Thread maalum kukumbushana michezo ya utotoni iliyosahaulika

doba ngumi
Cheza uchezavyo mpira usije penya kwenye doba yako, ikitokea umepigwa doba unashambuliwa na watu wote salama Yako ni kwenda kugusa object tuliyokubaliana uiguse endapo umepigwa doba......kimbembe inakua kufikia object maana wanakuzuia

Fimbo cheza
Sheria
Hurusiwi kushika fimbo zaidi ya Moja
Shika fimbo nchani
Unatakiwa uwe na fimbo mda wote

Zingn nimezisahau bn ila Kuna ile mnapinga hamna kuongea ko hutakiwi kuonekana unaongea ukidakwa ni kifinyo, nyingine hamna kuitika jina lako ukiitika stiki 3 zinakuhusu
 
Umenikumbusha enzi hizo mchezo wa KUWINDA NDEGE PORINI,
MJUBA NILIKUA NASOKOTA NYANGA ZANGU KAMA 100 HIVI,
ALAFU NAZAMA PORINI NIKIRUDI SIKOSI NDEGE KAMA 20 KWENYE KIFUKO,NILIKUA NALENGA NDEGE MPAKA WATU WANASTAAJABU.

SIKU MOJA NIMETOKA TU SCHOOL NILIVYOINGIA NDANI NIKABADILI NGUO NIKATOROKA BILA KULA,
VILE NAKATIZA TU KWENYE CHOCHO NIKAKUTANA NA WAZEE WAWILI,MMOJA AKIWA BABU YANGU WAKANIONYESHA NDEGE ALIKUA MKUBWA MFANO WA MWEWE AU KIPANGA,AKIWA JUU YA MNAZI,WAKANAMBIA UKIMSHUSHA HUYO TUNAKUPA BUKU,KUMBUKA HIYO MIAKA YA 90 NA...BUKU SIO MCHEZO ADA TULIKUA TUNALIPA 2000 MSINGI KWA MWAKA.
MWANAUME NIKAWEKA NYANGA KWENYE MANATI NIKAPIGA,NIKAMLENGA YULE NDEGE AKAANGUKA.WALE WAZEE WAKANIPA BUKU NIKARUDI ZANGU HOMU ILA NDEGE NILIWAACHIA MAANA NILISHAAMBIWA MWEWE AU KIPANGA HALIWI.
HII MIAKA HAKUNA HII MICHEZO YANI WATOTO WAMEKUA NA MICHEZO TOFAUTI KABISAA.
 
MICHEZO YA KIBABA NDIYO NILIKUA NAIPENDA MNO.

TENA MIMI NDIYO FATHER HOUSE.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Nilijaribu hii na kasichana kanaitwa Zai (mungu amlaze mahali pema peponi),kumbe watoto wenzangu walikua wanakula chabo,wakaenda kusema kwa bibi,bibi akauza kesi kwa dingi dah nilichezea stik sintokuja kusahau mpaka naingia kaburini.
 
--Mchezo wa BONG'OA,
Mchezo huu tulikuwa tunawekeana ahadi tunaita kupinga,,(tunagusana vidole vya mikono kama alama ya kuanza rasmi ahadi yetu)

Ni ahadi kwamba ukimwona mwenzako ameinama basi unampiga teke matakoni bila kujali position aliyopo..

Basi kuna siku ndugu yng mmoja tulipinga huo mchezo,,(BONG'OA)
Alikuwa ameinama jikoni anapuliza moto nilipiga teke la matako nusu aingie kwenye moto.
Mbaya Zaidi nilimpiga teke mbele ya baba yake mzazi akitazama mchezo.

Tulikula makofi + vibokon vya Dunia ,
ikawa ndy mwisho wa mchezo huo ,
tukaambiwa tupinguwe,,(kufuta ahadi)
 
Huu mchezo hatari sana. Wakati nikiwa primary mwaka 2000 darasa la tatu kipindi hicho mifuko ya Kamba aina ya sports inabamba, jamaa aliniotea assemble (mstarini) tukiwa tumechuchumaa. Daah nilichosikia ni plate kupasuka maana kama isingekuwa kuvaa ule mfuko wa sports wenye plate ndani ingekuwa balaa Sana. Wanafunzi walinicheka Sana.
Siku moja baada ya lile tukio la mstarini tuliambiwa na mwalimu tukateke maji bombani(maji ya chemchem). Sasa jamaa alienipiga bong'oa siku ile alikuwa na kiu ya maji kwa hiyo akaomba apishwe ainame kwenye bomba anywe maji mengi kwa haraka. Nikaona bahati ndio hii. Nilimpiga kigoti akabinukia ndani ya maji na kulowa chepechepe. Wanafunzi walimcheka Sana aisee. Baada ya hapo ilibidi tufute mchezo. Nilimwonea Sana huruma.
 
Mchezo wangu pendwa huu. Tulikuwa tunacheza mpira wa miguu kwa kuchora uwanja, kuweka magoli then mnachukua vijiti vya fagio la chelewa(Yanayotengenezwa kwa majani ya minazi) mnavichomeka chini ya udongo na kuvipanga kama wachezaji 11 wa mpira wa miguu wanavyojipanga uwanjani( Position).

Tulikuwa tunatumia mavi ya mbuzi au vile vimbegu vya mti wa muarobaini kama Mpira. Hapo tulikuwa tunavipa majina ya wachezaji tuliokuwa tunawasikia radio radioni wa Tomu unayoipenda. Mi nilikuwa Yanga ya 1994 ya akina Lunyamila. Nilikuwa naupenda sana huu mchezo.
FB_IMG_1704342233568.jpg
 
Huu mchezo hatari sana. Wakati nikiwa primary mwaka 2000 darasa la tatu kipindi hicho mifuko ya Kamba aina ya sports inabamba, jamaa aliniotea assemble (mstarini) tukiwa tumechuchumaa. Daah nilichosikia ni plate kupasuka maana kama isingekuwa kuvaa ule mfuko wa sports wenye plate ndani ingekuwa balaa Sana. Wanafunzi walinicheka Sana.
Siku moja baada ya lile tukio la mstarini tuliambiwa na mwalimu tukateke maji bombani(maji ya chemchem). Sasa jamaa alienipiga bong'oa siku ile alikuwa na kiu ya maji kwa hiyo akaomba apishwe ainame kwenye bomba anywe maji mengi kwa haraka. Nikaona bahati ndio hii. Nilimpiga kigoti akabinukia ndani ya maji na kulowa chepechepe. Wanafunzi walimcheka Sana aisee. Baada ya hapo ilibidi tufute mchezo. Nilimwonea Sana huruma.
Mimi almanusra nimpasue dogo pumbu zake. Nilipiga take hadi nilimuonea huruma. Ulikuwa mchezo wa kikatili sana.
 
Umenikumbusha enzi hizo mchezo wa KUWINDA NDEGE PORINI,
MJUBA NILIKUA NASOKOTA NYANGA ZANGU KAMA 100 HIVI,
ALAFU NAZAMA PORINI NIKIRUDI SIKOSI NDEGE KAMA 20 KWENYE KIFUKO,NILIKUA NALENGA NDEGE MPAKA WATU WANASTAAJABU.

SIKU MOJA NIMETOKA TU SCHOOL NILIVYOINGIA NDANI NIKABADILI NGUO NIKATOROKA BILA KULA,
VILE NAKATIZA TU KWENYE CHOCHO NIKAKUTANA NA WAZEE WAWILI,MMOJA AKIWA BABU YANGU WAKANIONYESHA NDEGE ALIKUA MKUBWA MFANO WA MWEWE AU KIPANGA,AKIWA JUU YA MNAZI,WAKANAMBIA UKIMSHUSHA HUYO TUNAKUPA BUKU,KUMBUKA HIYO MIAKA YA 90 NA...BUKU SIO MCHEZO ADA TULIKUA TUNALIPA 2000 MSINGI KWA MWAKA.
MWANAUME NIKAWEKA NYANGA KWENYE MANATI NIKAPIGA,NIKAMLENGA YULE NDEGE AKAANGUKA.WALE WAZEE WAKANIPA BUKU NIKARUDI ZANGU HOMU ILA NDEGE NILIWAACHIA MAANA NILISHAAMBIWA MWEWE AU KIPANGA HALIWI.
HII MIAKA HAKUNA HII MICHEZO YANI WATOTO WAMEKUA NA MICHEZO TOFAUTI KABISAA.
Nyanga unamaanisha gololi. Sisi tulikuwa tunazifinyanga/sokota kisha tunazianika juani then ndio tunazitumia kuwindia ndege.
 
3. KOMBOLELA.

Huu mchezo wengi mnaujua. Mtu mmoja analinda(anazinga) kopo au mpira kisha wachezaji wengine wanajificha maeneo ambayo sio mbali na kopo au mpira ulipo.

Mchezaji akionekana na mlindaji(mzingaji) basi hutajwa kwa jina. Mfano "KOMBOLELA ELVIS". Mchezo huu ulinoga hasa muda wa jioni jua likianza kuzama.

Kila mchezaji atakayeonekana na kutajwa jina lake basi aliwekwa kizuizini kwenye duara maalum lililochorwa mpaka wachezaji wote wapatikane. Kuna wachezaji wakienda kujificha walikuwa wanapotea mazima mpaka giza linatanda , basi ndio unakuwa mwisho wa mchezo.

Ikitokea mlizi wa mpira au kopo (Mzingaji) akajisahau basi hutokea mchezaji mjanja akabutua(kulipiga teke) kopo au mpira na kuwaokoa waliokwisha wekwa kizuizini na kwenda kujificha upya.

FUNZO: Mchezo ulikuza ushirikiano na kujuana baina ya watoto wa mtaa au kitongoji kimoja kwa kufahamiana majina wote.
Hahaaaaa nilishamvunja jamaa vidole. Tulianza jioni, sasa zamu yangu ya kuzinga ikaingia kigiza kilipoingia. Nikatoa mpira wa kuzingia nikaweka jiwe then nikafanya naenda wawatafuta jamaa akaja mbio kubutua mpira ili kuwakomboa wenzake niliowashika. Kakutana na kupiga jiwe, kilio chake hapo. Jamaa akavunja vidole na akabandua ngozi za vidole(Kutoa ikwaju)
 
doba ngumi
Cheza uchezavyo mpira usije penya kwenye doba yako, ikitokea umepigwa doba unashambuliwa na watu wote salama Yako ni kwenda kugusa object tuliyokubaliana uiguse endapo umepigwa doba......kimbembe inakua kufikia object maana wanakuzuia

Fimbo cheza
Sheria
Hurusiwi kushika fimbo zaidi ya Moja
Shika fimbo nchani
Unatakiwa uwe na fimbo mda wote

Zingn nimezisahau bn ila Kuna ile mnapinga hamna kuongea ko hutakiwi kuonekana unaongea ukidakwa ni kifinyo, nyingine hamna kuitika jina lako ukiitika stiki 3 zinakuhusu
Sisi tulikuwa tunaita tobo dunda au tobo ngumi. Aiseeee, hatari hiyo.
 
3. KOMBOLELA.

Huu mchezo wengi mnaujua. Mtu mmoja analinda(anazinga) kopo au mpira kisha wachezaji wengine wanajificha maeneo ambayo sio mbali na kopo au mpira ulipo.

Mchezaji akionekana na mlindaji(mzingaji) basi hutajwa kwa jina. Mfano "KOMBOLELA ELVIS". Mchezo huu ulinoga hasa muda wa jioni jua likianza kuzama.

Kila mchezaji atakayeonekana na kutajwa jina lake basi aliwekwa kizuizini kwenye duara maalum lililochorwa mpaka wachezaji wote wapatikane. Kuna wachezaji wakienda kujificha walikuwa wanapotea mazima mpaka giza linatanda , basi ndio unakuwa mwisho wa mchezo.

Ikitokea mlizi wa mpira au kopo (Mzingaji) akajisahau basi hutokea mchezaji mjanja akabutua(kulipiga teke) kopo au mpira na kuwaokoa waliokwisha wekwa kizuizini na kwenda kujificha upya.

FUNZO: Mchezo ulikuza ushirikiano na kujuana baina ya watoto wa mtaa au kitongoji kimoja kwa kufahamiana majina wote.
Wewe mtoto wa uswazi, hii michezo ukienda uswazi bado ipo inachezwa kwwni inaitaji muwe watoto wengi ambao hamfungiwi ndani yani mpo oya oya, so kama umecheza hii lazima uwe mtoto wa uswazi uzuri wa hii michezo huwezi kukuta kijana kawa shoga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom