Thread maalum kukumbushana michezo ya utotoni iliyosahaulika

wakati niko primary kucheza gololi na kujipikilisha ndiyo vilikuwa kwenye chat.

Funzo
1. Gololi, concentration
2. Kujipikilisha, waliokuwa serious ndo machef hao šŸ˜
Kama nakuona hapa.
FB_IMG_1704427824341.jpg
 
Umenikumbusha enzi hizo mchezo wa KUWINDA NDEGE PORINI,
MJUBA NILIKUA NASOKOTA NYANGA ZANGU KAMA 100 HIVI,
ALAFU NAZAMA PORINI NIKIRUDI SIKOSI NDEGE KAMA 20 KWENYE KIFUKO,NILIKUA NALENGA NDEGE MPAKA WATU WANASTAAJABU.

SIKU MOJA NIMETOKA TU SCHOOL NILIVYOINGIA NDANI NIKABADILI NGUO NIKATOROKA BILA KULA,
VILE NAKATIZA TU KWENYE CHOCHO NIKAKUTANA NA WAZEE WAWILI,MMOJA AKIWA BABU YANGU WAKANIONYESHA NDEGE ALIKUA MKUBWA MFANO WA MWEWE AU KIPANGA,AKIWA JUU YA MNAZI,WAKANAMBIA UKIMSHUSHA HUYO TUNAKUPA BUKU,KUMBUKA HIYO MIAKA YA 90 NA...BUKU SIO MCHEZO ADA TULIKUA TUNALIPA 2000 MSINGI KWA MWAKA.
MWANAUME NIKAWEKA NYANGA KWENYE MANATI NIKAPIGA,NIKAMLENGA YULE NDEGE AKAANGUKA.WALE WAZEE WAKANIPA BUKU NIKARUDI ZANGU HOMU ILA NDEGE NILIWAACHIA MAANA NILISHAAMBIWA MWEWE AU KIPANGA HALIWI.
HII MIAKA HAKUNA HII MICHEZO YANI WATOTO WAMEKUA NA MICHEZO TOFAUTI KABISAA.
Kama nakuona bro.
Screenshot_20240105_071624_Facebook.jpg
 
Mchezo wa kibaba baba.

Kuucheza: mnagawana majukumu na majina ya kufamilia. Mwingne mama, baba, mjomba watoto nk.
Mimi nilikuwa nachagua kuwa baba. Muda wa kulala namchukua mama yao naenda kumtafuna.
Funzo: Inanisaidia sahivi kwenye kugegeda wanawake
Hapo miye kila wiki nilikuwa baba harusi kisa tu na kaunda suti kama nne hivi do nikawa nafanana na baba harusi so kila mchezo wa kibaba tunaanza na harusi mwamba nakuwa baba harusi haa haaa mke wangu ANITA upo wapi njoo tuyajenge maisha
 
Hapo miye kila wiki nilikuwa baba harusi kisa tu na kaunda suti kama nne hivi do nikawa nafanana na baba harusi so kila mchezo wa kibaba tunaanza na harusi mwamba nakuwa baba harusi haa haaa mke wangu ANITA upo wapi njoo tuyajenge maisha
Hahaaaaa, tumetoka mbali sana.
 
2. DANADANA

Huu pia ulikuwa ni mchezo wa mpira wa miguu. Hapa wachezaji walikuwa wanaoneshana uwezo wa kuwa na stamina na control ya mpira ukiwa mguuni kwa kuupiga piga pasipo kuanguka.

Lilikuwa linachorwa jadwari kwa kila mshiriki(mchezaji) ili kuhesabu idadi ya DANADANA(idadi ya kuupiga mpira pasipo kuanguka kwa kugusa chini).

Mnawekeana milestone(kipimo/ukomo) ili mtu kushinda. Kwa mfano danadana 1000. Kisha mnapiga kwa zamu wakati wachezaji wengine wakihesabu.

Kuna wachezaji walikuwa mahiri sana. Unaweza kuhamaki kapiga DANADANA zaidi ya 500 kwa mkupuo (round moja) . Ukiwa na matege au njaa hawezi kufika mbali maana utaishia DANADANA 50. Ilihitaji stamina kubwa kusimamisha mguu mmoja kwa muda mrefu wakati mwingine ukipiga DANADANA . Pia control na focus ili mpira ubaki karibu yako.

Kinara wa DANADANA kwenye kitongoji chetu alikuwa anaitwa JOFU SHIBE. Huyu jamaa aliweza kupiga hadi DANADANA 800 kwa mkupuo mmoja. Siku hizi umri umeenda na alishaoa wake wawili hata 20 hawezi kufikisha .

Pia vijana wa hovyo wazee wa CHAPUTA dronedrake wasingeweza kupiga hata DANADANA 10 maana miguu ingeishia kutetemeka tu.

FUNZO: Stamina na Control ya miguu na Focus ya akili.
Kaka angu ni fundi wa Huu mchezo balaa, alikua anacheza had wenzake wanakereka.
 
3. KOMBOLELA.

Huu mchezo wengi mnaujua. Mtu mmoja analinda(anazinga) kopo au mpira kisha wachezaji wengine wanajificha maeneo ambayo sio mbali na kopo au mpira ulipo.

Mchezaji akionekana na mlindaji(mzingaji) basi hutajwa kwa jina. Mfano "KOMBOLELA ELVIS". Mchezo huu ulinoga hasa muda wa jioni jua likianza kuzama.

Kila mchezaji atakayeonekana na kutajwa jina lake basi aliwekwa kizuizini kwenye duara maalum lililochorwa mpaka wachezaji wote wapatikane. Kuna wachezaji wakienda kujificha walikuwa wanapotea mazima mpaka giza linatanda , basi ndio unakuwa mwisho wa mchezo.

Ikitokea mlizi wa mpira au kopo (Mzingaji) akajisahau basi hutokea mchezaji mjanja akabutua(kulipiga teke) kopo au mpira na kuwaokoa waliokwisha wekwa kizuizini na kwenda kujificha upya.

FUNZO: Mchezo ulikuza ushirikiano na kujuana baina ya watoto wa mtaa au kitongoji kimoja kwa kufahamiana majina wote.
Nimeucheza sanaa.
 
Mchezo wa kibaba baba.

Kuucheza: mnagawana majukumu na majina ya kufamilia. Mwingne mama, baba, mjomba watoto nk.
Mimi nilikuwa nachagua kuwa baba. Muda wa kulala namchukua mama yao naenda kumtafuna.
Funzo: Inanisaidia sahivi kwenye kugegeda wanawake
 
Wewe mtoto wa uswazi, hii michezo ukienda uswazi bado ipo inachezwa kwwni inaitaji muwe watoto wengi ambao hamfungiwi ndani yani mpo oya oya, so kama umecheza hii lazima uwe mtoto wa uswazi uzuri wa hii michezo huwezi kukuta kijana kawa shoga
Mawazo yako yanawaza ushoga tyuuh, na ulichojaza moyoni.
Bas wako mashoga kibao wamecheza kombolela na zaidi ya hiyo.
 
Nyanga unamaanisha gololi. Sisi tulikuwa tunazifinyanga/sokota kisha tunazianika juani then ndio tunazitumia kuwindia ndege.
Ndio hizohizo,tulikua tunachimba udongo then tunafinyanga,kwa lugha ya uswazi tulikua tunaita mbwewe.
 
Dah, umeifanya siku yangu iwe Murray kabisa bro. One touch, wacha weeeee. Dah, tumetoka mbali sana.
šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£Hv kumbe ni one touch tulikua tunakosea tunatamka "wen taji", sisi tulikua tunaita gusa na kuacha bn ngeli zero
 
Hahaha... Play station 1 mpaka 5, Nintendo, Xbox...
Hii PlayStation nakumbuka miaka hyo tukitoka school Mikocheni primary tunaingia nyumbani kwa rafiki yetu mmoja wa kishua hapo Victoria. Anatuachia tunacheza na wengine wanacheza basket nje..yeye anaenda kupiga tuition kwa mwalimu kitabu makumbusho. Enzi hizo ukifaulu umefaulu kweli...kwakwel ni yeye tu alifaulu akaenda Benjamini mkapa.

Ukirudi home unaonekana ulikuwa school unapiga book kumbe ulikuwa kwakina Billy.

Nimefungua code..kuna mwenzangu humu wa mikocheni ?
 
wakati niko primary kucheza gololi na kujipikilisha ndiyo vilikuwa kwenye chat.

Funzo
1. Gololi, concentration
2. Kujipikilisha, waliokuwa serious ndo machef hao šŸ˜
Hii ya kujipikilisha mbona ipo mpaka sasa na itaendelea kuwepo? Watoto wa kike karibu wote huwa wanapitilia huu mchezo. Tena sasa hivi dukani kuna vyombo vya kitoto vya kujipikilisha na ni duniani kote. Wanaume wao zaidi wanachezea toys za magari nk
 
Kwangu misamiati mipya hiošŸ¤ šŸ¤ !

Sema zama hizi watoto hawana michezo kabisa..hasa wa uswahilini
Mkuu una uhakika? Nadhani ni kwa sababu hauko kwenye circles zao hivyo huwezi kujua kila kitu. Ila nakubaliana na wewe kuwa watu hawaachii tena watoto kuzurura hovyo ila watoto dunaniani kote wanacheza michezo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom