TRA wamenidai kodi kwanza ili nipewe TIN number!

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,926
Wakuu poleni kwa majukumu. Jana nilipata kigugumizi cha mwaka pale ambapo katika harakati za kufungua kampuni yangu niliambiwa siwezi kupata TIN hadi nilipe provisional tax.

Nilimuuliza huyo afisa wa TRA inakuwaje mbona hata leseni ya biashara sijapata? Akniambia eti huo ndio i utaratibu na akanikadiria mahela kibao ambayo sijui nitoe wapi.

Jamani hivi ni kweli unadaiwa kodi kabla hujafungua hata biashara yenyewe au inakuwaje hii? TIN si bure au mimi ndio sielewi kitu hapa?

Tafadhali naombwa nieleweshwe maana wamenifrustrate moja kwa moja.
 
TIN ni bure,jaribu kuongea na ofc nyingine ya tra,labda kwa kufungua mgodi wa uranium ndo wanataka uhakika tin haitakaa bure!Inategemea pia umeongea na nani,kama ni receptionist atakuzingua.Sasa hiyo kodi unalipa ya nini,na kwa kutumia tin ya nani sasa?
 
Imeshanikuta hii mwaka jana tra mwenge nikatoka nduki, mpaka leo napiga inshu zangu na silipi kodi. Tatizo hawana ushirikiano kabisa
 
we fanya online itkuwa simple,hata ivo sina uhakika kama usemayo yanawezekana, ila turudi hapa , ukiseema provisional tax napata picha kuwa TRA wamegundua kuwa tayari ulikuwa unafanya biashara sasa hapa unataka kukwepa kodi kwa biashara uliyoishafanya, otherwise ueleze ukweli kwanza ndo upate jibu sahii. Nlishawahi usema hapa kuwa Jf na akili a watu ni kama google, ukibdili swali na majibu yatabadilika, sasa kama waataka ushauri ebu weka maelezo sahii ili michango yetu iendane na ukweli wa tatizoo lao.
 
Ukweli ni kwamba nimesajili kampuni tayari, sijafanya biashara yoyote , ninahitaji leseni na ili upate leseni lazima uwe na TIN number.
 
AMINI USIAMINI TRA NI MAJAMBAZI WALIOIDHINISHWA KISHERIA - sawa kabisa kama majambazi wa kuingilia watu usiku na pengine madhara ya TRA yakawa makubwa sana kuliko ya hao wa usiku,
Ushauri km ww ni mfanya biashara usiwazoee kabisa chukua tahadhali kubwa hasa kwa mahojiano yao(hawana elimu yeyote) hakika pana mifano mingi sana wamefilisi watu na hasa wajasiliamali wazawa wanaojitokeza kiuchumi.
 
Wakuu poleni kwa majukumu. Jana nilipata kigugumizi cha mwaka pale ambapo katika harakati za kufungua kampuni yangu niliambiwa siwezi kupata TIN hadi nilipe provisional tax.

Nilimuuliza huyo afisa wa TRA inakuwaje mbona hata leseni ya biashara sijapata? Akniambia eti huo ndio i utaratibu na akanikadiria mahela kibao ambayo sijui nitoe wapi.

Jamani hivi ni kweli unadaiwa kodi kabla hujafungua hata biashara yenyewe au inakuwaje hii? TIN si bure au mimi ndio sielewi kitu hapa?

Tafadhali naombwa nieleweshwe maana wamenifrustrate moja kwa moja.

mkuu .... TIN ni halali yako bure kabisa ... ninachujua mimi ni kwamba provisional tax utalipa baada ya kufunguliwa file na kuwa accessed kodi utakayolipa ... then unalipa kiasi fulani ili upate tax clearance certificate
 
Back
Top Bottom