Trump: Siwezi kukubali matokeo ya kushindwa

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Trump amesema kupitia debate ya Jana alipoulizwa swali na moderator kuwa je atakubali matokeo ya uchaguzi endapo atashindwa?

Amesema siwezi kukubali sasa nitakubali badae siwezi kuongea kwa undani nitaongea baadae.

Kama kawaida aliendeleza mashambulizi yake kwa kumrushia maneno makali tena Hillary Clinton na kuonyesha chuki yake zidi ya wanawake.

My take : kwanini hataki kukubali matokeo endapo atashindwa?

Au kashajua kwamba hawezi shinda?

=========
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump amesema kuwa atakubali matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani ''iwapo atashinda'' .

Amesema kuwa atakubali matokeo ya moja kwa moja yasio na udanganyifu wowote akiongezea kuwa ana haki ya kupinga matokjeo hayo iwapo hayatakuwa na utata.

Alionekana katika mkutano mjini Delaware jimbo la Ohio ,akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya mjadala wa tatu wa urais dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton.

Bwana Trump amekuwa akikosolewa kwa kusema kuwa hatakubali matokeo ya uchaguzi huo.

Donald Trump alikataa kuahidi kukubali matokeo ya uchaguzi iwapo atashindwa, katika mjadala wa mwisho wa urais dhidi ya Hillary Clinton.

"Nitakuambia wakati huo" alimwambia muendesha mjadala Chris Wallace. Kwa siku kadhaa amedai kuwa kuna 'udanganyifu' katika uchaguzi huo.

Mjadala huo wa televisheni Las Vegas uliendeleza uhasama katika kampeni huku Trump akimuita Bo Clinton "mwanamke muovu".

Kura za kutafuta maoni zinaonyesha Trump poteza umaarufu katika majimbo makuu baada ya kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono.

Mjadala huo wa mwisho wa umefanyika wiki tatu kabla ya siku ya uchaguzi Novemba 8.

Wagombea hao walikataa kusalimiana kwa mikono kabla na baada ya majibizano hayo ya kisiasa, hatua iliyofungua kile ambacho baadaye kiligeuka kuwa mjadala wa kelele na kukatizana kauli.

Trump alitoa ahadi kwa wanachama wa Republican kuwateua majaji wa mahakama ya juu zaidi wanaoegemea 'mrengo wa kihafidhina' watakaogeuza sheria kuu inayohalalisha uavyaji mimba Marekani na kulinda haki za kumiliki bunduki.

Alisisitiza ahadi yake ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji ambao hawakusajiliwa na kudhibiti mipaka ya Marekani.

Wakati huo huo, Bi Clinton ametangaza wazi kuwa atawatetea wapenzi wa jinsia moja, atalinda haki za kuavya mimba, atalenga kuinusha watu wa kipato cha wastani na kushinikiza kulipwa sawa kwa wanawake.

"Serikali haina shughuli yoyote katika maamuzi wanayofanya wanawake," alisema.

Katika mojawapo ya nyakati zilizokuwa na mvuto, Trump alikataa mara mbili kusema iwapo atakubali matokeo ya uchaguzi, hatua iliyobadili utamaduni wa muda mrefu wa wagombea wanaoshindwa kukubali matokeo baadaya kura kuhesabiwa.

"Hilo ni jambo la kuogofya," Clinton akajibu kwa ukali.

"Anaponda na kudharau demokrasia yetu. Na mimi kivyangu, nimeshangazwa kuwa mtu ambaye ni mgombea mteule wa mojawapo wa vyama viwili vikuu anaweza kuchukua msimamo wa aina hiyo."

Majibu ya Trump yamezusha shutuma kali kutoka kwa seneta wa Republican Lindsey Graham, aliyesema mgombea huyo "hawajibi ipasavyo kwa chama chake na taifa kwa kuendelea kuashiria kuwa anafanyiwa udanganyifu katika uchaguzi ujao," kwa mujibu wa taarifa.

Kauli nyingine kuu katika mjadala katika chuo kikuu cha Nevada ni :

  • Bi Clinton anasema Putin anataka Trump achaguliwe kwasababu anataka kinyago awe rais wa Marekani.
  • "Tuna watu wabaya na tuta watoa," amesema Trump, aliposhinikiza ahadi yake ya kujenga ukuta mpakani.
  • Bi Clinton amesema ataidhinisha mpango mkubwa wa ajira kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia.
  • Trump ameashiria bi Clinto na rais Barack Obama walipanga ghasia katika mkutano wake wa kisiasa Chicago mapema mwaka huu.
Chanzo: BBC
 
Ila mimi huyu jamaa nimempenda sana.. he speaks his mind.
 
Ukiona hivyo juwa kwisha kabisa hana uwezo anataka kutengeneza mazingira kuonyesha kaibiwa kumbe ukilaza wake kama hapa Tanzania hata kampeni haijanza MTU anasema ataibiwa kura kumbe hana uwezo wengine wangombea miaka nenda rudi wimbo huohuo
 
Uchaguzi wa Mwaka huu Marekani umeshambuliwa na Virusi vya Siasa za Ki Africa.

1) Kampeni zinahusu kushambuliana na kudhalilishana na kununua Media za kuchafuana

2) Hakuna Mpambano wa kisera wala wa Kimkakat Kama ilivyo Africa

3) Hillary Clinton kishatangaza kuwa akina Trump wamepanga kuiba kura zake
4) Jimbo mojawapo Jana imetangazwa mfumo umevurugwa kwa kutowatambua Wapiga kura halali.
5) Usaliti wa Kivyama kwa baadhi ya Wanasiasa hasa Republican akina Condlize rice kutangaza kujitenga na Trump

6) Siasa za Kibaguzi wa Dini na Rangi Kama ilivyo Africa

7) Mataifa ya nje kuingilia Uchaguzi Kama ilivyo Africa ( Urusi inatuhumiwa kumsapoti Trump)

8) Trump katangaza kutokutambua Matokeo Kama ilivyo kwetu Africa

9) Rais alipo Madarakani kuonesha Upendeleo wa wazi wazi Kwa Mgombea Mmoja kama ilivyo Africa ( Obama katangaza Trump hafai hata kuwa Mhudumu Dukani)

10) .......
 
Huyu jamaa mwanzo kabisa akitangaza nia nilimuunga mkono lakini kadri siku zilivyosonga na kusikia speech zake sina hamu nae tena, na mwaka huu America wamepitisha wagombea wabovu hadi sasa hivi wanatafuta aliye na unafuu kwa ubovu ndo wamchague kwa kuwa hamna namna.
 
Uchaguzi wa Mwaka huu Marekani umeshambuliwa na Virusi vya Siasa za Ki Africa.

1) Kampeni zinahusu kushambuliana na kudhalilishana na kununua Media za kuchafuana

2) Hakuna Mpambano wa kisera wala wa Kimkakat Kama ilivyo Africa

3) Hillary Clinton kishatangaza kuwa akina Trump wamepanga kuiba kura zake
4) Jimbo mojawapo Jana imetangazwa mfumo umevurugwa kwa kutowatambua Wapiga kura halali.
5) Usaliti wa Kivyama kwa baadhi ya Wanasiasa hasa Republican akina Condlize rice kutangaza kujitenga na Trump

6) Siasa za Kibaguzi wa Dini na Rangi Kama ilivyo Africa

7) Mataifa ya nje kuingilia Uchaguzi Kama ilivyo Africa ( Urusi inatuhumiwa kumsapoti Trump)

8) Trump katangaza kutokutambua Matokeo Kama ilivyo kwetu Africa

9) Rais alipo Madarakani kuonesha Upendeleo wa wazi wazi Kwa Mgombea Mmoja kama ilivyo Africa ( Obama katangaza Trump hafai hata kuwa Mhudumu Dukani)

10) .......
SA IVI WANAIGA AFRIKA
 
Back
Top Bottom