Tuhoji Gharama za Safari za Nje za Viongozi wetu!

Zed

JF-Expert Member
Mar 28, 2009
435
257
Uwingi viongozi wa juu na safari zao za nje ya nchi ni mzigo kwetu watanzania. Ni hivi majuzi tu waziri mkuu amerejea kutoka Brazili na Marekani, leo hii Makamu wapili rais wa Zanzibar yuko Uchina, Makamu wa rais yuko Uswiss, baada kurejea kutoka Msumbiji na rais mwenyewe ameelekea Australia. Je nina analipiga gharama hizi zote? Je kwa matumizi haya kodi za wanachi zinatumika vema. Wabunge tunaomba kikao kijacho ulizeni gharama za safari ili wnanchi tujue!
 
kusafiri sio shida, tabu yangu ni msafara wake ulivyo mkubwa sana, ukilinganisha na faida tunzopata.....yani inauma kweli na kodi ninayokatwa halafu kijijini kwetu hata maji hamna na ndugu zetu hata madawa kwenye zahanati ni za shida...ww ngoja tu iko siku
 
Kuhoji safari za nje za viongozi ni mbali sana . Hata safari za ndani tu zina mswali mengi.

Hoji gharama iliyotengwa kwa mafuta ya wiki ya VX ya wiziri au mkurugenzi wa wizara kuutoka masaki hadi Posta alafu linganisha na ghaama za mafuta inazopewa gari za dharura za Polisi. au ya ya kufanya patrol.

Hushangai gari ya polisi inaosa mafuta lakini gari ya kibosile tena VX haijwai kukosa mafuta.

Siasa ndio UTI wa mgongo wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom