Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,690
- 29,909
Habari wakuu.
Leo nimeona nilete kwenu hii hoja kwa mfumo wa swali. Kama nililivyoliweka hapo kwenye heading kuhusu taswira au umbo lionekanalo kwa macho pale inavyowezekana, hawa viumbe ambao tunaaminishwa kupitia imani zetu kwamba wameumbwa kwa moto na upepo wanabeba taswira gani?
Upepo sote tunaufehemu kwamba hauna umbo linaloonekana bali tunauona ukileta matokeo ambayo ni kutikisa ama kuhamisha vitu vinavyoonekana pale unapovipitia. Pia moto tunauona kwa macho ingawa tunasema hauna umbo maalumu wala haushikiki bali nao unapimwa kwa matokeo unayoyaacha kwa mguso ama kuvipitia.
Viumbe ninavyoviongelea, havijawahi kuwa dhahiri kwenye macho yetu kwenye ukawaida wa maisha yetu. Lakini tumekuwa katika kuamini na kujenga taswira ya namna muonekano wa viumbo hivyo vinavyotawala ulimwengu usioonekana. Ingawa kwenye kujenga taswira hizo tumeshuhudia itikadi za nyeupe ni utukufu na nyeusi ni uovu na laana ikipewa kipaumbele.
Kabla sijaendelea, napenda kuuliza jukwaa. KUNA AWAYE YEYOTE AMESHAWAHI KUONA MALAIKA AMA MAJINI? Je unaweza kushare nasi nini ulichoona? (Mimi nimewahi kuona majini na viumbe wengine) lakini kwa kuwa naandika uzi huu napenda kupata ushuhuda wa kutoka kwa wasomaji wengine. Kwenye uzi huu mbeleni nitachangia nini nilichokiona.
Tuendelee sasa.
Ufunuo wa Yohana 4: 6 anaelezea uwepo wa Wenye UHAI wanne. je ni kina nani hao na kama kuna ufafanuzi wa umbo lao ukoje?
Je, tunawezaje kumtofautisha Malaika kutoka kwa Kerubi? Tunamtambuaje Kerubi akiwa amesimama na Serafi? Je jini tunalitofautishaje na mapepo? Shetani na majini wana tofauti gani? Kama jini na mapepo na mashetani wanaweza kukaa ndani ya mtu, je malaika na jamii zao wanaweza pia kukaa ndani ya mtu?
Je viumbe hao wapo au ni illusions zetu wanadamu? Narejea taswira zilizochorwa na akina Michellangelo, Da Vinci, Raphael na wengine enzi za rennainsance?
Karibuni tukate maneno