Olumolongez
JF-Expert Member
- Dec 19, 2015
- 818
- 298
Sifahamu ni kifungu gani cha sheria lkn km umeuziwa kiwanja kilichopimwa unapaswa kulipa 10% ya bei ya kiwanja hicho na unalipia TRA na unapewa hati inayoitwa tax clearance certificate ndiyo uweze kuendelea na taratibu nyingine. Sifahamu utaratibu wa hao wanaouziana viwanja kienyeji kwa maeneo ambayo hayajapimwa.Hotuba ya Rais kwa wazee wa dsm imenikumbusha JIPU moja alipo sema watanzania wanauliza na kujadili kuwa katika siku 100 za kuingia madarakani Rais amefanya nini na kwamba wao hawajiulizi wameifanyia nini Tanzania.
Pia, amewataka watanzania kulipa kodi, kudai risiti kila wanapo nunua kitu.
Baada ya kuunganisha kuhimizwa kulipa kodi, kudai risiti, nimewaza kuwa hata unapo pata huduma serikalini na ukatakiwa kutoa fedha yakupasa kudai risiti.
Katika tafakuli hilo, nimejiuliza ni watanzania wangapi wamenunua mashamba au nyumba na hawakutekeleza au hawatekelezi kulipa kihalali 10% kodi ya serikali?
Ni hivi, kuna kautaratibu fulani kwamba unapo nunua shamba, nyumba na ukataka uthibitisho wa serikali ya kijiji, mtaa ama mahakama una ambiwa kutoa asilimia kumi ya thamani ya mauziano/manunuzi na kwamba matumizi ya fedha hiyo eti ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya eneo / chombo husika!
Kwanza
Naomba mwenye ujuzi wa hili anifahamishe kama ni kweli ndiyo matakwa ya sheria na sheria ipo. Ukiambatanisha kifungu husika itasaidia sana.
Pili
Naona kiasi hiki ni kikubwa sana na kinaweka mwanya wa kutoa rushwa badala ya utekelezaji wa takwa lenyewe.
Tatu
Kwa nini kiasi hiki kisipunguzwe ili a) kilipike b) mnunuzi ama muuzaji asishawishike kutoa rushwa kukwepa kutoa kiasi kikubwa cha fedha c) kuepuka kunemeesha viongozi wa ngazi husika d) serikali ipate haki yake kitu ambacho hata mtoaji atanufaika na mchango wake kwa Taifa?
Hili ni ombi maalum, serikali itafakari vizuri ipunguze kiasi hiki I we asilimia 1 tu. Nina amini ikiwa 1% ni kiasi ambacho kinalipika na serikali itanufaika nacho kuliko hali ilivyo sasa. Niombe pia serikali isione kwamba kupunguza kiasi hiki kutoka 10% hadi 1% itapunjika badala yake itanufaika na ni kiasi kitakacho msukuma mtanzania kulipa hususani anapo ona kodi yake inatumika vizuri na inamnufaisha!
Hili nalo jipu.