocket, n.k ina kifaa hicho na je vifaa hivyo huwa na the same quality au quality ni tofauti kulingana na uchumi Wa kila mhitaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom