Timu ya EPA yasema hailali

JuaKali

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
776
118
Timu inayochunguza mafisadi wa Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), ya Benki Kuu (BoT) imesema inafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi yake kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Kwa mujibu wa timu hiyo, hatma ya mafisadi wa makampuni 22 wanaodaiwa kuchota fedha za EPA, Sh. bilioni 133 itajulikana baada ya Oktoba 31 mwaka huu.

Imewataka wananchi kuvuta subira hadi tarehe hiyo, ambayo ndio muda wa mwisho waliopewa na Rais Jakaya Kikwete kurejesha fedha walizochota.

Msemaji wa timu hiyo, Omega Ngole, hakutaka kueleza kwa undani hatua waliyofikia na kiasi cha fedha walichorudisha.

``Kwa sasa hatutaki kuzungumzia kwa kina suala hili? tuna maana yetu kukaa kimya, watu wawe na subira, mambo yatawekwa hadharani wakati ukifika,`` alisema.

Timu hiyo inajumuisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah.

Timu hiyo iliundwa na Rais Kikwete Januari 9, mwaka huu, 2008 katika tangazo rasmi lililotolewa kwa waandishi wa habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

Wakati anaunda timu hiyo, Rais aliipa muda wa miezi sita kukamilisha kazi yake, ambayo ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa na kuchukua hatua za kisheria kwa waliohusika.

Rais aliunda timu hiyo baada ya kuwa amepitia taarifa ya ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2005/06 za EPA katika BoT, uliofanywa na wakaguzi wa Kampuni ya Ernst & Young, kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Ernst & Young iliombwa na Serikali kuifanya kazi hiyo, baada ya kugundulika wizi wa fedha BoT kufuatia ukaguzi wa awali uliokuwa umefanya na kampuni ya Deloitte Dutche ambayo ilikuwa imebaini wizi wa Sh bilioni 40 zilizokuwa zimechotwa na kampuni ya Kagoda Africutural Limited. BoT ilifuta mkataba na Delloite kutokana na kufuatilia wizi huo.

Ernst & Young katika ukaguzi huo, ilibainika Sh. bilioni 133 zilichukuliwa kinyume cha taratibu.

Kazi ya ukaguzi ilianza Septemba 2007 na kumalizika Desemba, mwaka huo

Rais Kikwete alikabidhiwa Taarifa hiyo Januari 7, mwaka huu, 2008 na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali.
Siku ya tatu, baada ya kuwa ameisoma na kuifanyia kazi, Rais aliitolea maamuzi taarifa hiyo, ikiwa ni pamoja na kuunda Timu inayoongozwa na Mwanyika. Pia Rais alitangaza kumfuta kazi aliyekuwa gavana wa BoT, Daudi Ballali.

SOURCE: Nipashe
 
timu inayochunguza mafisadi wa akaunti ya malipo ya nje (epa), ya benki kuu (bot) imesema inafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi yake kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Kwa mujibu wa timu hiyo, hatma ya mafisadi wa makampuni 22 wanaodaiwa kuchota fedha za epa, sh. Bilioni 133 itajulikana baada ya oktoba 31 mwaka huu.

Imewataka wananchi kuvuta subira hadi tarehe hiyo, ambayo ndio muda wa mwisho waliopewa na rais jakaya kikwete kurejesha fedha walizochota.

Msemaji wa timu hiyo, omega ngole, hakutaka kueleza kwa undani hatua waliyofikia na kiasi cha fedha walichorudisha.

``kwa sasa hatutaki kuzungumzia kwa kina suala hili? Tuna maana yetu kukaa kimya, watu wawe na subira, mambo yatawekwa hadharani wakati ukifika,`` alisema.

Timu hiyo inajumuisha mkuu wa jeshi la polisi (igp), said mwema, mwanasheria mkuu wa serikali (ag), johnson mwanyika na mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru), dk. Edward hoseah.

Timu hiyo iliundwa na rais kikwete januari 9, mwaka huu, 2008 katika tangazo rasmi lililotolewa kwa waandishi wa habari na katibu mkuu kiongozi, philemon luhanjo.

Wakati anaunda timu hiyo, rais aliipa muda wa miezi sita kukamilisha kazi yake, ambayo ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa na kuchukua hatua za kisheria kwa waliohusika.

Rais aliunda timu hiyo baada ya kuwa amepitia taarifa ya ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2005/06 za epa katika bot, uliofanywa na wakaguzi wa kampuni ya ernst & young, kwa niaba ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.

Ernst & young iliombwa na serikali kuifanya kazi hiyo, baada ya kugundulika wizi wa fedha bot kufuatia ukaguzi wa awali uliokuwa umefanya na kampuni ya deloitte dutche ambayo ilikuwa imebaini wizi wa sh bilioni 40 zilizokuwa zimechotwa na kampuni ya kagoda africutural limited. Bot ilifuta mkataba na delloite kutokana na kufuatilia wizi huo.

Ernst & young katika ukaguzi huo, ilibainika sh. Bilioni 133 zilichukuliwa kinyume cha taratibu.

Kazi ya ukaguzi ilianza septemba 2007 na kumalizika desemba, mwaka huo

rais kikwete alikabidhiwa taarifa hiyo januari 7, mwaka huu, 2008 na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali.
Siku ya tatu, baada ya kuwa ameisoma na kuifanyia kazi, rais aliitolea maamuzi taarifa hiyo, ikiwa ni pamoja na kuunda timu inayoongozwa na mwanyika. Pia rais alitangaza kumfuta kazi aliyekuwa gavana wa bot, daudi ballali.

Source: Nipashe

kisicho walaza kitu gani wakati kila kitu kipo wazi na sheria ipo,
labda hawalali kwa kujaribu kupindisha sheria kama ni haki wizi ni kasa la jinai na hukumu yake inajulikana
 
Back
Top Bottom