Tigo

Karao

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
1,053
580
Jamani wana jf , mtandao wa tigo umekuwa wakitapeli, mimi sijajiunga na promo zao zozote wala sijihusishi na bahati nasibu zao. Lakini mwenzenu nakatwa pesa daily . Tena viwango tofauti tofauti. Mara 34 mara 60 wakati mwingine 100. Bila sababu yoyote na hawatumi sms kuni inform kuwa wamekata kiasi cha pesa kwa malipo fulani. Wanafanya kimya kimya.

Utakuta nimeweka mfano 500 au 1000 bila kuitumia ikifika kesho yake nikicheck balance nakuta tayari wamesha mega credit yangu. Pia jamani wana jf mtandao huu wa tigo umekuwa ndio mtandao ambao unatoza bei ya juu kuliko mindanao mingine. Mfano kama una 500 kupiga simu tigo - tigo utaongea dk 2 au 3.

Wakati kwenye mitandao mingine kiasi hicho cha 500 unaongea dk 5 hadi 6.

Hawa jamaa wamekuwa matapeli jamani.
 
Back
Top Bottom