Wakuu huyu mama anajitahidi sema tuu amezungukwa na watu washenzi wengi kama vile mafisadi papa.Ndugu zangu tujaribu kuwa wakweli,huyu mama haiwezi hii wizara atabaki kupiga porojo tu then muda utakwisha.
Ngoja tuone sakata la kumfukuza OTIENO na Genge lake na kumnyang'anya Mkurugenzi Jiji la Mwanza maeneo yake ya Luchelele kama itafanikiwa. Hiyo ni blaa blaa tu. TUNAISUBIRI SARAKASI HIYO. Imeelezwa kwamba wale waliotorosha wanyama pori wakiwa HAI/ wazima na uzima wao pamoja na sakata lote hilo bado wamepandishwa vyeo!! ukistaajabu ya MUSA utaona ya FIRAUNI.................Nilijaribu kuangalia hotuba ya huyu mama kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake,pamoja na kumsikiliza hakijumuisha hotuba yake na zaidi wakati akijibu hoja za wabunge wakati bunge limekaa kama kamati ya matumizi..Niwe wazi na nadhani kama kuna mtu alitazama anaweza kuniunga mkono..Otherwise...sitegemei jipya kutoka kwake,zaidi nategemea hii wizara kufa kabisa...
- Huyu mama anaonekana haijui hii wizara vyema na hana majibu sahihi kwa hoja zenye mshiko
- Huyu mama pamoja na U-prof wake na uzoefu wa kazi katika nyanja ya makazi tena kimataifa hajui kujenga hoja na kujipanga kutengeneza hoja zenye tija.
- Huyu mama anaongea bila kuwa na taarifa za kuhusu hali ya nchi yetu...hajui mafisadi wameishika na bosi wake ni mmoja anaewalinda...
- Huyu mama nahisi ni mtendaji na sio kiongozi...anafaa sana kazi kama katibu mkuu nk..na sio uwaziri....