TRA yapunguza kodi kuondoa magendo ya Vitenge

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepunguza kodi katika vitenge vinavyoingizwa nchini ili kutoa unafuu kwa wafanyabiashara.

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano kutoka TRA, Richard Kayombo alisema hayo wakati Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alipotembelea mamlaka hiyo katika Maonesho ya Kilimo maarufu #Nanenane yanayoendelea mkoani Mbeya.

Kayombo alisema upunguzwaji huo wa kodi kwenye vitenge utaondoa magendo yaliyokuwa yakifanywa.

“Kwa miaka iliyopita tulikuwa na changamoto upande wa uletaji wa vitenge, zamani wafanyabiashara walikuwa wanatozwa kodi hivyo imeondolewa,” alisema.
 
Na magari wapunguze tu. Watapiga Kodi kwenye mafuta, leseni, na vipuri.
 
Back
Top Bottom