TISS, shirika bora la kijasusi Africa.

Junior Clinton Mr.

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,075
1,423
Kwa Afrika, Ujasusi wa "Kidola", Tanzania ndio mwamuzi wa siasa za Afrika. Hil linatazamwa tangu vuguvugu la uhuru wa Afrika mpaka kunako Karne ya 21. Kwa lugha laini ni kuwa TISS ndio idara yenye nguvu Afrika katika medani ya Ujasusi wa Kidola.

Kwa mujibu wa Takwamu za mwaka 2014, zilizotolewa na mtandao wa onlinenewspoint.com, Orodha ya Mashirika Kumi Bora ya Ujasusi Duniani ni kama ifuatavyo:

-Inter Service Intelligence (ISI) la Pakistan;

-Central Intelligence Agency (CIA) la Marekani;

-Secret Intelligence Services (MI6) la Uingereza;

-Ministry of State Security (MSS) la China;

-Federal Security Services (FSB) la Urusi;

-The Institute For Intelligence and Special Operation (MOSAD) la Israel;

-Direction Generale De La Securite Exterieure (DGSE) la Ufaransa;

-Canadian Security Intelligence Service (CSIS) la Canada;

-Research and Analysis Wing (RAW) la India;

-Australian Secret Intelligence Service (ASIS) la Australia.

Katika Afrika, hakuna takwimu muafaka zinazoainisha lipi shirika bora la ujasusi lakini mtandao wa africaintelligence.com unaojihusisha na habari za kijasusi, mwaka 2015, ulizua mjadala wa kijasusi ambapo jasusi mstaafu, Lizo Gibson Njenje wa The National Intelligence Agency (NIA) ya Afrika Kusini alisema SASS (South African Secret Service) ndiyo shirika bora akitumia kigezo cha ukubwa wa bajeti yao kwa mwaka.

Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa vikali na wadau kutoka nchi za Morocco, Ghana na Misri. Kwa pamoja wakakubaliana kutumia vigezo viwili vikuu: misheni ilizoshiriki idara husika; na majaribio ya mapinduzi kwa viongozi wa ndani hasa yale yaliyoshindwa kufanikiwa baada ya zuio la nguvu za shirika/idara husika. Idara ya ujasusi (TISS) ya Tanzania ilitajwa kuwa ya kwanza, ikifuatiwa na CIO (Central Intelligence Organisation) la Zimbabwe, DST (Direction de la Surveillance du Territoire) la Morocco, GID (General Intelligence Directorate) la Misri na SASS la Afrika Kusini.

Pia, kwa upande wa Jeshi bora na lenye nguvu Barani Africa, mwandishi wa habari za kijasusi, Micky Wren, katika andiko lake la kitafiti la mwaka 2015 aliloliita 35 Most Badass Fighting Units From Arround the world ameorodhesha kikosi hatari Afrika kiitwacho Koboko (black mamba) kilicho chini ya Jeshi la Tanzania, JWTZ, katika orodha hiyo kikosi hicho kipo nambari 27 ya vikosi kazi bora kabisa duniani, huku nambari moja ikishikwa na US Navy SEAL ya Marekani.

Takwimu hizi zinaitambua JWTZ kuwa ndio kikosi bora namba moja Afrika. Pamoja na changamoto za ndani hasa ujio wa mfumo wa vyama vingi, ambapo siasa za vyama kupewa kipaumbele cha taifa, na kuporomoka kwa Maadili ya Taifa na hasa mvurugano wa elimu ya Tanzania, bado TISS ni chombo madhubuti na ina watu makini sana. Zaidi, TISS imekuwa mkufunzi imara wa taasisi na idara nyingi za ujasusi barani Afrika.......

Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.......

Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ni 80,000/= tu.

Piga simu 0715865544 au 0755865544 popote ulipo utaletewa...

Source: Yeriko Nyerere
 
Kweli TISS ilikuwa ni bora sana ila kwa sasa imeshuka sana kutokana na kutokuwa na uadilifu baadhi ya nguvu kazi zao(rasilimali watu)na kuingiliwa na wanasiasa ndio kumeharibu sura ya TISS.
Huko TPDF kwa upande wa physical training tupo vizuri ila rasimali vifaa vya kisasa ndio tatizo na rasimali vifaa inahitaji budget iliyojitosheleza na hiyo budget inahitaji uchumi imara
 
Yaani TISS ya zimbabwe ndio ya pili afrika??? Basi huo utafiti nimeupuuza tayari!! Nchi imevurugwa ile na wazungu baada ya kuwekewa vikwazo hata pesa ikashuka thamani hao TISS ya zimbabwe walishindwa kushauri ili kuepuka hiyo dhahama mpaka leo hii wananchi wanateseka kiasi kile

Hii ranking ya ajabu sana.....
 
Nadhani kigezo kikuu ni kudhibiti wapinzani na wakosoaji wa serikali na kubeba watawala ila kinyume cha hapo hakuna kitu Tanzania wala Zimbabwe
 
Tiss hii ya kung'oa watu kucha na meno bila ganzi ndio iwe #1 kwa Africa? Tuacheni utani bhana. Jeshi bora ni letu lilifanya misheni kule komoro na huko mashariki ya kongo kwa waasi wa maimai?!

% kubwa ya wanajeshi wetu wana vitambi utafikiri ni moja ya sifa ya kuwa mjeda
 
Yaani TISS ya zimbabwe ndio ya pili afrika??? Basi huo utafiti nimeupuuza tayari!! Nchi imevurugwa ile na wazungu baada ya kuwekewa vikwazo hata pesa ikashuka thamani hao TISS ya zimbabwe walishindwa kushauri ili kuepuka hiyo dhahama mpaka leo hii wananchi wanateseka kiasi kile

Hii ranking ya ajabu sana.....
Aha nilipoona Zimbabwe tu nikajua hizi Ni shuduu zimeandaliwa ccm
 
Kwa Afrika, Ujasusi wa "Kidola", Tanzania ndio mwamuzi wa siasa za Afrika. Hil linatazamwa tangu vuguvugu la uhuru wa Afrika mpaka kunako Karne ya 21. Kwa lugha laini ni kuwa TISS ndio idara yenye nguvu Afrika katika medani ya Ujasusi wa Kidola.

Kwa mujibu wa Takwamu za mwaka 2014, zilizotolewa na mtandao wa onlinenewspoint.com, Orodha ya Mashirika Kumi Bora ya Ujasusi Duniani ni kama ifuatavyo:

-Inter Service Intelligence (ISI) la Pakistan;

-Central Intelligence Agency (CIA) la Marekani;

-Secret Intelligence Services (MI6) la Uingereza;

-Ministry of State Security (MSS) la China;

-Federal Security Services (FSB) la Urusi;

-The Institute For Intelligence and Special Operation (MOSAD) la Israel;

-Direction Generale De La Securite Exterieure (DGSE) la Ufaransa;

-Canadian Security Intelligence Service (CSIS) la Canada;

-Research and Analysis Wing (RAW) la India;

-Australian Secret Intelligence Service (ASIS) la Australia.

Katika Afrika, hakuna takwimu muafaka zinazoainisha lipi shirika bora la ujasusi lakini mtandao wa africaintelligence.com unaojihusisha na habari za kijasusi, mwaka 2015, ulizua mjadala wa kijasusi ambapo jasusi mstaafu, Lizo Gibson Njenje wa The National Intelligence Agency (NIA) ya Afrika Kusini alisema SASS (South African Secret Service) ndiyo shirika bora akitumia kigezo cha ukubwa wa bajeti yao kwa mwaka.

Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa vikali na wadau kutoka nchi za Morocco, Ghana na Misri. Kwa pamoja wakakubaliana kutumia vigezo viwili vikuu: misheni ilizoshiriki idara husika; na majaribio ya mapinduzi kwa viongozi wa ndani hasa yale yaliyoshindwa kufanikiwa baada ya zuio la nguvu za shirika/idara husika. Idara ya ujasusi (TISS) ya Tanzania ilitajwa kuwa ya kwanza, ikifuatiwa na CIO (Central Intelligence Organisation) la Zimbabwe, DST (Direction de la Surveillance du Territoire) la Morocco, GID (General Intelligence Directorate) la Misri na SASS la Afrika Kusini.

Pia, kwa upande wa Jeshi bora na lenye nguvu Barani Africa, mwandishi wa habari za kijasusi, Micky Wren, katika andiko lake la kitafiti la mwaka 2015 aliloliita 35 Most Badass Fighting Units From Arround the world ameorodhesha kikosi hatari Afrika kiitwacho Koboko (black mamba) kilicho chini ya Jeshi la Tanzania, JWTZ, katika orodha hiyo kikosi hicho kipo nambari 27 ya vikosi kazi bora kabisa duniani, huku nambari moja ikishikwa na US Navy SEAL ya Marekani.

Takwimu hizi zinaitambua JWTZ kuwa ndio kikosi bora namba moja Afrika. Pamoja na changamoto za ndani hasa ujio wa mfumo wa vyama vingi, ambapo siasa za vyama kupewa kipaumbele cha taifa, na kuporomoka kwa Maadili ya Taifa na hasa mvurugano wa elimu ya Tanzania, bado TISS ni chombo madhubuti na ina watu makini sana. Zaidi, TISS imekuwa mkufunzi imara wa taasisi na idara nyingi za ujasusi barani Afrika.......

Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.......

Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ni 80,000/= tu.

Piga simu 0715865544 au 0755865544 popote ulipo utaletewa...

Source: Yeriko Nyerere
Kwq vigezo hivyo ni sawa lkn ni historian kabla ya vyama vingi, uchumi wa kidola Tanzania tuko nyuma, sasa tutumie vigezo vya TISS katika mission za kiuchumi na maendeleo imehusika vipi kama Tanzania itaonekana,

Yerick ametumia nukuu ili kitabu kiwe na credibility pamoja na nafsi ya mwandishi juu ya machapisho mengine.

Tiss imebaki kuwa mbovu baada ya sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1996
Pia yerick aliweka bandiko na kuipinga sasa kwenye kitabu kaandika? Inanipa mashaka ya weledi wa huyu MTU.
 
System imevurugwa kwenye Awamu pili za Mzee wa msoga ni kweli amefanya mengi ila Idara hata tusiokuwa tunaifahamu kwa sasa tuna abc zake Huu ni udhaifu tayari hii ina maana we don't have loyal servants who serving for us, Kama Raia wa kawaida tu anaweza kujua kinachoendelea Idarani basi ni hatari sana kwa wanaofanya espinoge kutokea nearby countries, Nategemea Pia reform ila isiathiri utendaji wala holes zaidi, Tunaimani na JPM
 
Back
Top Bottom