Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Kutakuwa na faida gani au hasara gani endapo tutaamua kuitisha uchaguzi mkuu mapema na hivyo kuondokana na mlolongo wa kashfa na watuhumiwa wa kashfa mbalimbali na hatimaye kuunda serikali mpya?
Wakati serikali mbalimbali duniani zinapokabiliwa na tuhuma za ufisadi wa viongozi wake huwa zinalazimika kuitisha uchaguzi mpya kwanini na sisi tusiamue kuitisha uchaguzi mpya ili kuunda bunge jipya na hatimaye kupata timu mpya ya viongozi?
Kwa mfano, Bunge likiamua kuikataa hii bajeti inayokuja kwa sababu x,y na hivyo kuonesha kukataa sera za serikali, je tutakuwa tayari kuitisha uchaguzi mkuu mapema?
Je yawezekana tiba ya matatizo yetu kwa wakati huu ni kuamua tu kuanza moja na serikali mpya huku wale wote ambao wanatajwa kuhusishwa na ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka kutokupewa nafasi na kuwekwa pembeni na vyama vyao?
Kwa mfano, baada ya kashfa za matumizi ya fedha ambazo zinaikabili serikali ya Uingereza msukumo mkubwa upo kwa Waziri Mkuu Gordon Brown kujiuzulu na mawaziri wake kadhaa tayari wameamua kuachia ngazi. Na kuna uwezekano ni masaa tu kabla Brown mwenyewe hajaamua kujiuzulu ingawa inaonekana anapata kuungwa mkono kwa wakati huu na watu ndani ya chama chake.
Je, serikali ilivyo sasa yaweza kujikuta inalazimishwa kujiuzulu siyo kwa sababu ya Kikwete ambaye bado anaungwa mkono na wananchi wengi bali kwa sababu ya mawaziri wake ambao ameendelea kuwang'ang'ania licha ya udhaifu mkubwa wa kiuongozi?
Yawezekana kuitisha uchaguzi mkuu mapema unatunusuru na siasa za uchafu na kisasi ambazo zinaelekea kutawala tunapoelekea 2010. Kulisalimisha taifa letu na kuleta uongozi mpya ambao utakuwa na ajenda mpya (ila ya maisha bora imeshindwa) ndiyo njia pekee ya kurudisha heshima na mwelekeo wa ujenzi mpya wa taifa.
Tuendelee kusubiri hadi 2010 kuanza upya, au tuamua kuanza upya mapema kwani inaruhusiwa kikatiba?