TRC inakemea unyanyasaji wa wafanyakazi katika kambi za SGR

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
251
595
Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kuwa mnamo tarehe 18 Machi 2023 lilitokea tukio la kushambuliwa kwa mfanyakazi wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa - SGR aitwaye Lucy Paulo mwenye fani ya upishi katika kambi ya mradi wa SGR Fela mkoani Mwanza.

Lucy alishambuliwa na raia wa taifa la China aitwaye Bwana Zheng Yuan Feng majira ya saa tatu kasoro asubuhi eneo la jikoni kwa kumtolea lugha chafu na kumpiga, kitendo hiki kilipelekea Lucy kupata majeraha na kupelekwa hospitali ya Bugando na Siku ya Jumatatu tarehe 20 Machi 2023 alipatiwa matibabu a kuruhusiwa siku ya Jumanne ya tarehe 21 Machi 2023 majira ya asubuhi na kwasasa yupo kambini ya Fela chini ya angalizi wa Daktari wa mradi.

Kufuatia tukio hilo Bwana Zheng alikamatwa a kuzuiliwa kwenye kituo cha Polisi Reli na baadaye kuhamishiwa kituo cha Polisi wilaya ya Misungwi, Mamo tarehe 24 Machi 2023 alipandishwa katika mahakama ya Wilayani Misungwi a Kusomea Mashtaka yake kwa kosa la kujeruhi kesi Na 44 ya mwaka 2023.

Kwasasa yupo rumande katika kituo cha Polisi Misungwi baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

TRC imemtaka Mkandarasi kampuni ya CCECC-CRCC kuhakikisha Lucy Paulo anapatiwa stahiki kwa kufuata sheria, taratibu na kuhakikisha anafanya kazi kwa uhuru wakati wote wa mradi, mkandarasi ameridhia kutekeleza matakwa hayo na TRC itaendelea kutatilia.

Shirika linakemea kitendo hicho na vitendo va aina voyote vene lengo la kuleta uonevu na unvanavasaji kwa wafanvakazi na kuwataka wakandarasi kutatilia nvendo zote za wafanvakazi na kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria za chi na matakwa ya kimkataba.

squarephoto.photoeditor.photosquare_2023325121735778.jpg
 
Kumekuwa na kawaida ya Wachina wanaofanya kazi kwenye Reli yetu ya SGR kuwatendea vitendo vya Kinyama Raia wa Tanzania.
Jambo hili halikubaliki hata kidogo,haiwezekani Mtanzania akawa mtumwa kwenye nchi yake.
Leo kumetokea Unyama huo wa Machina wa SGR kumpigia na kumtolea maneno ya matusi Mfanyakazi anayewapikia chakula, jambo hili limetokea Mkoani Mwanza Wilayani Misungwi. Inasemekana Mchina kashakamatwa tunaomba hatua Kali zichukuliwe kwa Mchina huyo.
IMG-20230325-WA0011.jpg
IMG-20230325-WA0006.jpg
 
Kumekuwa na kawaida ya Wachina wanaofanya kazi kwenye Reli yetu ya SGR kuwatendea vitendo vya Kinyama Raia wa Tanzania.
Jambo hili halikubaliki hata kidogo,haiwezekani Mtanzania akawa mtumwa kwenye nchi yake.
Leo kumetokea Unyama huo wa Machina wa SGR kumpigia na kumtolea maneno ya matusi Mfanyakazi anayewapikia chakula, jambo hili limetokea Mkoani Mwanza Wilayani Misungwi. Inasemekana Mchina kashakamatwa tunaomba hatua Kali zichukuliwe kwa Mchina huyo.View attachment 2565425View attachment 2565426
Huyo mchina inabidi awe wa mfano wamezoea sana hao wanajiona wao huu ulimwengu wao ndyo wana haki
 
Inaonekana kapigwa na kitu kizito maana ni kama ametoboka usoni
kama ningekuwepo eneo la tukio huyo mchina wallah ningemfanyia kitendo cha ajabu zaidi ya hicho

hapo utakuta kuna mitaahira inaona mtanzania mwenzao anafanyiwa ufirauni kama huo na yenyewe inachekelea tu kisa posho ya elf 10 inauopewa kwa siki sjui nani katuroga watanzania
 
kama ningekuwepo eneo la tukio huyo mchina wallah ningemfanyia kitendo cha ajabu zaidi ya hicho

hapo utakuta kuna mitaahira inaona mtanzania mwenzao anafanyiwa ufirauni kama huo na yenyewe inachekelea tu kisa posho ya elf 10 inauopewa kwa siki sjui nani katuroga watanzania
Hapo unakuta wachina wako wawili watz 13 😀 kuna mwenzao nadhani kuna clip iliwekwa hapa akimkata mitama mchina 😆
 
Back
Top Bottom