The worst valentine's day

Nimepigika

Member
Dec 17, 2012
9
4
THE WORST VALENTINE’S DAY
0683213365
“….kwa,kwa,kwa” ile sauti ya viatu bado ilisikika ikitembea katika korido ya nyumbani kwangu na hali ya hewa ilikuwa ya upepo mkubwa..hofu ilitaka kunikamata lakini nilihisi kuwa naota na hivyo nilitoka tena kwa mara nyingine taratibu nikichungulia ni nani aliyekuwa akija lakini sikuona kitu,,,nilifungua dirisha nakutazama nje niliona giza nene na sauti na mwanga wa radi ukipiga hapo mvua ikafata na ile sauti sikuisikia tena,,,bado shauku yangu ilikuwa ni kukutana na JAMSHID JABIR ambaye ni mwaka wa tatu sasa toka nimekutana nae kwenye mtandao wa kijamii wa FACEBOOK,,,alikuwa mwanaume mtanashati kwa kumwangalia kwenye picha nakumbuka ni wakati natoka Finland kuja Tanzania ndiyo siku niliamua kuwa nitakuwa na yeye, hapo ikiwa ni miaka miwili toka anitongeze na mimi kukubali kuwa na yeye,,ingawaje nilikuwa mkristu lakini niliamini kabisa kwa Jamshidi nitabadilisha dini,,wengi wangeona uamuzi wangu huu ni wa kishenzi lakini sikujali kwa kuwa mapenzi hayana kanuni maalumu wala hakuna sehemu ya kuweza kuonana na mtu ambaye angeweza kuyafanya maisha yako yawe ya furaha,,niliamini hivyo.
Nakumbuka mara baada ya Jamshid na mimi kukubaliana kuwa wapenzi alifunga safari na kuja Finland kunifata kipindi icho nikisoma chuo kikuu cha Helsinki kule Finland,,alinieleza mengi kuhusu yeye lakini kikubwa ni kwamba baba yake alikuwa ni mfanya biashara wa mafuta huko Mascat nchini Oman na kwamba asilia yao ni visiwa vya karafuu Zanzibar na kwa wakati huo anaishi Zanzibar na wazazi wake,,nilimpenda sana si kwa sababu kwao walikuwa na uwezo hapana nilimpenda kwakuwa yeye alikuwa mwanaume wa kwanza kunivutia,,historia ya maisha yangu haikunipa kabisa mwanya wa kuyatamani mapenzi licha tu ya kuyasogelea na hii ndiyo sababu kubwa iliyonifanya niamini kwa hakika kabisa nilikuwa nikimpenda Jamshid,,,katika maisha na Jamshid nilijitahidi sana kukusanya taarifa zinazomuhusu na kuchunguza kwa kadiri nilivyoweza na nilijiridhisha kabisa kuwa Jamshid ndiye mwanaume wa maisha yangu, nilitunza usichana wangu ili kumuhifadhia Jamshid kwa kipindi chote toka nijuane naye na LEO HII ikiwa ni siku ya wapendanao nilijiandaa kabisa KUUTOA USICHANA WANGU kwa Jamshid,,nakumbuka wakati narudi kutoka masomoni nilitamani sana kuwaarifu marafiki zangu kuhusu Jamshid lakini nililiweka hilo kuwa siri kwa muda mpaka nikatambulishwe nyumbani kwa kina Jamshid,,,kwakuwa wazazi wangu walifariki siku nyingi na sikuwa na ndugu nchini Tanzania niliishi peke yangu na Magret ambaye ni mfanyakazi wa ndani kwenye lile jumba kubwa nililoachiwa na Mzee Herman Obieng ambaye ndiye baba yangu aliyefariki dunia miaka mingi iliyopita baada ya mama yangu kubakwa na majambazi nane waliovamia nyumba yetu siku mbili kabla ya kifo cha baba yangu,,,unyama ule uliotendeka mbele yangu ndio uliofanya niwachukie wanaume kuliko kitu chochote lakini kwa Jamshid siku na la kusema…
*******
Jana yake asubuhi nilipokea simu kutoka kwa Jamshid akinitaarifu kuwa angekuja kwangu siku iliyofuata mabayo ilikuwa ni siku ya wapenda nao maarufu kama Valentine’s day,,hii kwangu ilikuwa taarifa ya furaha sana,,,siku iyo nilikaa nikiwasiliana na Jamshid na maongezi yetu yote yalilenga katika kufanya mapenzi tu,,kwa hakika na dhati ya moyo wangu nilitamani sana kulala kitanda kimoja na Jamshid,,nilitamani sana Jamshid aweke historia katika maisha yangu..
*****
Niliamka mapema siku hiyo na nilianza kufanya usafi kila kona ya nyumba hiyo,,furaha niliyokuwa nayo siku hiyo ilikuwa ni kubwa kuliko furaha yangu niliyowahi kuwa nayo siku nilipofika nchini Finland,,ni kubwa sawa na furaha ambayo ningekuwa nayo kama wazazi wangu wangerudishwa katika maisha yangu,,,majira ya saa 8 mchana ya siku iyo niliwasiliana na Jamshid na alinitaarifu kuwa yuko bandarini huko Zanzibar akisubiri boti ya kuja Dar na majira ya saa 12 jioni nilimtuma Magret kwa rafiki yangu akalale ili kunipa uhuru wa kula raha na Jamshid,,,nilifahamu fika nyumba ile ilikuwa kubwa kwa yeye kukaa lakini nilitaka kuwa huru zaidi kama ni kulia na kucheka nilitaka nilie na kucheka mpka mwisho wa uwezo wangu,,,kwa hakika hii ilikuwa siku kubwa kwangu ukizingatia ilikuwa ni siku ya kwanza ya wapendanao mimi kuwa na mpenzi, kwaiyo niliichukulia kwa uzito wa peke yake..
“kwa,,kwa,,kwa”nilisikia tena ile sauti ya viatu ikitembea kwenye korido kuelekea jikoni,,hapo ilikuwa inaelekea saa 3 ya usiku na simu ya Jamshid haikua inapatikana tena,,,taratibu upepo na radi zilizidi na hatimaye sasa umeme ukakatika na mwanga wa mishumaa ulianza kuiangaza nyumba ile toka pale sebuleni mpaka chumbani,,hofu na woga ulianza kunijia nikanyanyua simu yangu ya mkononi kutaka kupiga kwa Jamshid lakini nilichoka baada ya kukutana na ujumbe unaoonyesha kuwa hakukuwa na mtandao “NO SERVICE”,,,hapo ilizidi na taratibu furaha yangu ilianza kupotea zile ngurumo za radi na sauti za kutisha ziliusumbua ubongo wangu nisijue cha kufanya na ghafla nilitazama ile nguo niliyokuwa nimevaa nikashtuka kuona si nyeupe tena bali nyekundu taratibu nilianza kusikia milango ikifunguliwa na upepo mkali ukiingia ndani lakini ile mishumaa haikuzimika nilianza kulia kwa nguvu lakini sauti haikutoka, nilianza kusikia sauti za ajabu kama wanyama wa mwituni na ghafla madirisha yalifunguka na kwambali kulikuwa na mwanga mkubwa na kundi kubwa la watu wakija usawa wa nyumbani kwangu sikuelewa chochote na hapo mkojo mwembamba machozi na kamasi vilinitoka,,mawazo ya Jamshid hayakuwepo tena na hapa sikuwaza kitu chochote,,nilitamani iwe ni ndoto lakini haikuwa,,,wakati nataka kukimbia nilishtuka kuona siwezi kutoa mguu pale nilipo,,,na mpaka hapo lile kundi kubwa la watu lilikuwa limekaribia kabisa na niliona ukuta wa nyumba ukifunguka kama geti la uwanja wa taifa na wale watu waliingia na kusimama mbele yangu walikuwa wamevaa nguo nyekundu na wamejifunika vitambaa vyeusi,,nilipatwa na haja ndogo kwa mara nyingine tena na hapo mmoja aliyekuwa mbele alivua kile kitambaa na hapo ndipo nilipogundua ni Jamshid………
UNAHISI NINI KILIMTOKEA HUYU MSICHANA BAADA YA HAPO?? HII NI ZAWADI YANGU KWENU YA SIKU YA WAPENDANAO….SI KILA MZUNGU PADRI,,HUO NDIO UJUMBE.
 
hadithi hadithi, hadithi njoo utamu kolea!

King'asti, season ya hadithi haijaisha tu? Daym Mtamu mchungu.
 
Last edited by a moderator:
Mmmh.....Usianze kutuogopesha maana mie mpenzi wangu nimempata humu JF halafu nategemea kuonana nae hiyo siku ya Wapendanao.. Lol
 
isije ikawa ni ndoto.hadithi kama hizi,hazifai kusomwa usiku.nitajitisha bure
 
it is scary nini kilitokezea tena after heee mbona naogopa tena mapenzi ya fb
 
Back
Top Bottom