Mkuu Nsaji,Mkuu mda nao ulikuwa umetutupa mkono na ukumbuke ishara ya serikali kutekeleza maagizo ya bunge ilikuwa imetoweka.Badala ya kutekeleza maagizo ,serikali ikapeleka maigizo ya kesi ya Gire.Sisi wengine kwa kuangalia athari ambazo zingelikumba taifa kwa kuingia gizani tukaona ni afadhali tuinunue hiyo Mitambo ya Dowans ambayo tunayo hapahapa.Lakini wenzetu mkakataa na sisi tukakubali ya wengi wape,rejea thread hiyo ya Dowans na ile aliyoanzisha Mwanakijiji kwa kichwa cha habari''Mwachieni Gire Nunueni Mitambo ya Dowans Yaishe'' .
Mimi ninachokipinga tabia ya watu kukosa uvumilivu ya mawazo yanayotofautiana na ya kwao na kuanza kushutumiana kuwa fulani kanunuliwa.
Nakubaliana na ulichoandika hapo juu; hilo ndilo tatizo la sisi Watanzania. Tunaangalia kila jambo kwa kutumia black and white scenario au angelikuwa Bush anasema you are either with us or with the terrorists. Ni yale yale ya pande mbili za shilingi huku ukiwa una macho yanayofanya kazi au mikono inayoweza kupapasa unaona/unagundua wazi shilingi ina pande zaidi ya mbili.
Mimi nimeshangaa hatred iliyopo kwa mhesh. Zitto kwasababu tu alitetea kununuliwa kwa mitambo ya Dowans. Watu wamesahahu mazuri yote ya Zitto na sasa wanaanza kumtukana eti kanunuliwa.
Kama nilivyoandika kwenye hiyo thread; hata mimi ningeona hiyo mitambo inunuliwe kama mambo yote mengine kuhusu uhalali wa hiyo mitambo yangewekwa wazi na pia bei yake ingelikuwa nafuu. Watu wengi walikataa; tunaojua demokrasia tunasema wengi wape. Matokeo yake miezi sasa inakatika na hakuna kinachoendelea na tunachoona ni hayo hayo matatizo ya kukata umeme.
Mhesh. Zitto amefanya mengi makubwa kuendeleza upinzani labda kuliko kiongozi mwingine yeyote ukiondoa Dr. Slaa. Badala ya kumbeza inabidi kumpa respect yake. Of course sio wakati wote atakubaliana na sisi lakini hiyo sio sababu ya kuanza kumbeza.
Badala ya kuhangaika hapa kutafuta kiongozi gani kanunuliwa, labda tuwe tayari kuvichangia hivi vyama ili viongozi wake wasiwe ombaomba. Lakini kama tunakaa nyuma na kazi zetu ni kulaumu, kweli hao viongozi wakizidiwa kuna baadhi yao watachukua fedha kwa mafisadi.