sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,064
Hata obama huyuhuyu ambae kaanza kusingizia uongo kwamba trump anatembelea trend ya uchumi aliouacha ni muongo sana, kiukweli obama alisema "haiwezekani" uchumi wa marekani kurudi upya uwe imara labda uchawi ukitumika iwapo trump atachaguliwa.
Trump kafanya mara 10 ya walichodhani hakiwezekani ila fake news kama cnn, msnbc, cbs, nbc, n.k zimeungana na democrats kubeza mafanikio, hata hivyo haisaidii kitu kwasababu wahapewa jina fake news
Tangu aingie:
1, kwa mara ya kwana ukuta umejengwa, imesaidia mno kupunguza maharamia haramu wasio na vibali wanaochangia mno uhalifu
1. Ajira milioni 7
2. Kwa mara ya kwanza nafasi baadhi ya kazi zimezidi wanaozitafuta
3. tatizo la ajira lipo chini mno, rekodi mpya kipindi cha miaka 50 iliyopita hadi sasa
4. tatizo la ajira lipo chini ya asilimia 4 kwa miezi 21 iliyopita
5. tatizo la ajira lipo chini mno rekodi mpya kwa miaka 65 iliyopita
6.idadi ya wanaoomba bima ya kutokuwa na ajira imeshuka ipo chini tangu uhuru
7. Rekodi mpya ya kushuka kwa tatizo la ajira kwa waafrika wamarekani
8. Rekodi mpya ya kushuka kwa tatizo la ajira kwa walatino
9. Rekodi mpya ya kushuka kwa tatizo la ajira kwa wa asia
10. Rekodi mpya ya kushuka kwa tatizo la ajira kwa maveterani
11. Rekodi mpya ya kushuka kwa tatizo la ajira kwa watu wenye disabilities
12. Rekodi mpya ya kushuka kwa tatizo la ajira kwa watu wenye elimu ya chini
13. kwa mara ya kwanza mishahara kuongezeka kwa haraka katika kipindi cha miaka 100, kila mwaka inakua kwa asilimia 3
14. familia za kati kipato kimeongezeka zaidi ya $63,000
15. wamarekani milioni7 wamejitoa katika tiketi za chakula kutoka kwa serikali kwasababu ya kuwa na kipato kidogo
16. umaskini kwa waafrika weusi kiujumla umekuwa chini mno kuliko vipindi vyote
17, umaskini kwa walatino kiujumla umekuwa chini mno kuliko vipindi vyote
18. DOW, S&P 500, and NASDAQ zimegonga juu kuliko vipindi vingine
Dah huyu mzee ananichosha kutype sasa. ila mzee yupo moto, kuna kipindi alienda graduation ya airforce alishikana mkono na wahitimu zaidi ya elf 1 kuwapa kila la kheri ila hivi vitu fake news hawaoneshi ni media chache tu kama fox news ndio wanaonyesha.
ila licha ta haya yote haya mafanikio yamekuwa msumari wamoto kwa chama pinzani na wameshindwa kuficha chuki zao na kuishia kuonekana watoto