Trafic wageuza JKT Mlalakuwa chanzo binafsi cha mapato kutoka kwa daladala

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,508
8,129
Habari wakuu,

Wakati sakata la rushwa kwa matrafik likiendelea nimewakumbuka Trafic 'wanaotega' kabla kidogo ya daraja la JKT Mlalakuwa (Wana kibanda chao pia pembeni). Ndugu zetu hawa asubuhi huzisimamisha daladala zote zinazoelekea Kawe kupitia Old Bagamoyo na kawaida huchukua 2,000 kwa kila daladala.

Hizi ni daladala za Kawe-Gerezani, Mbagala-Kawe, Kawe-Tandika na nyinginezo. Ni daladala nyingi sana ndani ya saa moja.

Wakipiga mkono, daladala itasimama mbele kidogo na kondakta atashuka kwenda kumalizana nae, trafic hatalisogelea gari wala kulikagua. Zipo tetesi Trafic hawa hucheza 'upatu' wa 70 elfu kwa kila mmoja kutoka kwenye mapato yanayoletwa na makondakta.

Pamoja na utawala uliopita kuruhusu 'Hela ya kubrashia' rushwa ya barabarani haikuwahi kuwa wazi kiasi hiki.
 
Habari wakuu, wakati sakata la rushwa kwa matrafik likiendelea nimewakumbuka Trafic 'wanaotega' kabla kidogo ya daraja la JKT Mlalakuwa (Wana kibanda chao pia pembeni). Ndugu zetu hawa asubuhi huzisimamisha daladala zote zinazoelekea Kawe kupitia Old Bagamoyo na kawaida huchukua 2,000 kwa kila daladala. Hizi ni daladala za Kawe-Gerezani, Mbagala-Kawe, Kawe-Tandika na nyinginezo.

Wakubwa wao nao pia wananufaika na hiyo michezo
 
Kama Mimi konda natoa Buku 2 sisumbuliwi mpaka jioni? Shida yangu nini? Kapata 70,000 Kwa siku? Wala hainiumizi, nenda Kwenye kesi ya Mbowe ujue hela kiasi gani zinachezewa, wacha wale!
 
Kuna siku tulikuwa tunatoka Kariakoo kuchukua vitu vya hardware tunapeleka Bagamoyo. Dereva akashauri ili tupunguze matrafiki tupitie njia ya Kawe.

Bwana weee, alijutaaa kila konaaa wapo anatoa elfu 5,000 mpaka tunafika Boko Ununio ameshatoa elfu 30,000
 
Wewe nae akili huna na ndiyo tatizo kubwa linaloikumba nchi hii.

Traffic wanatii maagizo ya boss wao huyu hapa👇
Sasa kosa la matraffic liko wapi?!WTF!!!

Wameagizwa kuwa wapate kutoka kwenye maeneo yao halafu wewe unaibuka na uzi wa kuwalaumu?Akili za wapi hizi?
 
Tuache tule mkuu, Kwani wewe ungekuwa traffic ungefanyaje?
Na Kimsingi kupata gari haina kosa Tanzania ni kipengele kwahiyo chagua wewe ulimwe faini kubwa au utoe elfu 2 maisha yaendelee
 
Kama Mimi konda natoa Buku 2 sisumbuliwi mpaka jioni? Shida yangu nini? Kapata 70,000 Kwa siku? Wala hainiumizi, nenda Kwenye kesi ya Mbowe ujue hela kiasi gani zinachezewa, wacha wale!
Hizi centers kadri siku zinavyoenda zinaongezeka, wapo wanadai 5,000 siku hizi. Na kama zingekuwa haziwaumizi wasingekuwa wanabadili barabara sehemu wanazoweza kufanya hivyo.
 
Kuna wale wa pale msimbazi center Ilala ni noma kwa kukusanya elfu mbili mbili za daladala
 
Back
Top Bottom