Tofauti kati ya sentensi ambatano na sentensi changamano

oxlade

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
601
94
naomba msaada wenu wajuzi wa lugha juu ya utafauti wa aina hizo mbili za sentensi. shukran
 
[h=1]Uchanganuzi wa Sentensi[/h]
• Sarufi • Sentensi • Uchanganuzi wa Sentensi
Kuchanganua sentensi ni kugawa sentensi kulingana na makundi ya maneno na aina ya maneno.
Kuna njia tatu za kuchanganua sentensi:
  1. matawi
  2. jedwali
  3. mishale

Angalia:

  1. Uainishaji wa Sentensi za Neno Moja
  2. Uchanganuzi wa Sentensi Sahili
  3. Uchanganuzi wa Sentensi Ambatano
  4. Uchanganuzi wa Sentensi Changamano

[h=2]Mifano[/h][h=3]Kuchanganua Sentensi Sahili[/h]
  1. Nimefika.
    1. Matawi
      nimefika.png
    2. Jedwali
      S
      KT
      T
      Nimefika
    3. Mishale
      S → KT
      KT → T
      T → Nimefika​

  2. Jiwe Limeanguka.
    1. Matawi
      jiwe.png
    2. Jedwali
      S
      KNKT
      NT
      Jiwelimeanguka
    3. Mishale
      S → KN + KT
      KN → N
      N → Jiwe
      KT → T
      T → limeanguka​

  3. Mvua nyingi ilinyesha jana usiku.
    1. Matawi
      mvua.png
    2. Jedwali
      S
      KNKT
      NVTKE
      TEE
      Mvuanyingiilinyeshajanausiku
    3. Mishale
      S → KN + KT
      KN → N + V
      N → Mvua
      V → nyingi
      KT → T + KE
      T → ilinyesha
      KE → E1 + E2
      E1 → jana
      E2 → usiku​

[h=3]Kuchanganua Sentensi Ambatano[/h]
  1. Barua ilitumwa lakini haikumfikia Shakila.
    1. Matawi
      barua.png
    2. Jedwali
      S
      S1US2
      KN1KT1UKT2KN2
      N1T1UT2N2
      BaruailitumwalakinihaikumfikiaShakila
    3. Mishale
      S → S1 + U + S2
      S1 → KN1 + KT1
      KN1 → N1
      N1 → Barua
      KT1 → T1
      T1 → ilitumwa
      U → lakini
      S2 → KT2 + KN2
      KT2 → T2
      T2 → haikumfikia
      KN2 → N2
      N2 → Shakila

  2. Mwalimu alikunja shati lake na kuwachapa wanafunzi kwa kiboko.
    1. Matawi-
      mwalimu.png
    2. Jedwali
      S
      S1US2
      KNKTUKTKN
      NTKNUTKNKE
      NTNVUTNUN
      mwalimualikunjashatilakenakuwachapawanafunzikwakiboko
    3. Mishale
      S → S1 + U + S2
      S1 → KN1 + KT1
      KN1 → N
      N → mwalimu
      KT1 → T + KN2
      T → alikunja
      KN2 → N + V
      N → shati
      V → lake
      U → na
      S2 → KT2 + KN3 + KE
      KT2 → T
      T → kuwachapa
      KN3 → N
      N → wanafunzi
      KE → U + N
      U → kwa
      N → kiboko

[h=3]Kuchanganua Sentensi Changamano[/h]
  1. Wote waliokufa watafufuka
    1. Matawi
      waliokufa.png
    2. Jedwali
      S
      KNKT
      WsT
      Wotewaliokufawatafufuka
    3. Mishale
      S → KN + KT
      KN → N + s
      W → wote
      s → waliokufa
      KT → T
      T → watafufuka

  2. Wanafunzi ambao hawatasoma vizuri wataanguka mtihani
    1. Matawi
      wanafunzi.png
    2. Jedwali
      S
      KNKT
      NsTN
      NVKTTN
      NVTETN
      Wanafunziambaohawatasomavizuriwataangukamtihani
    3. Mishale
      S → KN + KT
      KN → N + s
      N → wanafunzi
      s → V + T + E
      V → ambao
      E → hawatasoma
      KT → T + N
      T → wataanguka
      E → mtihani


:noidea:
 
2. Sentensi Ambatano.
Sentensi ambatano ni sentensi zenye zaidi ya kishazi huru kimoja na huwakilisha mawazo mawili au zaidi. Aghalabu sentensi hizi hutumia viunganishi(U) au alama za uakifishaji kama vile kituo(,) na nukta-nusu (;) ili kubainisha wazo moja toka nyingine.

Kwa mfano:

  • Chesi alisoma kwa bidii. Chesi alianguka mtihani.


= Ingawa alisoma kwa bidii, Chesi alianguka mtihani.​


  • Dadangu amerudi nyumbani. Dadangu amelala.

= Dadangu amefika nyumbani na kulala.



Mifano mingine:

  • Tulifika, tukaona, tukapiga na tukatawala.
  • Leo inaonekana Karimi amejipamba akapambika.
[FONT=arial, sans-serif]Soma zaidi kuhusu muundo, uchanganuzi na mifano ya sentensi ambatano hapa.


3. Sentensi Changamano
[/FONT]

Hizi ni sentensi zinazoundwa kwa kuunganisha huru pamoja na kishazi tegemezi kwa kutumia o-rejeshi ili kuleta zaidi ya wazo moja.
Mfano:
Juma amenilitelea kitabu. Nilikuwa nimetafuta kitabu hicho kwa muda mrefu.
Juma ameniletea kitabu ambacho nilikuwa nimekitafuta kwa muda mrefu
Yeye ni mwizi. Alipigwa jana jioni.
Yeye ndiye mwizi aliyepigwa jana jioni


[FONT=arial, sans-serif]Soma zaidi kuhusu muundo, uchanganuzi na mifano ya sentensi changamano hapa.[/FONT]
 
tofauti kubwa inaonekana kua kiunganishi cha sentensi/mawazo mawili.
Sentensi ambatano zinatumia alama za uafikishaji (, ; )
Sentensi changamano zinatumia kishazi tegemezi (ndie, ambae, kilicho Nk)
I hope this helped...
 
tofauti kubwa inaonekana kua kiunganishi cha sentensi/mawazo mawili.
Sentensi ambatano zinatumia alama za uafikishaji (, ; )
Sentensi changamano zinatumia kishazi tegemezi (ndie, ambae, kilicho Nk)
I hope this helped...

shukrani mdau wa lugha.
 
tofauti kubwa inaonekana kua kiunganishi cha sentensi/mawazo mawili.
Sentensi ambatano zinatumia alama za uafikishaji (, ; )
Sentensi changamano zinatumia kishazi tegemezi (ndie, ambae, kilicho Nk)
I hope this helped...

Mwali uko safi kwenye Kiswahili enh,.Ila Mwali hiyo elevator yako ni kiboko,hayo macho kama yanaita vile,vijana wataruka kweli?mimi ni mzee:..Itabidi nianze kusoma kiswahili,umenikumbusha miaka mingi iliyopita wakati nasoma kiswahili...
 
Tofauti:
sentensi changamano - ni tungo inayoundwa na kishazi tegemezi kimoja au zaidi; mfano-Mtoto aliyekuja hapa jana alikuwa rafiki yangu, Ukuta uliobomoka ulijengawa juzi.
Ilhali,
sentensi ambatano- ni tungo inayoundwa na sentnsi mbili au zaidi kwa kiungania. inaweza kuwa sentensi huru+huru,ambatano+ambatano,huru+ambatano,changamano+huru,changamano+changamano) n.k
mfano- juma analima na anna anacheza(huru+huru),mwalimu anafundisha wakai akiandika huku wanafunzi wanaandika na kumsikiliza(ambatano+ambatano), mimi ninacheza mpira ilhali wazazi wangu wanalima mara wanavuna(huru+ambatano), aliyekuja leo ameondoka lakini mimi sikumwona(changamano+huru), mti uliokatwa una kuni nyingi na walioukata walibeba kuni nyingi(changamano+changamano)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom