Traffic Police Arusha (Omba Omba) ni Mafisadi?

PauliMasao

JF-Expert Member
Nov 26, 2007
286
39
Mimi nimechoka na hawa traffic police hapa Arusha. Baadala ya kuongoza magari au kuangalia wavunja sheria barabarani wao hujikusanya sehemu mbali mbali ya jiji letu, kazi kubwa ni kuomba pesa. Unasimamishwa halafu wanajifanya kucheki gari wakiona hamna kitu wanakuomba japo buku tano ya lunch. Sasa kwa hesabu za haraka haraka, traffic police mmoja akisimamisha magari ishirini kwa siku, anweza kujipatia shilingi laki moja kwa siku. Je huu sio ufisadi?
 
Wakikuomba buku tano, basi watakua wamekuona wewe sharo.
Buku buku natoaga mara moja moja kwa roho safi.
 
kumbe wanaomba tu..nlidhani wanakubambikia kesi..apo ngoma droo, ukiombwa si lazima utoe!
 
hivi na sisi wenye magari tukaombe wapi?kama ni hayo magari hata wao wanayo tena sio moja au mawili,inakera sana wametugeuza mtambo wao wa kutengeneza hela
 
Aisee kweli wamezidi kuomba juzi kuna mmoja kanisimamisha nikamwambia ndio asubuhi hii nakwenda kutafuta, hakunielewa nikamwambia hapa nilipo nina Buku 2 tu! Akaniambia aisee tugawane hata Bukubuku angalau nikatoe Lock! Nilimuonea huruma sana na ukizingatia baridi iliyopo Arusha sasa hivi.
 
hivi na sisi wenye magari tukaombe wapi?kama ni hayo magari hata wao wanayo tena sio moja au mawili,inakera sana wametugeuza mtambo wao wa kutengeneza hela

Nasikia wengine wana dala dala mbili au tatu
 
Kinachoudhi zaidi ni pale wanapokutamkia ya kuwa gari haiwezi kukosa kosa ikikaguliwa kwa hiyo wewe nipe tu changu mapema ama nikukague ukalipe notification kuna kipindi nilitembelea Arusha nikakumbana na hilo janga ikabidi nimpe elfu tano anasema haitoshi ongeza maana tuko watatu haigawanyiki ikabidi niongeze elfu ili niondokane na adha ya kuvurigiwa ratiba yngu ya siku hiyo
 
Back
Top Bottom