Traffic Kanda Maalumu Dar es Salaam mlichowafanyia bodaboda leo ni uhuni mtupu

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
968
2,029
Mmewakamata asubuhi kwa makosa ya usalama barabarani,

Yes ni sahihi kabisa, lakini kwanini mnafanya oparesheni kwa matukio. Leo mmeendesha oparesheni ya kihuni kwa kisingizio kwamba mwenzao Jana Kagongwa na mwendokasi. Hivyo mmepata maagizo kutoka juu muwashugulikie.

Nyinyi askari mnachangia bodaboda wawe na tabia hizi ambazo wanazo, kwasababu zifuatazo
1. Mnapopanda bodaboda tena kwa msaada huwa hamvai kofia ngumu (helmet).

2. Bado hamjatoa elimu kwa upana kuhusu bodaboda kutambua kwamba na wao wanaendesha vyombo vya moto hivyo SHERIA za usalama barabarani zinawahusu. Media zipo lakini hamtaki kuzitumia vizuri mnababaisha tu kwenye vipindi vya dk 10 au 20.

3. Bado nyinyi hamjaamua kusimamia barabara SHERIA za usalama barabarani kwasasabu mnaendesha jeshi la polisi kana kwamba tupo mwaka 1974 kumbe ni 2023. Hivi niwaulize, dereva akivuka mataa yanayomkataza kufanya hivyo mnampataje ili kum penalize? Kwanini bodaboda wanawapita mkiwa mnaongoza magari na wala hamuhangaiki nao pale wanapo force kupita wakati mmezuia?

Sasa angalia leo hapo kanda maalumu ya trafiki, mmewakamata mnawalazimisha waende Kariakoo Kununua helmet ndiyo muwaachie. SHERIA ipi inaelekeza hivyo? Tatizo la bodaboda nchi nzima ni mfumo wenu ndiyo umelileta, hili janga. Msiwageuze kitega uchumi. Toeni elimu Kisha msimamie sheria.

Na wewe mama afande mtu mzima na maji ya kunde mwenye maneno mengi acha tabia hiyo, kuwa makini na abiria mnaowakamata hapo kwa kudhani wote ni mbumbumbu wa SHERIA. Utanaswa kwenye tundu bovu.
 
Ni ujinga mkubwa sana wa Mamlaka kuwaacha bodaboda kufanya kazi katikati ya mji
 
Yaani mnasamehewa kwa kuambiwa kanunueni helmet,mnalalamika?
Ilitakiwa wawekwe ndani na kisha wapigwe faini.
 
Nakumbuka nilipigana mgumi na traffic wakanipeleka kituoni wakanipa kipigo kitamu hatariii. Niseme ukweli wale afande waliniweka sawa kitabia manake kiburi kilinitoka baada ya kile kipigo.

Nikapangiwa nipelekwe mahakamani kwa kosa la kuhatarisha maisha ya traffic na kosa la kumshambulia traffic akiwa kazini.

Mzee alikuja pale simu 2 tatu mwana nimetolewa nimejaa manundu kama natoka kwa mganga wa kienyeji. Nilikaa home mwezi mzima ndio nikatoka nje, hata uwe na hela hawa jamaa ukiingia kwenye 18 zao utakomaaaa🤣
 
🤣🤣🤣
Ukianza tu kurusha ngumi unakuwa umehalalishi kipigo chochote watakachokupa, hapo watajitetea kuwa walikuwa wanajihami baada ya wewe kumshambulia askari.
 
Mmewakamata asubuhi kwa makosa ya usalama barabarani,

Yes ni sahihi kabisa, lakini kwanini mnafanya oparesheni kwa matukio. Leo mmeendesha oparesheni ya kihuni kwa kisingizio kwamba mwenzao Jana Kagongwa na mwendokasi. Hivyo mmepata maagizo kutoka juu muwashugulikie.

Nyinyi askari mnachangia bodaboda wawe na tabia hizi ambazo wanazo, kwasababu zifuatazo
1. Mnapopanda bodaboda tena kwa msaada huwa hamvai kofia ngumu (helmet).

2. Bado hamjatoa elimu kwa upana kuhusu bodaboda kutambua kwamba na wao wanaendesha vyombo vya moto hivyo SHERIA za usalama barabarani zinawahusu. Media zipo lakini hamtaki kuzitumia vizuri mnababaisha tu kwenye vipindi vya dk 10 au 20.

3. Bado nyinyi hamjaamua kusimamia barabara SHERIA za usalama barabarani kwasasabu mnaendesha jeshi la polisi kana kwamba tupo mwaka 1974 kumbe ni 2023. Hivi niwaulize, dereva akivuka mataa yanayomkataza kufanya hivyo mnampataje ili kum penalize? Kwanini bodaboda wanawapita mkiwa mnaongoza magari na wala hamuhangaiki nao pale wanapo force kupita wakati mmezuia?

Sasa angalia leo hapo kanda maalumu ya trafiki, mmewakamata mnawalazimisha waende kariakoo Kununua helmet ndiyo muwaachie. SHERIA ipi inaelekeza hivyo? Tatizo la bodaboda nchi nzima ni mfumo wenu ndiyo umelileta, hili janga. Msiwageuze kitega uchumi. Toeni elimu Kisha msimamie sheria.

Na wewe mama afande mtu mzima na maji ya kunde mwenye maneno mengi acha tabia hiyo, kuwa makini na abiria mnao wakamata hapo kwa kudhani wote ni mbumbumbu wa SHERIA. Utanaswa kwenye tundu bovu.
Hili ni tatizo la uongozi/utawala. Wanapoapa kuwa watalinda raia na mali zao sijui wangepewa mtihani wanaelewa maana ya maneno hayo ni nini wangesemaji.

Katika hadhari ambazo watalii wa nchi nyingine wanazopewa kuhusu Tanzania ni kuwa madereva hawafuati sheria, ogopa piki piki. Vibaka wa piki piki wapo. Lakini viongozi wetu ati wanakampeni watalii waongezeke.

Tanzania uwanja wa fujo mtupu.Kila kiongozi ana king"ora, wanaosimashwa ni wananchi wao haijalishi humo barabarani wana shida gani!

Askari polisi ni wa kuagizwa tu na kiongozi hao wanaoapa kwamba tangu sasa waendesha piki piki watafuata sheria kama za waendesha magari. Sijui hawa viongozi wetu wakisafiri huko Ulaya hawaoni ustaarabu wa barabarani.

Kule hakuna mtoto wa mfalme kwenye sheria za traffic! Baba wa Taifa aliwahi kuhoji mtuambie mnataka uongozi ili mfanye nini ili tuwapime! Basi nisije ambiwa nimetukana mtu, naachia hapa.
 
Bodaboda wana wenge sana

Na kwa uendeshaji wao watazidi kukatika

Ova
 
Askari walichelewa sana!
Kutoka Agha Kan /Ocean Road kuja Ubungo Plaza , mida ya saa 12 kasoro Jioni kwa bodaboda ndani ya dakika Tisa !!! Ilikuwa ni "dare devil "!! Yaani yule bodaboda alikuwa Jack Chein na nusu!!! Watu wa salama barabarani walikuwa busy kuiongoza magari!!! Hawana taimu...Hata wale voda faster sikuwaona!!!
 
3. Bado nyinyi hamjaamua kusimamia barabara SHERIA za usalama barabarani kwasasabu mnaendesha jeshi la polisi kana kwamba tupo mwaka 1974 kumbe ni 2023. Hivi niwaulize, dereva akivuka mataa yanayomkataza kufanya hivyo mnampataje ili kum penalize? Kwanini bodaboda wanawapita mkiwa mnaongoza magari na wala hamuhangaiki nao pale wanapo force kupita wakati mmezuia?
Wao wenyewe wanakiuka sana sheria za barabarani
 
Back
Top Bottom