Tujifunze jinsi ya kuandaa Unga wa lishe hadi jinsi ya kuupika uji huu

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,274
20,673
Haya tena jamani leo nataka tujifunze namna ya kuandaa unga wa lishe hadi jinsi ya kuupika uji huu.
Ningeomba sana kanuni nitakayo itumia hapa basi kila mmoja airekebishe kulingana na jinsi anavyopenda yeye.

KANUNI ZA KUANDAA UNGA WA LISHE.

Vifaa
=ulezi kg 1
=mahindi yasiyokobolewa kg 1/2
=ngano isiyokobolewa kg 1/2
=karanga kavu ila mbichi 1/2
=soya isiyobanguliwa 1/2.

Njia ya kuandaa,
1) chukua ulezi wako upete vizuri kwenye ungo. kisha weka kwenye maji kuupembua. Hakiksha kwamba unaupembua mara nyingi zaid kwa kutumia maji masafi na chombo cha bati hadi mawe/mchanga uishe wote kabisa. Kumbuka kwamba ulezi huwa michanga sana.

hivyo matumizi ya vitu vya bati. chuma wakati wa kupembua hukufanya uweze kuona mawe vyema, pia mawe yasiteleze sana as yanakuwa kama yananatiana na chuma hivi. so muda wa kupembua kuwa mchache tofauti na ukitumia chombo cha plastic.

2)ukishahakikisha ulezi wako ni msafi basi tenga ungo wako kisha umimine ulezi na uanike juani ili ukauke kabisa.

3) peta mahindi yako vyema toa yote yaliyo mabovu, peta ngano yako toa punje zote zilizo mbovu kisha osha vizuri kwa maji ya kutosha na anika kwenye ungo wake tofauti.

4) peta na chagua soya, kisha chemsha soya zako jikoni kwa dk 10 zitokote, kisha anza kuzimenya maganda, ni rahisi as yanakuwa yanamenyeke kwa kuteleza hivyo ukifikicha mkononi tu yanatoka. baada ya kutoa maganda yote anika hizi soya kwenye ungo wake hakikisha zinapigwa jua sana sana zikauke kabisa ziwe kama vile hazijagusa maji kabisa.

5) zikisha kauka kabisa zitie kwenye sufuria na moto mdogo sana anza kuziaanga kama vile unakaanga karanga ama ziweke kwenye oven 60 degree kwa nusu saa. zikitoka kwenye moto ziweke sehem ya wazi ili zipoe bila kupeana unyevu.

6) chagua karanga zako vizuri, hakikihsa kila punje mbovu unaitoa (jamani naomba niseme wazi kila karanga mbovu itolewe) kisha zikaange kwa moto mdogo sana ziwe kavu kabisa lkn zisiungue. ama ziweke kwenye oven kwa 60 degree for 15-20 mints. ukishazikaanga zianike tena juani ili zipoe lkn zipoe bila kuabsorb moisture kabisa.

zikishakauka kabisa zidunde kama mbegu ya ubuyu basi zimenye maganda yote kisha upete halafu uchague zile punje nzuri tu ambazo hazina rangi ya njao ama hazina kutu.

7) hakikisha wamba nafaa zako hizi zimekauka sana na hakuna hata punje moja mbovu ndipo uziwee pamoja na kuazisaga mashine. hakikaisha pia unga unaposagwa unarudiwa mara ya pili ili uwe mlaini usiwe na chenga chenga.

8) baada ya kusaga anika unga wako mahali pakavu hadi upoe, na hakikaisha wakati wa kuanika hautachafua. kuwa safe zaid ni bora ukajitahd nyumban ukawa na kitambaa ambacho unakiweka juu ya ungo wako kisha unamimina unga wako, ukiuweka juani tafuta kitambaa kingine kilicho cha nyavu nyavu uweke kwa juu kufunika unga wako usifwatwe na wadudu ama kupata uchafu.

Ukisha kauka tafuta chombo kikavu uweke na ufunike vizuri kisiwe na sehem ya kupitasha wadudu.
nitarudi baadae kueleza namna ya kuupika uji huu. ila naamini maandalizi ya awali mtakuwa mmesha yapata vyema.

da AshaDii The secretary kumbukeni kwamba uji huu anaweza kulishwa mtoto wa kuanzia miezi 6.

Kwanini zinataiwa ziwe
 
gfsonwin ukiweka kg 1 moja ya ulezi kwa ratio ya vitu ulivyovitaja hapo itakuwa inazidi cha muhimu ulezi uwe kg 2 na vinavyofata viwe katika ratio ya robo kg.

mfano: ulezi kg 2,uwele,ufuta,soya.karanga,na ngano isiyokobolewa mi huwa sipendelei kuwaeka mahindi ikiwa nafaka za aina nyingine nikiwa nimezitumia kwa sababu mahindi hufanya uji kuwa mzito pindi utakapo wekwa kwenye chupa na vilevile huwa na chenga kubwa kwa mtoto anayeanza lishe.

Pia karanga huwa natumia zilizokaangwa na kumenywa ili kufanya unga uwe mlaini na huwa ni vizuri kwa kuwa soya imetumika pia ikiwa na kiwango kikubwa cha protini. Soya inatakiwa ukisha chemsha loweka kwa masaa 24 hadi 48 kabla ya kuanika ikiwa pamoja na kuondolewa maganda.

Ulezi kwa umakini zaidi unaweza kuubuluza kwenye kinu kwa kiwango kidogo kwa sababu kuna ulezi mwingine unakuta hauja pwaguliwa vizuri unakuwa umeshikana na mapumba.kwa wanaopenda kuweka na dagaa wale ambao hawawa kauzu ni vizuri zaidi na huwa una harufu nzuri.

cc: Karucee na Erickb52
 
Last edited by a moderator:
The secretary,
unless kama unapenda unga ambao umezidi ulezi kwa ratio ya robo robo ni sawa ila kwa kufuata viwano vya lishe nusu ni nzuri zaid.

ikumbukwe kwamba ulezi una wanga mwingi zaid ukilinganisha na mahindi, lkn mahindi ya protein na vitamin katika kiini chake, ngano ina ginsen ndani yake hivyo humfanya mtoto akili isichoke na hufanya aweze uwa na akili zaid.

pia nimependa zaid wewe unavyoweka dagaa kwaajili ya calcium ni vizuri sana. yaelekea wanao ni mabonge sana mweeeh!

BTW uji huu ukimpa huzzy mambo yake yanakuwa mazuri sana sana tena ukute una maziwa fresh na siagi isiyokuwa na chumvi.
 
nitaandaa kwa kuzingatia hivyo vipimo kwa ajili yangu mwenyewe. Thanks
 
Niaje kuhusu ratio zenye uwiano sawa? je kunaweza kuwa na tatizo? i.e. ulezi kg 1, ufuta kg1, mahindi ya njano kg1, ngano kg1, soya kg1, dagaa 1/2 ukipenda (kwa kuwa kuna ufuta sidhani kama karanga zinahitajika sana), mbaazi kg 1 je hapo vipi. mie napenda kujitengenezea hivi (mtu mzima).
 
Mara nying watu hutofautisha vipimo... Ndiyo maana unaweza kuta unga wa lishe ambao ukipika uji wake unakuwa mtaamu sana na hali unga mwingine uji wake unapoa na hali vilivyochanganywa ni vile vile ila tofauti huja kwenye vipimo.

So far kwa vipimo hivi vya kwako gfsonwin naona uwiano ni mzuri na uji waweza kuwa mzuri. Alafu umenifanya nitamani uji... Sijanywa kitambo sana.
 
Niaje kuhusu ratio zenye uwiano sawa? je kunaweza kuwa na tatizo? i.e. ulezi kg 1, ufuta kg1, mahindi ya njano kg1, ngano kg1, soya kg1, dagaa 1/2 ukipenda (kwa kuwa kuna ufuta sidhani kama karanga zinahitajika sana), mbaazi kg 1 je hapo vipi. mie napenda kujitengenezea hivi (mtu mzima).

soya ina protein sana ukizingatia umeshaweka ufuta naona kama utazidisha protini
 
Thanks The secretary, na gfsonwin.... na wengine pia. I truly appreciate.
 
gfsonwin,
Halafu mtaani kwangu mijitu utaisikia "baba nasra umenawirije?" we mivyakulati ninayo kopia humu mchezo? utatutaka tunavyogombea bakuli na baby wangu?
 
rafiki yangu gfsonwin nikiweka order naweza kupata?
si unajua situation yangu rafiki?
kununua hivyo vitu sokoni kunatakiwa mwenyewe ndo haswa ufanye hiyo kazi. maana kuna vitu utakuta nusu ni mchanga, sasa kama dada ndo anaandaa ni kujiandaa na appendectomy tu
sasa hawa watoto wanahitaji hayo mambo mazuri tuachane na yale ya shoppers, lol!
 
Last edited by a moderator:
rafiki yangu gfsonwin nikiweka order naweza kupata?
si unajua situation yangu rafiki?
kununua hivyo vitu sokoni kunatakiwa mwenyewe ndo haswa ufanye hiyo kazi. maana kuna vitu utakuta nusu ni mchanga, sasa kama dada ndo anaandaa ni kujiandaa na appendectomy tu
sasa hawa watoto wanahitaji hayo mambo mazuri tuachane na yale ya shoppers, lol!

Jitahidi hata weekend moja jitoe mhanga uandae ni muhimu kuandaa mwenyewe mwandikie list akanunue utengeneze
 
Last edited by a moderator:
unapika kama kawaida ila hakikisha unapika muda mrefu ila usiungue
Thanks The secretary. Ukishachemsha kwa dakika kumi na kutoa maganda, unaroweka tena for 24-48 hours. kwanini? je nikiroweka moja kwa moja bila kuchemsha kwa dakika 10?
Please nikisie muda mrefu. Dakika/Masaa karibia mangapi?
 
Last edited by a moderator:
Please naomba pia kuelekwzwa namna ya kuandaa dagaa kwa ajili ya kutengeza uji huu. Dagaa aina gani ambao ni preferred na wanaandaliwaje?
 
Please naomba pia kuelekwzwa namna ya kuandaa dagaa kwa ajili ya kutengeza uji huu. Dagaa aina gani ambao ni preferred na wanaandaliwaje?

Mi nimezoea dagaa wa kanda ya ziwa unawaosha vizuri bila kutoa vichwa unawaanika nenda sokoni usinunue waliokwisha kuwa kauzu wana shombo chukua wenye rangi yao asilia
 
Back
Top Bottom