TRA, huu ni uonevu!

Konzogwe

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
434
155
Mimi nimeamua kusema kuwa TRA mnatuonea watanzania wenzenu. Nazungumzia ushuru wa magari.
Unakuta gari linauzwa Japan dola 100FOB, nalinunua na kulisafirisha kwa jumla ya dola 1400CIF.

Cha ajabu TRA wanalipandisha thamani kutoka dola 100 hadi 700. kwa nini? eti kuna udanganyifu wa bei! Udanganyifu gani wakati hata kwwny mtandao bei imeandikwa hivo hivo? na bado risiti inaonyesha bei ni dola 100?

Huu kama sio uonevu ni nini jamani?
 
Siku hizi wanatumia calculator zao zenye bei ya gari likiwa jipya na depreciation rate. Tembelea website yao
 
Mimi nimeamua kusema kuwa TRA mnatuonea watanzania wenzenu. Nazungumzia ushuru wa magari.
Unakuta gari linauzwa Japan dola 100FOB, nalinunua na kulisafirisha kwa jumla ya dola 1400CIF.

Cha ajabu TRA wanalipandisha thamani kutoka dola 100 hadi 700. kwa nini? eti kuna udanganyifu wa bei! Udanganyifu gani wakati hata kwwny mtandao bei imeandikwa hivo hivo? na bado risiti inaonyesha bei ni dola 100?

Huu kama sio uonevu ni nini jamani?

Watu ndiyo wanatakiwa kuliona hilo OCt.2015 fanyeni Maamuzi. Siyo mnalialia.

Biashara huru /Biashara kwa Mujibu wa Soko iko wapi.

100 - 700 huku kote ni kukosa binu ya ukusanyaji Kodi.

Mimi nimeamua kusema kuwa TRA mnatuonea watanzania wenzenu. Nazungumzia ushuru wa magari.
Unakuta gari linauzwa Japan dola 100FOB, nalinunua na kulisafirisha kwa jumla ya dola 1400CIF.

Cha ajabu TRA wanalipandisha thamani kutoka dola 100 hadi 700. kwa nini? eti kuna udanganyifu wa bei! Udanganyifu gani wakati hata kwwny mtandao bei imeandikwa hivo hivo? na bado risiti inaonyesha bei ni dola 100?

Huu kama sio uonevu ni nini jamani?

Mkuu, mie bado sielewi TRA wanafanya makadirio toka vichwani mwao au kwenye documents za gari. Nliagiza gari mwaka 2011 Toyota IST ya 2004 ndio zimeanza kuingia nchini kwa dola 2600 CIF wakaipandisha bei mpaka dola 3500 CIF nikajaribu kila njia kuwaelewesha ila waligoma. Waliishia tu kuniambia hii gari huwezi kununua kwa bei hiyo! Hapo gari iko bandari kavu nao wanaingiza dola 10 kwa kila siku pale gari inapozidisha muda uliopangiwa kama nakumbuka ilikiwa siku 7!
Mkuu nlisarenda na kulipa kodi plus mazagazaga mengine jumla 4.0m wakati kodi ya awali kabla ya kupandishwa bei ilikuwa iwe 2.0m.
System ya TRA pamoja na kuwa kwa sasa wameweka kikokotozi bado haielewiki wana-base kwenye nini.., vichwa vyao, nyaraka za gari au vile wanavyoamka siku hiyo!
 
Hawa TRA hawana huruma na watanzania.....wana roho mbaya sana....kinachofanyika ni uhuni mtupu.....mengine wanatoa vichwani mwao......hawa jamaa wanajiona wao miungu watu.....
 
Back
Top Bottom