TIMU YETU YA MAJIMAJI, NI FAHARI YETU WANA WA RUVUMA

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
954
510
Pamoja na changamoto za kifedha zinazowakabili lakini bado mnaendelea kupambana kiume kuhakikisha kuwa mnaendelea kubaki katika ligi kuu Tanzania bara. Tunawashukuru kwa roho yenu na moyo wenu wa kizalendo kwa mkoa wetu wa Ruvuma. Sisi wana wa Ruvuma tuko nyuma yenu, tunawaunga mkono sana, endeleeni kupambana kiume ile mbaki kwenye ligi kuu, mapungufu yetu ya msimu huu tutayarekebisha msimu ujao, kwanza kwasasa tunahitiji kupigana kufa kupona ili tuweze kubaki ndani ya ligi kuu. Tunajivunia uwepo wenu, ninyi ni wenzetu, tegemeo kubwa kwa wana Ruvuma.

Kwa nafasi yenu mliyopo katika msimamo wa ligi kuu inahitajika jihadi kubwa kwa ajili ya mkoa wetu. Naamini mnaweza. Hebu pambaneni. Ninyi ni wana Ruvuma hasa. Damu yetu. Wanakwetu, wakunyumba. Mnapofungwa tunapata maumivu makali sana. Tunakosa raha. Tunahitaji mtutoe kimasomamoso ili nasi tufurahi.

Nafasi mnayo tunajua mnaweza kufanya kitu kikaamsha furaha yetu, pambaneni tuko nyuma yenu. Laiti uongozi wa timu ya majimaji ungeandaa utaratibu wa harambee ya kuwawezesha kifedha, naamini wana Ruvuma wenye mapenzi mema na timu yetu ya majimji wangewawezesha na kuwapunguzia ukata mlionao. Katika hili wangetumiwa wanasiasa wetu maarufu, wabunge na mawaziri wote, wafanyabiashara wakubwa na watu wengine wenye ushawishi, vyombo vyetu vya habari vilivyopo ndani ya mkoa wetu wa Ruvuma kama vile Jogoo Fm, Ruvuma Tv , mablogers nk, vilevile vikundi vya sanaa vyote vya mkoa kwa lengo la kutengeneza hamasa ya kwa wana wa Ruvuma kuisaidia Timu yao

Wenzetu Njombe na Iringa wamefanikiwa kuzirejesha timu zao kwenye ligi kuu Daraja la kwanza wakati tumeshazoea majirani zetu hao kuja mkoani kwetu kwa ajili kuzitazama timu kubwa zinapokuja kucheza na timu yetu ya majimaji. Ujio wa timu kubwa kutoka nje ya mkoa wetu zinareta shamrashamra na kuuchangamsha mji wetu wa Songea ambao ndiyo kioo cha mkoa wetu.

Vijana wetu mliyokabidhiwa bendera ya kupepurusha mkoa wetu, pamoja na ukata mlionao, tunawaomba mpigane kufa kupona kuutetea hadhi ya mkoa wenu. Mna wajibu mkubwa kwa wana wa Ruvuma na mkoa kwa ujumla wake. Macho yetu yote yako kwenu.

Nawatakia kila la kheri, aluta continua. Viva Majimaji.

Aman Ng'oma
Mwana wa Ruvuma
0767989713
 
Me ni mngoni pia..naamin kabisa mechi ngumu zilishakwisha..kilichobaki ni kuchukua points kwa vitimu vilivyobaki na tulianza na Toto Africa kesho tunachukua kwa Africa Lyon...Chini ya King Kali Ongala kila k2 kinawezekanaaaa
 
Binafsi siipendi hiyo timu kwa sababu za kisiasa, ukitaka kujua namaanisha nini tuombe uzima, kama itashuka daraja basi 2019 lazima ipande
 
Back
Top Bottom