Tuelimishane: Sakata la Mafuta ya kula (TRA vs. TBS) - Hiki ndicho kinachobishaniwa

Even though uzalishaji wa ndani ni mdogo , kwanini hawa wafanyabiashara wasistimulate uzalishaj wa ndani? Wao wanakimbilia kule nje maana wanachota pesa za bure tuu! They should be creative ili walinde uchumi wetu sio kunufaika wao tuu na nchi inabaki kuwa na deficit kila siku. Hawaoni wenzao walilijua mapema wakaanza kujenga viwanda vya mafuta ya alizeti? Tuwe wazalendo bwana hatuwez kuachia market maker wakacontrol uchumi wetu. JPM ni mzalendo na mbunifu sana sana ! Hata India na baadhi ya nchi wamevalia njuga suala hili la mafuta na sukari.
 
Tukubaliane kwamba, wafanyabiashara wana uaminifu mdogo sana! Hakuna importer wa bongo anayeweza kukupa ukweli, hadi uhangaike saaana! Bahati mbaya hata wakikamatwa, adhabu ni ndogo sana ukilinganisha na faida ya udanganyifu.

Tujiulize kwa nini wote sasa wanagiza mafuta ghafi? Ni kweli viwandani kwao wanafanya refinement kwa wingi kiasi hicho? Ukiuliza vijana wetu viwandani utaambiwa udanganyifu wa ajabu sana!

Tatizo pia liko Bungeni. Muagizaji anakuwa mbunge, halafu anawekwa kamati ya biashara na viwanda eti aishauri serikali kukamata kodi! Haiwezekani. Maabara zinanunuliwa kwa bei rahisi kabisa na kusema uongo kweupeee!
BASI ITABIDI TRA WAWE NA MAABARA YAO.KWA SABABU KAMA TBS WANAWEZA KUNUNULIWA KWA BEI RAHISI ITASHINDIKANAJE "TBS" YA MALAYSIA KUNUNULIWA?
 
Mtoa uzi nina hoja mahususi
1. Umegusia tu mgongano wa kimamlaka kati ya TBS na TRA lakini kuna taasisi inaitwa TFDA ambayo inahusika na ishu za madawa na vyakula na hapa issue ni mafuta ya kula hilo likoje?
2.Kwa uelewa wangu TRA ni wakusanyaji kodi,TBS wazee wa viwango na TFDA ni mamlaka ya Vyakula,dawa na vipodozi je hao hawatoweza kutuondolea utata huo? Maana wao wanazo maabara kabisa ambazo zinaweza kupima na kujua,sina hakika kama TRA na TBS kuwa na maabara
3.Je,hakuna uwezekano wa hivi vyombo 3 kufanya joint venture/muunganiko wa kiutendaji ili kuondoa ishu kama hizi utata?
Nawasilisha
Yaani huna uhakika kama TBS wana maabara?
 
Hapo tatizo ni sheria, hakuna kiwango cha kodi mtu anapoingiza mafuta ambayo ni semirefined, Hapo nyuma yalikuwa yanaingia lkn kwa kuhesabiwa kuwa ni crude oil na itahesabika hivo baada ya kutembeza mrungula.
Kuna ukweli kiasi flani. Narudia kusema mifumo yetu ya ulipaji kodi Tz haiko wazi. Ni tatizo la Wizara ya Fedha, TRA na serikali yote.
 
Habari wakuu.

Sasa kama nchi tuna sakata la mafuta ya kula. Yamekwama bandarini.

Msingi wa kukwama ni ubishani kati ya mamlaka za serikali hasa TRA vs. TBS
Mamlaka ya Mapato (TRA) yenye wataalam wa kodi na Shirika la Viwango (TBS) yenye wataalam wa viwango na ubora.

Kinachobishaniwa ni je yale yaliyopo bandarini ni mafuta "ghafi" au "safi"?.

Kabla sijaeleza zaidi natoa hitimisho hili. Hakuna namna TRA na TBS watakuja kukubaliana ktk hili hata ashuke malaika gani.

Sababu ni kwamba mtazamo wa kimantiki kati ya hizi taasisi mbili ni tofauti kabisa.

Katika hili serikali inajaribu kuunganisha ncha ya kaskazini na ncha ya kusini. Haitawezekana. Nitaeleza.

Mantiki ya "u-ghafi" na "u-safi" kwa TBS:
- TBS wanatumia kigezo kikubwa kimoja kuamua kwamba ni ghafi au ni safi. Kigezo hiki ni je haya mafuta yanafaa kwa mlaji au bado yanatakiwa kusafishwa zaidi ndio yafae kwa mlaji?!. Kwa sababu kiuhalisia mafuta yanayoletwa na hivi viwanda ni "concentrate" na huja kusafishwa na kuchujwa na kupakiwa Ndio yanakuwa tayari kwa mlaji; basi TBS wataamua kuwa ni "ghafi".

- "Concentrate" ya mafuta haifai kuliwa, hivyo kwa viwango ni "ghafi". Simple like that.

- Kisichofaa au ambacho hakijawa tayari kwa kula/kutumika kwa TBS ni lazima kiwe ghafi.

Mantiki ya "u-ghafi" na "u-safi" kwa TRA:
- Hawa ni wataalam wa kodi. Swali la wengi limekuwa wanawezaje kusema haya ni mafuta "ghafi"?. Wana maabara?.
Jibu ni kwamba hawana maabara lakini wanaweza kusema ni "ghafi" au "safi"

- Kwanza hawatumii maabara kuamua hilo. Wao wana kanuni moja ya "sharia ya forodha ya Afrika Mashariki". Hii ni kanuni ya "asili ya bidhaa ni nchi ipi?" kwa kiingereza ni EAC RULES OF ORIGIN

- Kiufupi sheria ama kanuni hii inasema "bidhaa itahesabika imetengenezwa katika nchi flani ikiwa sehemu kubwa ya uzalishaji imefanyika ktk nchi hiyo". Hii ni kanuni inayotumika kutafuta nchi ilikotengenezwa bidhaa pale ambapo bidhaa hiyo hutengenezwa ktk nchi A na kwenda kumalizia utengenezaji ktk nchi B.

Sasa kwenye ishu ya mafuta:
Kwa kuwa yanaagizwa huko Indonesia n.k yakiwa ni "concentrate" (yani yamekuwa processed kiasi) na kuja kumalizia utengenezaji Tz basi ni nchi ipi bidhaa hii itakuwa ime procesiwa zaidi?

Kama uzalishaji mkubwa umefanyika INDONESIA na kwa uchache huku Tz basi hiyo itahesabika yamezalishwa fully huko huko Indonesia. Na kodi itapigwa kama mafuta kamili hata kama kuna hatua chache za kumalizia huku Tz.

Huo Ndio ufafanuzi mdogo. Nimetumia lugha nyepesi zaidi ili kueleweka.

Kwa mantiki hizo hakuna namna TRA na TBS wakakubaliana. Haipo. Haipo. Haipo!

Ombi langu kwa serikali:
Iweke mifumo mizuri ili haya mambo yawe yanashughulikiwa na vyombo sahihi.

Wanaweza kwenda South Africa ambao wako vizuri sana kwenye mifumo ya "RULES OF ORIGIN" na wakajifunza.
Hapa Tz ni TCCIA (Tz Chamber of Commerce and Industries Association) ndo wenye jukumu hilo ingawa hawana wataalam na hawaaminiki pia.

Naishia hapo.

Ahsanteni.
Ambacho hujasema mkuu ni kuwa nyundo ya TRA inalima kodi iliyotulia kwenye 'concentrate' kama 'final product'. Huo ubishani wote ni kodi tu.
 
Waziri mkuu kasema ataingia mtaani kusaka walioficha mafuta, kwanini mda huo wasiutumie kwenye kutatua mgogoro uliopo kati ya TBC na TRA..
 
Even though uzalishaji wa ndani ni mdogo , kwanini hawa wafanyabiashara wasistimulate uzalishaj wa ndani? Wao wanakimbilia kule nje maana wanachota pesa za bure tuu! They should be creative ili walinde uchumi wetu sio kunufaika wao tuu na nchi inabaki kuwa na deficit kila siku. Hawaoni wenzao walilijua mapema wakaanza kujenga viwanda vya mafuta ya alizeti? Tuwe wazalendo bwana hatuwez kuachia market maker wakacontrol uchumi wetu. JPM ni mzalendo na mbunifu sana sana ! Hata India na baadhi ya nchi wamevalia njuga suala hili la mafuta na sukari.
We ni kilaza. Huna akili
 
Tukianza kuona kila kilichokuwa kikifanyika nchini kilikuwa ni cha wizi wizi haki ya nani hizo biashara tutazifanya na familia zetu ndani ya majumba yetu...
Viwanda tutavionea kwenye vitabu vya hadithi na movi za kiindonesia..
Maendeleo ya wananchi yatahamia kwenye kuumarisha nguvu ya polisi ili watu walazimishwe kuamini nyeupe ni nyeusi..!!
Wale wawekezaji wakubwa watakimbilia nchi zingine siye huku tutabaki na uwekezaji wa chini ya kitovu..!!
 
mtoa mada hebu nieleweshe, miaka ya nyuma walikua wanakubaliana vipi? au hayo mafuta yameanza kuagizwa hivi karibuni tu?
Miaka ya zamani no body cared, matatizo yanajitokeza wakati huu sababu hatukushughulika kuondoa mlolongo wa hii migongano na mikanganyiko ya sheria, kanuni na taratibu mbalimbali.
Hutokea hivyo sababu kila taasisi inakuwa makini kufanya kazi yake kwa kufuata sheria na kanuni zake. cha msingi tuandae miongozo mipya ya kuamua nini kifanyike yanapojitokeza mambo kama haya ya mafuta au tufute kabisa baadhi ya sheria tata.

Na utaratibu wetu wa kodi ni shida bado, kuna utitiri wa kodi kuliko inavyo takiwa. Utitiri wa vibali vya mamlaka kibao hadi kero
Yaani upate kibali TBS, TFDA, ....., n.k.
 
Habari wakuu.

Sasa kama nchi tuna sakata la mafuta ya kula. Yamekwama bandarini.

Msingi wa kukwama ni ubishani kati ya mamlaka za serikali hasa TRA vs. TBS
Mamlaka ya Mapato (TRA) yenye wataalam wa kodi na Shirika la Viwango (TBS) yenye wataalam wa viwango na ubora.

Kinachobishaniwa ni je yale yaliyopo bandarini ni mafuta "ghafi" au "safi"?.

Kabla sijaeleza zaidi natoa hitimisho hili. Hakuna namna TRA na TBS watakuja kukubaliana ktk hili hata ashuke malaika gani.

Sababu ni kwamba mtazamo wa kimantiki kati ya hizi taasisi mbili ni tofauti kabisa.

Katika hili serikali inajaribu kuunganisha ncha ya kaskazini na ncha ya kusini. Haitawezekana. Nitaeleza.

Mantiki ya "u-ghafi" na "u-safi" kwa TBS:
- TBS wanatumia kigezo kikubwa kimoja kuamua kwamba ni ghafi au ni safi. Kigezo hiki ni je haya mafuta yanafaa kwa mlaji au bado yanatakiwa kusafishwa zaidi ndio yafae kwa mlaji?!. Kwa sababu kiuhalisia mafuta yanayoletwa na hivi viwanda ni "concentrate" na huja kusafishwa na kuchujwa na kupakiwa Ndio yanakuwa tayari kwa mlaji; basi TBS wataamua kuwa ni "ghafi".

- "Concentrate" ya mafuta haifai kuliwa, hivyo kwa viwango ni "ghafi". Simple like that.

- Kisichofaa au ambacho hakijawa tayari kwa kula/kutumika kwa TBS ni lazima kiwe ghafi.

Mantiki ya "u-ghafi" na "u-safi" kwa TRA:
- Hawa ni wataalam wa kodi. Swali la wengi limekuwa wanawezaje kusema haya ni mafuta "ghafi"?. Wana maabara?.
Jibu ni kwamba hawana maabara lakini wanaweza kusema ni "ghafi" au "safi"

- Kwanza hawatumii maabara kuamua hilo. Wao wana kanuni moja ya "sharia ya forodha ya Afrika Mashariki". Hii ni kanuni ya "asili ya bidhaa ni nchi ipi?" kwa kiingereza ni EAC RULES OF ORIGIN

- Kiufupi sheria ama kanuni hii inasema "bidhaa itahesabika imetengenezwa katika nchi flani ikiwa sehemu kubwa ya uzalishaji imefanyika ktk nchi hiyo". Hii ni kanuni inayotumika kutafuta nchi ilikotengenezwa bidhaa pale ambapo bidhaa hiyo hutengenezwa ktk nchi A na kwenda kumalizia utengenezaji ktk nchi B.

Sasa kwenye ishu ya mafuta:
Kwa kuwa yanaagizwa huko Indonesia n.k yakiwa ni "concentrate" (yani yamekuwa processed kiasi) na kuja kumalizia utengenezaji Tz basi ni nchi ipi bidhaa hii itakuwa ime procesiwa zaidi?

Kama uzalishaji mkubwa umefanyika INDONESIA na kwa uchache huku Tz basi hiyo itahesabika yamezalishwa fully huko huko Indonesia. Na kodi itapigwa kama mafuta kamili hata kama kuna hatua chache za kumalizia huku Tz.

Huo Ndio ufafanuzi mdogo. Nimetumia lugha nyepesi zaidi ili kueleweka.

Kwa mantiki hizo hakuna namna TRA na TBS wakakubaliana. Haipo. Haipo. Haipo!

Ombi langu kwa serikali:
Iweke mifumo mizuri ili haya mambo yawe yanashughulikiwa na vyombo sahihi.

Wanaweza kwenda South Africa ambao wako vizuri sana kwenye mifumo ya "RULES OF ORIGIN" na wakajifunza.
Hapa Tz ni TCCIA (Tz Chamber of Commerce and Industries Association) ndo wenye jukumu hilo ingawa hawana wataalam na hawaaminiki pia.

Naishia hapo.

Ahsanteni.
Mawese yetu kule Kigoma hatuna uwezo kuongeza uzalishaji ili tujitosheleze kwa mafuta? Hao wanazalisha ziada kwa nchi zao wana ardhi kuliko sisi?
 
Back
Top Bottom