"The torch on kilimanjaro" kitabu cha baba wa taifa kwa shule za msingi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
''THE TORCH ON KILIMANJARO'' KITABU CHA SHULE ZA MSINGI KINACHOELEZA HISTORIA YA MWALIMU NYERERE WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

OUP walialika waandishi wa Afrika ya Mashariki kupeleka miswada yao kwao kwa ajili ya mradi wa vitabu vya historia kwa shule za msingi.

Nia ilikuwa kuwafunza wanafunzi lugha ya Kiingereza pamoja na historia za nchi zao.

Vitabu karibu 15 vilichapwa kutoka Kenya na Uganda lakini kwa bahati mbaya hapakuwa na mswada hata mmoja ulioandikwa kutoka Tanzania.

Jambo hili liliwahuzunisha OUP.

Hapo ndipo waliponiomba niandike kitabu kuhusu harakati za Mwalimu Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Niliwafahamisha kuwa sijawahi kuandika kitabu cha watoto lakini wao wakaniambia wako tayari kunielekeza ili kipatikane kitabu cha Mwalimu Nyerere kwa ajili ya shule za msingi za Tanzania na Afrika ya Mashariki.

OUP walinifunza namna ya kuandika vitabu vya watoto na ndipo nikaandika kitabu hiki kwa muda mfupi na nikawapa mswada na wakachapa kitabu hiki, ''The Torch on Kilimanjaro."

Kitabu kilifanyiwa uzinduzi Kilimanjaro Kempinski hafla ambayo ilihudhuriwa na maofisa waaandamizi wa Wizara ya Elimu, walimu wa shule za msingi, na wauza vitabu na kila aliyehudhuria hafla ile alitunukiwa nakala ya kitabu.

Kitabu hiki kimekataliwa kuwekwa kwenye mtaala wa Tanzania.

OUP wameniambia hawajui nini sababu yake ingawa kitabu kimekidhi viwango vyao vyote vya ubora.

Kwa kuwa mswada huu haukufaulu kutiwa kwenye mtaala wa Tanzania, OUP ambao waliniomba niwape mswada makhsusi kwa ajili ya Zanzibar na nikawapa waliamua kusitisha kuchapa kitabu hicho.

Kitabu hiki, ''The Torch on Kilimanjaro,'' kimewekwa ndani ya nyumba ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Magomeni ingawa wanafunzi wa shule za msingi waliokusudiwa kukisoma hakijawafikia kutoka mwaka wa 2007 kitabu kilipochapwa.

Picha: 1. Watafiti wa Kumbukizi ya Nyumba ya Mwalimu Nyerere wakikiangalia kitabu, ''The Torch on Kilimanjaro,'' (2007) First Edition 2.Mohamed Seif Khatib katika Uzinduzi wa Kitabu, ''The Torch on Kilimanjaro,'' Kilimanjaro Kempinski Hotel kulia kwake ni Sheikh Abdillah Nassir aliyepata kuwa Managing Director wa OUP 3. Mwandishi katika sherehe ya uzinduzi wa kitabu.4. ''The Torch on Kilimanjaro (2015) Second Edition.
Screenshot_20201125-121209.jpg
Screenshot_20201125-121308.jpg
Screenshot_20201125-121352.jpg
Screenshot_20201125-121329.jpg
 
Back
Top Bottom