Shilewashile
Senior Member
- Dec 2, 2014
- 121
- 48
Tido mtu safi sana tatizo TBC lilikuwa CCM sasa hivi Azam TV itakuwa juu sana mimi namkubali sanaaaaaa!!!!
TIDO alianza TBC na inaonekana kule kulikuwa na siasa nyingi na jana tumeona Azam wamejenga studio ambayo kwa picha zinaonekana si haba!
Cha kujiuliza; Je, alishindwa vipi TBC? Na Je, ataweza AZAM kwa Bakhressa?
Tido ni jembe usipime! amepiga kazi ya ukweli BBC mpaka kesho wanamkubali ijekua hapa Bongo? TBC waliingiza mizengwe na hta hivo alikuea kishawaweka pazuri! Tbc ipo hapo ilipo kwa sababu yake!
Dastan Tido Mhando gwiji na jabali la habari.
ccm na hofu ya mijadala ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kwa ukweli, uwazi na weledi walishindwa kuhimili kishindo cha mbabe huyu mwenye mashiko katika tasnia ya habari.
ccm wakamtimuwa Tido kwa kisingizio cha kuisha mkataba tukijuwa wazi ilikuwa kazi ya ku-review na kumpa mkataba mwingine.
Dastan Tido Mhando aliazimia kukata ngebe za ccm na wanasiasa wake kuifanya TBC isiwe yakisiasa/ccm bali chombo cha umma kwelikweli. Ccm wakaona wanaporwa pakuwahadaa watanzania kwa propaganda za kizushi, vitisho na danganya toto. Kuondoa tishio hilo ccm na kikwete wao wakakataaa katakata ku-review contract hatimaye Mhando kutoswa.
Amakweli sasa watajuta maana huyu jamaa nimbunifu sana sana. nachelea kusema Super sport na bei zao za ajabu watatoweka muda si mrefu hapa TZ. EPL namazagazaga mengine yakutosha yatapatikana AZAMTV. Na chaguo langu ITV kwa kweli imepata mshindani wa kweli.
Bilashaka Tido ataifanya Azam kuwa juuu kabisa.
Jamani mbona BBC Swahili Service ilihanzishwa katikati ya miaka ya 1950s, Hamza Kassongo aliwahi kufanya kazi pale, Oscar Kambona na wengine wengi tu, sisi hatujui mkataba wa Tido na Serikali ulikuwa na masharti yapi - sasa haya mambo ya ku-blame blame tu Serikali bila ya kujua upande wa pili wa shillingi sio fresh kabisa, sio kwamba tuna-under rate uwezo mkubwa wa Ndugu TIDO lakini sio vizuri vile vile kuongeza chumvi.