Toa maoni yako shost - kwa wanawake zaidi

Da Asia

JF-Expert Member
Sep 25, 2011
731
819
Nimeikuta mahali hii nikaona tushee japo mimi hainiingii akilini sana kuna K inajisafisha yenyewe.

Habari zenu kina dada, mama na wadogo zetu.

Tungependa ku-share nanyi kuhusiana na jambo moja. Tafadhali tumia hii kama changamoto kutaka kutafuta habari zaidi, kama sio kwaajili ya kuhakiki tuliyoandika humu basi pia kwaajili ya kupata habari zaidi, uelewe zaidi ili uweze kufanya maamuzi mazuri na sahihi kwa afya yako.

Sisi ni kina dada wasomi tu, unaweza hata kutuita “when I was”. Basi si unafikiri you know what you know and what you know is what it is!! Mmh! Tuvunje ukimya, tuliongelee hili na tuelimike.

Mmoja wetu hizi habari alikua nazo lakini haikuwahi kumclick kwamba wenzake labda hawana au hawana habari kamili au wana habari potofu. Ongea na watu kadhaa ikaonekana kuna misinformation ya hali ya juu kuhusiana na swala zima la....Kwa Bibi

Mtuwie radhi kwani tunaelewa kwamba kuna makabila ambayo huwafundisha mabinti zao tangu wakingali wadogo juu ya hili. Na japokuwa kulikua bado kuna asilimia kubwa ya wasichana ambao hawakuyajua haya na labda hata wasingeyawaza, sasa hivi kumetokea mfumuko wa kitu kinaitwa kibao kata!!! Funda nikufunde!! Hata kitchen party nazo. Huko ndugu zetu ndio tunatumia kama jukwaa la kuelezana na kudanganyana hukusu...

Usafi wa uke!...wa ndani

Imani au uelewa uliokuwepo:
•Uke ni sehemu chafu chafu chafu sana tena yenye wadudu wa kutosha yenye kunahitaji kusafishwa kila siku
•Uke unahitaji kusafishwa kwa hali ya juu zaidi mara baada ya siku za hedhi au tendo la ngono
•Uke wapaswa kuwa mkavu wakati wote ute unakuwepo ukeni ni uchafu usiopaswa kuwa pale
•Uke haupaswi kuwa na harufu hata kidogo. Harufu ni ishara ya uchafu au ugonjwa!

Kinachofanyika kutokana na imani hii ni kwamba uke husafishwa kila siku nje na ndani. Hasa ndani kwa kutumia vidole na:
•Maji ya kawaida, labda vuguvugu
•Maji ya iliki
•Maji ya mchele
•Asali
•Rose water
•Vidonge vya kufyonza uchafu
•Maji yenye dettol
•Maji ya vinegar...

Ukweli ni kwamba:
•Uke ni mfumo unaojisafisha wenyewe kwa ndani na ni sehemu moja ya mwili wako ambayo ni safi kuliko maelezo, safi kuliko midomo yetu. Habari ndio hiyo.
•Mfumo huu husafisha damu ya hedhi na shahawa wenyewe, hauhijaji msaada wa aina yeyote
•Uke wenye afya una bacteria, lactobacilli, ambao ni kawaida kuwepo humo. Hawa hupambana na vijidudu visivyopaswa kuwepo huko kulinda uke na mfumo wa uzazi kwa ujumla.
•Uke wenye afya sio mkavu, muda wote una ute usiokua na rangi (kama maji), mwepesi na unaonata. Uzito, wingi na mnato wa ute huu hutegemea na mabadiliko ya mwili wa mwanamke. (Jifunze tofauti ili ujue muda inapaswa kumuona daktari)
•Uke wenye afya una harufu, ambayo ni nzuri, murua na isiyokera J. Kama harufu itakua kali na inayokera (kama yai bovu) basi uke wako hauko katika afya njema na unahitaji kumuona daktari.

Madhara ya kusafisha uke kama ilivyoainishwa hapo juu:

Ni kitu kimoja tu kinachopaswa kuingia kwa kibibi……ambacho ni babu toshaaaaaaaa, vidole na vingine vyote vilivyoinishwa hapo juu it’s a no no situation na….

Unaporuhusu kitu chochote kisichotakiwa kuingia ndani ya uke wako, unatoa nafasi ya kuharibu mfumo wake wa asili, na unajua ukishadisturb mfumo wowote, athari zake ni chain reaction.
•Vidole vyako vinaweza kuwa na vijidudu (kumbuka uke ni msafi kuliko vidole vyako) vijidudu hivyo vikashamiri na kuwashinda nguvu Lactobacilli. Ukapata vaginal infections za kila namna.
•Kitendo hiki chaweza kupeleka vijidudu kwenye njia ya mkojo ukasababisha UTI – Urinary Tract Infection
•Unawaua/kuwaondoa Lactobacilli na kuacha uke wako wazi na hatarini kwa mashambuizi ya kila aina. Hakuna walinzi!!
•Mfumo wa uke usipofanya kazi vizuri ndio utaona ute mwingi kuliko inavyotarajiwa au mkavuuuu kabisa.
•Uchafu wowote mwingine unashindwa kusafishwa naturally unalundikana matokeo yake ofcousre infections na harufu mbaya.
•Amini usiamini ni sababu mojawapo inayoleteleza saratani ya shingo ya uzazi.
•Mashambulizi mengine yanasaabisha utasa (infertility)
•Ute unakauka, na pale unapouhitaji (tenda la ndoa) hautakuwepo na kusababisha michubuko ambayo inaongeza fursa za maambukizi ya magonjwa ya ngono.

He? Sasa tusafishe vipi uke kuhakikisha una afya njema?
•Safisha nje tu kila siku unapooga au unapojisikia kwa maji safi na mikono misafi. Nje ya uke kunahusisha mashavu na katikati yake.
•Waweza kutumia sabuni isiyokua na kemikali kali, japo haishauriwi pia but Hakikisha sabuni haipenyi ndani kabisa

Yap that’s it, no more!! Wewe safisha nje, ndani kutajisort kwenyewe.

Kwa ujumla tutahakikisha vipi afya njema ya uke? Ukiacha kusafisha? – Hii ni topic nyingine kubwa na ndefu na yenye mijadala kibao. Wataalamu naona wanaintervene.


Sisi ni zaidi ya Takwimu – UNFPA 7 Billion Actions Campaign

M & M

Tafadhali tuma ujumbe huu kwa wanawake wote unaowapenda, na kama kuna jinsi ya kusafisha uke unayoitumia haijatajwa, iongeze mwisho ya barua pepe hii kuzidi kuelimishana. Kila unapotuma tafadhali jumuisha anwani
pepe hii:

Hey, waambieni na kina kaka pia, ukiacha ishu za usafi binafsi, asilimi kubwa yetu tunafanya kwaajili yao.

Tunawapenda sana.

 
Undhani aliyetengeneza uke hakujua unatakiwa kuwa msafi?

Ndio ni kweli unajisafisha kiasi ambacho si cha kuleta magonjwa.

Sasa hivi matumizi ya viungo yamebadilika, unakuta mdomo wa mtu uko ukeni na pua zake ziko huko lazima basi hata usafishaji wa asili usaidiwe na artificial usafi. Tusipobadili matumizi ya viungo, k inajisafisha yenyewe.

Afu usafi ni reletive, kuna baadhi ya watu wanalilia kulala kwenye shamba la mbolea.
 

Unaporuhusu kitu chochote kisichotakiwa kuingia ndani ya uke wako, unatoa nafasi ya kuharibu mfumo wake wa asili, na unajua ukishadisturb mfumo wowote, athari zake ni chain reaction.
•Vidole vyako vinaweza kuwa na vijidudu (kumbuka uke ni msafi kuliko vidole vyako) vijidudu hivyo vikashamiri na kuwashinda nguvu Lactobacilli. Ukapata vaginal infections za kila namna.
•Kitendo hiki chaweza kupeleka vijidudu kwenye njia ya mkojo ukasababisha UTI – Urinary Tract Infection
•Unawaua/kuwaondoa Lactobacilli na kuacha uke wako wazi na hatarini kwa mashambuizi ya kila aina. Hakuna walinzi!!
•Mfumo wa uke usipofanya kazi vizuri ndio utaona ute mwingi kuliko inavyotarajiwa au mkavuuuu kabisa.

:biggrin1: naonea huruma wale waliozoea kutumia vidole/vibrators kila siku...sijui itakuaje... jamani hii topic na ilivyoelezea mambo ya bakteria na uchafu na ute...eeeh...nahisi uvinza kuingia mwisho leo....ameshaniharibia apetite yote. thanks alot mtoa mada!! :A S embarassed::shock:
 
Haya mambo ya kisayansi nayo bana.....sometimes yanachanganya, kwani wangapi waliosafisha huko wakaongeza kasi ya kuwa infected??
 
huo mfumo unaosemwa ni vaginal secretion ambazo ni anti-bacterial lakini haimaanishi kusioshwe.....panatakiwa pasafishwa say kila ukioga na hapo hupelekea ku-trigger fresh secretion nyingine....jamani pakiwa na utomvu watu wataweza kwenda uvinza kweli.....kwahiyo hata kamasi nalo ni secretion za kulinda bacteria, tusilitoe....
 
Useful information da asia....thaaank yu mamii,ntafanyia kazi..
 
Unaporuhusu kitu chochote kisichotakiwa kuingia ndani ya uke wako, unatoa nafasi ya kuharibu mfumo wake wa asili, na unajua ukishadisturb mfumo wowote, athari zake ni chain reaction.

Kumbe kinachotakiwa kuingia ni nini?
 
Haya jamani tusafishieni vizuri hizo K, ila siku hizi kuna menu na Bufee, hapa umetoa darasa jinsi ya kusafisha menu, ila ile 0713 inaitwa Bufee yaani unajisevia mwenyewe, nayo haina darasa lake jinsi ya kuisafisha vyema?
Nilikuwepo.
 
ndio inajisafisha yenyewe.



Kwa hiyo mchezo wa kuchokonoa uishe....
Mchezo wa kuingiza vidonge,eti vya kunyonya uchafu ukome....
Mchezo wa kuingiza pamba yenye asali uishe mtajitafutia cancwr buureee............
 
Usisafishe kama anavyo shauri huyo mtaalam halafu uone kunavyotoa huko. Nyie mnataka kuwachanisha watu na waume zao. Mie kama sijasikia udi ukitokea huko si dive.
 
kweli kabisa inajisafisha yenyewe...
mimi kwangu hakiingii kitu chochote...
 
kweli kabisa inajisafisha yenyewe...
mimi kwangu hakiingii kitu chochote...

sasa kama akiingii kitu chochote unakosea, utapata magonjwa wewe,unajua hilo tund limewekwa hili vitu viingie mfano mpododo!
 
asante kutupa hili darasa la ukubwani. nitalifanyia kazi kuanzia leo.
 
Back
Top Bottom