The Working Class, Savages in Suits

Dk 10 izo zishaenda af Lara 1 hajatokea bado. Hii alosto nomaa. Pamoja kwamba nasinzia lakini ntasubiri mpaka nione mwisho wake. Lara 1 ukiamua leo naweza kesha na wewe
 
Dk 10 izo zishaenda af Lara 1 hajatokea bado. Hii alosto nomaa. Pamoja kwamba nasinzia lakini ntasubiri mpaka nione mwisho wake. Lara 1 ukiamua leo naweza kesha na wewe
Alosto haswaaa ukiangalia pusher mwenyew amenyuti
 
Anthing is possible under the sky!

Wakakubaliana kumshughulikia HOM ipasavyo, by the time he is HIV+ ataisoma namba. Linda ikabidi tu amwambie Ronny uweli kuwa inambidi aende cause HOM kamshika pabayaa. Asipoenda HOM atamkomoa Mina, ili kumkomoa Linda ki design.Mmmmmhhhhhh! Ronny akakubali shongo upandeee sasa afanyajae na kikombe ndo kichunguuu. Maskini wasipoteteana wao kwa wao ndo watakuwa washajimalizaa.

Joy huku akawa kaanza kwenda clinic hizi za ARV, ikaonekana CD 4 ziko chini, ikawa lazima aende kwenye ushauri na dawa. Akamwambia Linda mwenzio naogopaaa, watu hapa wakijua itakuwajee. Linda akmwambia mimi nitakuwa nakusindikiza Temeke, hakuna mtu wa humu atakuwa kituo cha huko, hakuna atakae jua. Siku ya kwanza kwenda Linda akamsindikiza ikawa watu wote kwenye folleni watu wazimaa tu, hakuna hata kijanaa. Looh! Basi ukimya hamna mtu anae ongea na mwenzie, hali ya hewa kama Sobibor. Akachukua dozi, wakarudi.

Akawa kaianza ile dozi kimya kimya maskini ya Mungu. Sasa akameza zile dawa kipaketi kikaishaa. Huku akawa anamtumia sms HOM, nimekuelewa sanaa, i want us dating. HOM akawa anazingua, hakatai wala hakubaliii. Asipomuanza Joy basi, ila akimuanza anajibu vizurii tu, basi akawa ana push for a date na HOM. HOM anajitia im so busy na hii lauch, i dont hve much time, hivo yani anazingua kaya.

Linda yupo standby kwa tour n kumfatilia Joyce mpango unaendajeee. Basi akipunch hivi wanakuja hiviii. Ikawa bado hakijaelewekaaa. Sasa Jose uzembe wake kile kikasha cha dawa hizi za ARV akakitupa kwenye dustbin ya ofisini kwao. Hawa wafagizi wakakiona wakati wa kwend akumwaga. Ikawa mfagizi mmoja akawaambia wenzie utaamini yule dada ana UKIMWI! Watu hawakuaminiii. Mfagizi akamnongoneza bosi mmoja, akamtonya mwenzieee, akamtonya mwenzieee, ikaenea ofisi nzima chini chini.

Wa kwanza kuuliza alikuwa dada Asha hivi huyu Joyce ana UKIMWI? Linda akamwambia mimi sijui kwani umesikia wapi? Akamwambia nasikia anakunywa ARV. Mmmmh Linda akajua kimenukaaa. Linda akamwambia sidhaniii. Dada Asha akasema jamanii nyie wadada muwe waangalifuuu Kama kweli itakuwa makubwaa.

Fukunyuku zikamfikia Vicencia, akazipeleka kwa HOM, HOM akamtext so ulitaka kuniua makusudi? Joy akastukaaa! Unaamaanisha nini? HOM akamwambia si unakunywa ARV wewe? Kila mtu humu ndani anajua. Joy akachokaa. Akasema kwa hio ndo mlipanga na Linda kunikomoa? Joyce akasema walaa hio mipango yangu binafsiii. Bahati yako! HOM akamuuliza kwani Joy mimi nilikukosea nini mpaka utake kunidedisha na deadly virus? Makusudiii? Sawa mimi naweza kuwa navyo vyangu binafsiii, ila kuniongezea mshikaji ni hatari mjue. Kumbe humu ndani mnanichukia kiasi hiko? Basi nitabadilika kuanzia sasa. Haya mambo yetu tumeyapeleka mbali sanaa.

Siku hio ofisini Vicencia akaenda kwa HR kutaka Joy atengwe choo, na asishee vyombo mule ndani, yaani anyanyapaliwe. Hr akamwambia haiwezekani kuna sheria za nchi zinawalinda hawa watu. Basi akaanza kumtangaza flani ana UKIMWI, flani ana UKIMWI. Pressure ikawa kubwa sanaa, Joy aka resign, akacha kazi, ila urafiki ukaendela siku ya dawa anampelekaaa. Ikawa baada ya kuacha kazi akaacha kujificha tena, akawa anaenda kuchukua dawa Mnazi mmoja, mchana kweupeee, anaenda tour za mashuleni hizi na NGO kuwafundisha wanafunzi kujikinga na kupima wajue afya zao, akawa na maisha mengine

Huku Linda tour ikafika, Wakaenda Linda, Vincencia, HOM, na junior staff wa marketing wengine. Vicencia ndo anajitia close na boss HOM. Linda kakaa na wafunga stage, wabeba fliers, hana habariii. Gari ya HOM Prado ilikuwa ina nafasi, akaamua tu kupanda double cabin ya crew. Kufika lunch wakala wote Linda akalipa cause ana hela za office. Kito cha kwanza Tanga kuzindua hio product.

Viccencia kazi hajui, hata common sense hanaaa. HOM akawa anafanya kazi za watu wawili, Viccencia kuendekeza uzuriii. Wamefika Tanga, road show ya kwanza doroooo. Katika kula akamwambia HOM, tuwakodi Baikoko wataleta watu kinomaa nomaa. HOM akaja hapanaaa, namjua sijui mtu wa agency gani tumkodi Roma Mkatoliki, casue anatokea Tanga itaja. Believe me Chriss nyingi. HOM akasema kutokana na hali ilivo mbaya he cant afford another day ilio doda. Akasema waletwe woteee.

Wakaanza Baikoko, Watu walijaaa, watu walijazanaaa, ikawa hakuna nafasi ya kupumuaaa. Mara Vicencia akawakatia mda, akampandisha Roma, sasa Hip Hop na watu wa Tanga wapi na wapi, wakasepaa, kukaanza kudoda tenaa. HOM akaingilia akasema Baikoko wapande mpaka mwishooo. Kukanoga fresh tu, mpaka mwishooo.

Ikawa usiku, Vicencia anambanaa HOM, kila dakika yuko hapaaa, hata kuliwa na boss sio hivo. Ronny nae anabanaaa hatariii, anaongea usiku kucha, mradi ajithibitishie HOM hajalala na Linda. Maiha ya tour yanachosha sio kitoto, siku hio y pili akawa kakaa tu mgahawani anapunga hewa, HOM huyu hapaaa. Akanunaaa kabla ya yote. HOM akasema nashukuru kwa yote, for saving the day. Akasema kawaida tuuu. Akaendelea kuchat na simu yake.

HOM akasema i have to admit, hii kazi ungeiweza kuliko Vicencia, i regret every day. Akamwambia you deserve each other. Basi HOM akaanza kumuuliza kwanini unanichukia, sawa mimi nili kupost ila wewe ulimtuma Joy aniambukize UKIMWI, now we are equal! Linda akashtukaa, akasema ndo Joy alivokwambia? Akasema Joy kasema mipango binafsi ila najua she is not that smart ku pull that idea on her own, and the only one who hates me and wants me dead is you, Joy hakuwa na motive ya kuniua kwa UKIMWI. Sawa nilikukosea ila na mimi what you wanted done to me is INHUMAN, kwa hio tumelipanaaa, ngoma droo. Im a changed person you know, ningeweza kumpost Joy kwenye group about HIV and you ploting together to kill me but i didnt, see. Linda akanyamaza tu kimya.

Safari iliofuata Arushaaa. Wamepiga show mpaka saa 4 usiku, Linda hakupaki sweta, akawa anajikaza tu. HOM akamwmbia chukua koti langu la suti, Linda akajikaza kisabuniii. Baridi likamkolea kisawsawa.Wakaenda hotelini, akanza kuhisi vichomi. Akaoga maji ya moto, kumbe ndo kaharibuu. Akaanza kuhisi anabanwaaa mbavuuu. Mmmmh! Akajikaza, hali ikazidi kuwa mbayaa Akawaza pale ana watu wawili 2 hotelini Viccencia na HOM wote quinini kwake, akasema ngoja niende Hospital mwenyewe, akaita room service akamwambia yule kaka amuitie tax. Akawa katoka na blanket, kutembea hawezi, anatetemekaaa. Room service akamuuliza utafika kweli hospitali? Waite wenzio. Akasema hapana nitafika.

Yule dada wa mapokezi akapiga kwa HOM, mwenzenu huku ana hali mbayaa sanaa anenda mwenyewe hospital. HOM akasema nakuja hapo. Basi ndo kumkimbiza hospital na nini, akapata tibaaa. Waka kaa mpaka saa 10 usiku, HOM yupo nae ndo baba yake ndo mama yake mda huo. Sasa kumi na mbili asubuhi wakarudi hotelini, HOM anamzingua STILL MAD AT ME? After everything. Hahahaaa! Linda akachuna tuuu. Basi akamwambia Ronny kaumwa, Ronny akapanic.


Yeye lala huku, dada Asha anampigia akwambia wewe umemtuma Ronny HR? Akamwambia sijamtumaa kwani vipi? Akamwambia mwenzio kaenda kumpigia magoti sio metaphor, kapiga magoti chini kabisaa sakafuni kwa yule dada wa HR urudishwe. Hali yako mbaya sanaa. HR akamuuliza HOM, HOM akagomaaa kwamba ni vchomi tu sio big deal uko fit kuendelea na tour

Akatoka hapo Ronny kaenda kumpigia magoti chini kabisaaa mwanaume mzima anapiga magoti kwa Head wa CS yule mama wanayelumbanaa, akamsujudia kabisaaa amuombe HOM akurudishee. Ujue kumsujudia binadamu mwenzio tena mwanamke afu yeye mwanaume sio kitu rahisiii. Basi shoga zangu ndo wamenipashaa nimekosa la kusemaaa. Nimesikitikaa tu

Dada Asha akae ndelea kusema Ronny amenifanya niitake CIMA kwa kasi sanaa, manake maisha haya ukilegea utasujudia wtu kila sikuuu, sasa utafanyajeeee! Cheo huna, hela hunaa, ana pumbu zake tu, ikabidi tu msujudie banadamumwenzie mwanamke! Hahahahaaaaaaaaaaaa! It is not a laughing matter and i am ashamed of myself ila tujifunze kitu Linda, kazini usiwe mtu mdogooo.

Linda machozi yakamtiririka tu, akaapa yeye kwa gharama yoyote atakuwa HOM, ili yeye wala Ronny wasimsujudie mtu tenaaa.

ITAENDELEA KESHO SAA 5.
 
dk 6 zishakata, asee fanza mambo basi
Dk 10 izo zishaenda af Lara 1 hajatokea bado. Hii alosto nomaa. Pamoja kwamba nasinzia lakini ntasubiri mpaka nione mwisho wake. Lara 1 ukiamua leo naweza kesha na wewe
Naaam Lara 1, kama uliniita vile??...... Au nshaanza kuota??
Lara1 tupo na wewe vipi hushushi mzigo nini. Uzuri mapopo tupo
........................................................................
Hmmmmmm iyo avatar kidogo niingie uvunguni mwa kitanda......mambo lakini?
Nimekujaaa
 
lara 1, naomba kuijua style ya iphone six ndio ipoje.. Npm kama ni ya kiutu uzima zaidi na haifai hadhara.
Hahaaaaaa! Hio ukipewa bila kushurutishwa na MTU yoyote. Ukiwa Na akili zako timamu utaingia Dukani kulipia IPhone Six Plus Na kwenda kumuhonga aliekupa hio style. Ni hatari sanaaa. Weka mbali Na wallet
 
Back
Top Bottom