Kumekuwa na malalamiko mengi sana dhidi ya JF kuwa inawachafua watu binafsi, taasisi na vyama vya siasa kutokana na tuhuma za uongo. Mzee Mwanakijiji ndiye aliyeanzisha tuhuma za uongo humu JF kuwa kuna ufisadi ndani ya PPF. Sidhani kama alikuwa ana nia mbaya, tatizo ni kuwa kuna ignorance kubwa sana. Watu huwa wanakurupuka na kutoa tuhuma zisizo sahihi.
Moderators wa JF kuruhusu matusi, kejeli na tuhuma za uongo kama hizi ndiyo chanzo cha malalamiko mengi dhidi ya JF. Kuna umuhimu wa free speech ila ni changamoto kwa JF kutoruhusu tuhuma zisizokuwa na msingi, kwani hatimaye JF itapoteza credibility na kuonekana kuwa ni kichaka cha kutoa tuhuma za kutungwa na kashfa na si "The Home of Great Thinkers" kama inavyojitamba.
Mzee Mwanakijiji anayeheshimika sana huku JF alikuja na post inayosema -- "MALIPO YA Mamilioni Parastatal Pensions Fund (Invoices): Rewarding and Defending Corruption"
Imekuja kubainika kuwa zile tuhuma za malipo kwa menejimenti ya PPF zilizoanzishwa na Mzee Mwanakijiji humu JF ambaye aliziita kimakosa kuwa ni "corruption" na kudakiwa na Zitto Kabwe na kamati yake ya POAC, si tuhuma sahihi.
Kuhusu hii post mpya yenye kichwa cha habari: "Hivi SSRA ni kichaka cha mafisadi wa PPF? SSRA Haitaipendelea PPF kwenye ufisadi na uizi?", huu ni uzushi na udaku mtupu.
Kazi zilitangazwa SSRA na zikafanywa interview pale. Ukweli ni kuwa wafanyakazi kutoka mifuko mbalimbali ya pensheni, ikiwemo PPF, NSSF, PSPF, LAPF na kutoka sekta ya fedha waliomba kazi SSRA na kulikuwa na ushindani mkubwa.
Baada ya interview, waliokuwa wafanyakazi kadhaa wa PPF wakapita na kushinda nafasi za kazi SSRA. Pengine hii ni sifa kwa PPF kuwa na wafanyakazi wenye sifa kubwa na shirika lenyewe kuheshimika mpaka wakapata nafasi za kazi SSRA.
These are the real facts. Hakuna ufisadi wowote PPF kama inavyodaiwa humu JF kila mara. Ukweli ni kuwa mfuko huu umepewa "clean audit opinion" na CAG na good governance award kwa nchi za Afrika.
Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye amewahi kuwa director general wa NSSF na hivyo anafahamu vizuri uendeshaji wa mifuko ya pensheni Tanzania amesema kuwa malipo hayo yanayolalamikiwa sana PPF ni sahihi na yanafanywa na kila shirika la umma tangu miaka ya 1990s. Mkulo amesema kuwa malipo hayo ya gratuity na group endowment scheme yamepitishwa kisheria na serikali, hivyo PPF haijavunja sheria yoyote. Hakuna rushwa, wizi wala ubadhirifu wowote wa pesa.
Jamani wana JF tuache kukurupuka na kuharibu credibility ya JF kuifanya ionekane kama jukwaa la kashfa, matusi, kejeli, uongo na tuhuma zisizokuwa na msingi.
Mkulo defends PPF managers' payments
By ALVAR MWAKYUSA in Dodoma, April 20, 2011
MINISTER for Finance Mr Mustafa Mkulo has said the gratuity and endowment payments to management of Parastatal Pension Fund (PPF) were in line with regulations.
The minister made the clarification in the National Assembly on Wednesday evening while contributing to reports by three parliamentary committees, presented to the House earlier in the morning.
"The payments are in accordance with the decision of the PPF Board of Trustees in 2002. The management of the fund operates on a contractual basis and they are entitled to the gratuity.
PPF employees are of two categories, permanent and pensionable and those on contracts," elaborated the minister.
Apart from gratuity, the fund has in place arrangement for group endowment to all its employees which is paid to employees who have completed their terms of service, retiring, retrenched or deceased.
"The gratuity and endowment payments attract a 30 per cent deduction in taxes and are paid according to the law," maintained the minister.
He said the endowment payments are made to all employees of the pension fund, adding that they were designed in the early 1990s under the then National Insurance Corporation (NIC).
If the payments are to be stopped then the management of PPF has to be hired on permanent basis, said Mr Mkullo.
The Parliamentary Public Organisations Account Committee (POAC) had recommended that the Controller and Auditor General (CAG) and the Treasury Registrar intervene in the matter, saying the payment system gave room to double payment in the form of gratuity and endowment benefits.
Source: (Daily News | Mkulo defends PPF managers' payments)
Najua watakurupuka watu humu JF na kusema nimetumwa, nimehongwa, kwa kuitetea PPF kama kawaida ya watu kukurupuka. Lakini tusimame kwenye facts na mambo yaliyo sahihi. Tujenge hoja kwa kutumia facts na si matusi, kejeli na tuhuma za kutungwa.
Ngao One,
Without research, no right to speak.
Inawezekana ukawa unajaribu kutaka kudodosa ili kujua ukweli.
Ukweli ni kuwa Mustapha Mkulo kalidanganya Bunge na waheshimiwa wabunge. Mkulo bila kufanya utafiti, kakurupuka kwa kudanganywa na William Erio kuwa malipo haya ni sahihi.
Utaratibu wa Group endowment upo PPF na hauna utata, tatizo waliolipwa sio walengwa. Utaratibu huu ulianzishwa ili kutoa golden shake hand kwa wafanyakazi wa kudumu pale wanapostaafu kwa kufikisha miaka 55.
Wafanyakazi wa mikataba wana malipo yao yanayoitwa gratuity. Kosa lililopo ni hawa wakurugenzi ambao ni wa mikataba kuamua kujilipa pia group endowment ambayo sio haki yao. hili ndilo kosa. Mkulo anasikisha na sijui CPA yake kama ni sahihi, malipo kutozwa kodi sio kigezo cha uhalali.
Mkulo na serikari yake wanatakiwa kupata ukweli toka kwa wafanyakazi wasio wa mkataba hasa hasa aliyekuwa Mhasibu Mkuu mwaka 2008. Huyu anajua vizuri. Pia serikali wasome majibu ya wakurugenzi kwa Bodi ya wadhamini vikao vya May, 2008 na June 2008 wataona jinsi majibu ya kila wakati yanavyotofautiana.
Serikari pia iangalie malipo ya Mr. David Mattaka alipokuwa kwenye mkataba, ione kama alilipwa group endowment. Mattaka alilipwa 25% gratuity kwa miezi 19 tu aliyofanyia kazi. Kama alistahili group endowment, kwa kipindi cha mkataba mbona hakupewa, apewe sasa kama aliibiwa.
Mkulo anaposema If the payments are to be stopped then the management of PPF has to be hired on permanent basis, kwahiyo waendelee kuiba kwa kuwa Waziri anaogopa kuwaajiri kwenye mfumo wa kudumu.
Naandaa majibu mazuri kwa mpangilio na ushahidi kuwa PPF Management wameliibia shirika.