Tuambie Mechi yako Bora zaidi ya soka ambayo umewahi kuishuhudia

Liverpool vs Ac Milan - Istanbul 2005. (Miracle of Istanbul)

Wenyewe wanakuambia hawezi sahau, password za wengii kwenye Account(Gmail/yahoo etc) zilikuwa na neno hilo. (Istanbul)
 
Italy vs Germany 2006 world cup semi final Del piero alifanya unyama Sana pale pale ardhi ya wajerumani alipiga bonge la curve hatari
Also Liverpool vs Barcelona Origi anawaua chuma ya nne one of the best comeback in Ucl

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nimekuwa shabiki wa soka kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka 20 sasa. Nimeangalia mechi nyingi sana na za kutosha, zaidi ya 1000 hadi leo hii.

Toka enzi za goli la dhahabu hadi leo hii ambapo goli la ugenini limefutwa kwenye mashindano ya Ulaya na technolojia ya VAR inatumika.

Nimeangalia fainali 6 za kombe la dunia, toka 2002 hadi 2022. Nimeangalia zaidi ya fainali 14 za Uefa Champions league. Nimeangalia mechi nyingi sana za mashindano tofauti tofauti na zenye matukio ya kusisimua na matokeo ya kustaajabisha....Jaribu kuwaza,,

Nani amesahau kuhusu usiku wa Liverpool dhidi ya Ac Milan 2005?..Je ile comeback ya Barcelona dhidi ya PSG 2017?...vipi kuhusu usiku wa Drogba pale Allianz Arena 2012?....Bila shaka wote tunakumbuka goli la Iniesta lilivyowapa ubingwa Spain mbele ya Uholanzi pale Soccer city kwa madiba....Na vipi kuhusu ile Acrobatic ya Wayne Rooney dhidi ya Man city dakika za kuelekea mwisho kabisa kwenye mechi muhimu ya kuamua bingwa wa EPL 2010/2011...Mungu amlaze pema Cheikh Tiote anayetukumbusha Comeback ya Newcastle dhidi ya Arsenal game ambayo Newcastle wanatoka nyuma kwa bao 4 na kufanya matokeo kuwa 4 kwa 4...vip kuhusu Madrid dhidi ya City UCL mwaka jana?

Hakika kuna mechi nyingi sana ambazo tumezishuhudia na kuzifurahia. Na ambazo zilituacha na kumbukumbu nzuri sana mioyoni mwetu. Lakini pamoja na hayo, kuna mechi moja ambayo kwangu mimi nimeiweka katika kilele cha ubora. Ndiyo, ni Mechi Bora zaidi ya soka ambayo nimewahi kuishuhudia. Unataka kuifahamu?

Usipate tabu, rudisha kumbukumbu zako hadi Jioni ya Tarehe 18.12.2022 pale Qatar...ARGENTINA vs FRANCE....Dakika 120 za dhahabu. Ni mechi kubwa iliyoamuliwa na wachezaji wakubwa katika hatua kubwa ya mshindano makubwa zaidi ya soka duniani.

Kwangu mimi Argentina Vs France ndio mechi yangu bora zaidi ya soka niliyowahi kuishuhudia toka nimeanza kuangalia soka....

Tuambie kwa upande wako, ipi mechi bora kwako!!!
Mechi ya Champions league mwaka 2000 Realmadrid vs Valencia ilikuwa binge la mechi
 
Kwangu mimi mechi bora inabaki kuwa kati ya Bayern Munich vs Manchester united mwaka 1999 usiku wa kukumbukwa kwa timu ya Manchester.

Hii mechi mpaka inaenda dk ya 90 ilikuwa Bayern anaongoza goli 1 kwa bila Ferguson alifanya sub za dakika ya mwishoni mpaka mwamuzi wa mchezo aliona Ferguson anapoteza tu muda huku mashabiki wa Bayern wakishangilia kuwa uefa tayari ni mali yao.

Bayern hawakuamini macho yao kwa magoli ya dk za lala salama ya ted 91 ole guna 93 na mchezo ukawa umeisha hapo.

Mpaka leo kichapo chochote Bayern akimpa man u bado anaona akitoshi kulipiza kisasi icho.
 
Chelsea walianza lambwa mbili kwanza kipindi cha kwanza, nilikaa na kaka yangu shabiki wa Chelsea alinuna balaa yaani. Nikawa nacheka kama mwehu ndiyo kwanza nikamtia hasira, walivyosawazisha alishangilia kama hamnazo. Isingekuwa sub ya lampard ingeisha 4-2
Mkuu mimi kipundi hicho nilikua na jamaa yangu ni shabiki wa Liverpool alinifunga shati kama wanavyofungwa wafungwa wawili asee ilikua na tension kubwa sana.
 
Hizo za 90 uliziona au uliona marudio
1994 kombe la Dunia lilichezwa Marekani na mechi zilikuwa zinaanza saa 8:30 usiku. Mnalala kwanza kisha mnaamka mnaangalia mechi. Nikiwa Shinyanga kipindi hicho mechi zinaonyeshwa Bitiama Hotel na Bwalo la Polisi.
1999 nyumba nyingi zilishanunua TV tukitumia madishi makubwa. Hii niliiangalia nyumbani kwangu sebleni kwenye TV niliyonunua mwenyewe.
Umenielewa Mkuu?
Mimi nimeanza kuangalia live kombe la Dunia 1990 ushindi wa Germany dhidi ya Argentina kwa goli la penati ya Andreas Brehme.
 
1994 kombe la Dunia lilichezwa Marekani na mechi zilikuwa zinaanza saa 8:30 usiku. Mnalala kwanza kisha mnaamka mnaangalia mechi. Nikiwa Shinyanga kipindi hicho mechi zinaonyeshwa Bitiama Hotel na Bwalo la Polisi.
1999 nyumba nyingi zilishanunua TV tukitumia madishi makubwa. Hii niliiangalia nyumbani kwangu sebleni kwenye TV niliyonunua mwenyewe.
Umenielewa Mkuu?
Mimi nimeanza kuangalia live kombe la Dunia 1990 ushindi wa Germany dhidi ya Argentina kwa goli la penati ya Andreas Brehme.
Sawa mkuu
 
Alafu extra aliingia marcelo upande mmoja di maria upande mwingine marcelo atletico aliita maji mma ila ni kweli walionewa lile goli la ramos la kusawazisha lilikua offside
Ulisimuliwa au ulitazama mwenyew. Alisawazisha kwa kona sasa offside itokee wapi.
 
National team fainali yangu bora ni ARGENTINA na france.

France tuliwafanya mbaya na hawatosahau, wamecheza na timu bora na mchezaji bora kuwahi kutokea.
 
UEFA 98/99
The competition was won by Manchester United, coming back from a goal down in the last two minutes of injury time to defeat Bayern Munich 2–1
 
1. Brazil vs France 1998 nililia
2. Senegal vs France 2002 nililia
3. Senegal vs Uturuki 2002 nililia
4. Arsenal vs barca 2006 niliumia

2005 ac milan na liver/ 2021 liver na barca hizi mechi mbili kwangu ni bora sana sababu nilikuwa emotional sana yaan saut ilikata kabisa mechi nyingi ile ya simba na nkana nilijuwa uwanjan saut ilikata

Ila mechi ya man u vs madrid ile ya 3-3 delima akitupia huku nestroy akitupia ndo mechi bora kabisa kuwah kuona sikutaka iishe sababu ya utam wa ball
 
Back
Top Bottom