Kama wiki 2 zilizopeta nilienda TIB BENKI nikauliza mkopo kwa ajili ya mradi wa kilimo na ufugaji.
Niliwauliza kuhusu pesa walizopewa kwa ajili ya kukopesha wakulima na wafugaji, wakasema hawana habari kama hiyo.
Pia wakasema kama ni kukopesha ni wakulima wakubwa tu wenye mashamba makubwa kama heka 100 na zaidi.
Pia wanasema Riba ni kubwa, sasa sijui wakulima wadogo nao watafaidika na hiyo mikopo au ni matajiri tuuu?
Sasa nashangaa nimesoma kwenye gazeti kuwa wapeleka bilion 3 za EPA TIB, ni kiini macho, au nini?
Naomba kama kuna mtu anafahamiana na Mbunge waulize ni lini wataanza kutoa hiyo mikopo? Pia Mikopo ni kwa wakulima wakubwa tu au na wadogo watapata? Pia Riba ni nafuu au ni kama commercial bank nyingine kama NBC,CRDB,NMB,AKiba, ...??
Hizo habari za EPA kupelekwa TIB ni SIASA au ni Ukweli???
Wananchi ni lini watawezeshwa, tuachane na siasa za majukwaani?